Dar: Majambazi yapora na kuua

Dar: Majambazi yapora na kuua

JAFE

Senior Member
Joined
Sep 1, 2012
Posts
191
Reaction score
42
Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi muda mchache uliopita na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea leo saa 11:16 jioni inavyosemekana mdada huyo alikua akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.

Mpaka tunaingia mitamboni hakuna habari yoyote ya kukamatwa kwa wahalifu hao.

Kwa hisani ya audifacejackson blog
 
Sijui tunakwenda wapi,
Hizo hela haziwezi kuwafikisha hata wiki moja watakuwa wamechacha tena
R.I.P
 
Dah! Very sad jamani. RIP dada! Haya ndio mambo ambayo serikali kupitia vyombo vyake vya usalama vilitakiwa vitumie nguvu za ziada kuwatia nguvuni wahusika na sio blah blah za akina Mulungo kwa Lema huko Arusha.
 
R.I.P madam.Wafiwa poleni sana,Mungu atalipa
 
Naomba pia tusiwadharau M23,kama taifa tuweke siasa pembeni kwa sasa tushirikiane kuhakikisha nchi yetu inakuwa salama wakati wote,tutowe taarifa kwa kila dalili itakayo kuwa inatilia mashaka usalama wetu.
 
Watakuwa M23 hao kama walivyofanya kule
 
eh MWENYEZI TULINDE NA MAJANGA HAYA YATUEPUSHE MBALI RIP DADA NA WAFIWA WOTE HASA KATIKA KIPINDI HIKI KIGUMU.
 
habari ya leo j2 au jana?. sina uhakika kama crdb wanafanya kazi j2. nahofia itakua ni ile ishu ya jana ya marehemu mwasiti r.i.p.mia
 
Mungu mlaze mahala pema peponi mja huyu inaumiza sana.
 
M23 ? acheni kula vinyec nyie wadanganyika, hii ni habari ya jana au juzi kama sikosei...na haya ni matokeo ya sera ya Magamba eti vijana wajiajiri kwa kuendesha Toyo, sasa hakuna alie salama/
 
weka taarifahapa kama ulivyofanya otherwise usingezileta hapa, mambo ya audiface tangaza
 
Back
Top Bottom