Dar: Majambazi yapora na kuua

Dar: Majambazi yapora na kuua

Majambazi yapora mama mmoja kiasi cha shilingi milioni kumi muda mchache uliopita na kutokomea kusikojulikana. Tukio hilo limetokea leo saa 11:16 jioni inavyosemekana mdada huyo alikua akitoka benki ya CRDB tawi la Uhuru ambapo majambazi yakiwa na pikipiki yalikua yakimfuatilia, alipotoka tu wakaligonga gari lake makusudi ndipo dada huyo
aliposimama ili angaalie nani kagonga gari yake ambapo jambazi mmoja alishuka na kumpiga risasi ya kifuani na kutokomea na kiasi hicho cha pesa.

Mpaka tunaingia mitamboni hakuna habari yoyote ya kukamatwa kwa wahalifu hao.

Kwa hisani ya audifacejackson blog

R.I.P mdada , huku tunakoelekea sasa ni unyamani, naona utu tumeuvua na kubakia wanyama sasa watanzania
 
wabongo tuamuke tuache ushabiki lacvo c muda misri hii hapa nyie subirini tangu lini kiwete akaongoza umati wawatu lazma wapotee.
 
Sijui tunakwenda wapi,
Hizo hela haziwezi kuwafikisha hata wiki moja watakuwa wamechacha tena
R.I.P
Chris Lukosi, ndiyo maana huwa nasema unahitaji kuwa na kichwa cha mwendawazimu ili kuweza kuishabikia CCM. Yaani serikali ya CCM, usalama wa Taifa na polisi wapo busy na CHADEMA, na kusahau kabisa jukumu lao la kulinda usalama wa raia na mali zao. Wamesahau kulinda fedha yetu na rasilimali zetu za nchi. Kwa kweli mtu mwenye akili timamu akisimama na kuwashangilia wahuni hawa ni lazima watu wote tumshangae. Halafu usishangae huyu dada naye alikuwa ni mmoja wa mashabiki wakubwa wa CCM. Msisahau kwamba haya ambayo CCM wanafanya hayatuumizi CHADEMA au wasio na chama peke yao. Yana backfire haya mambo. So kindly please watanzania tuungane kuukataa utawala wa waganga njaa hawa. Watatumaliza.
 
Last edited by a moderator:
R.I.P mdada , huku tunakoelekea sasa ni unyamani, naona utu tumeuvua na kubakia wanyama sasa watanzania

Mtoa taarifa, naomba uwe na uhakika na unachokiandika kwa kuangalia tukio lenyewe ni kubwa sana. CRDB uhuru/ Kariakoo hawafungui jpili. Kwa maana hiyo hakutokea CRDB Bank. Hata kama ni kwenye ATM, atachukuwa Milioni moja tu na sio kiasi ulichokitaja.

Chunguza chanjo chako vizuri, usipende kukurupuka tu.
 
Leo J.pili bank gan ilikuwa wazi mida hyo ya saa 11,,afu ATM mwisho Laki 5,vp hiyo Mil.10 imetokajetokaje,,!!??
 
R.I.P Mwasiti. Tutakukumbuka kwa ucheshi wako na upendo wako. Halafu na wewe unaeleta masuala ya siasa kwenye vifo acha hizo ni ufinyu na uchanga wa kisiasa. kwani marekani watu hawauliwi? hakuna majambazi?
 
tuilaumu serikali ilioshindwa kuborsha maisha ya kawaida ya Mtanzania
tungesimamia wenyewe madini yetu,utalii,gesi lazima kila kaya kwa mwezi wangelipwa sio chini ya laki moja
umaskini kama huu ungetoweka
kuna nchi ina mafuta na gesi ulaya wananchi wake wanalipwa kila mwezi kwa wasio na kazi
sisi tumeshindwanini wakati tuna utajiri mkubwa kuliko wao?
CCM wanafaid tu wenyewe
nashauri majambazi fuateni hao wezi na mafisadi .sie maskini tuacheni,
nawalaumu kwa kuuwa wangechukua na kusepa tu nadhani majambazi hao sio wa Dar.

NB: mleta mada nashauri uitoe picha ya marehemu hapa
ana haki ya kusitiriwa,tumtendee haki huyu dada.
 
Hii ndiyo habari ile ile tuliyoipokea awali paka JF ya dada mmoja akiitwa Mwasiti aliyeuawa kihivi wikiendi hii hii au hii habari nyingine?

Maana nayo ilitokea maeneo ya Kariakoo inanifanya nifikiri labda hii ni muendelezo ha habari ile ile, ikiwa ile ya kwanza ilitolewa kama breaking news na hii imepata muda zaidi.

May all beings attain enlightenment.

May all employers use armoured services.
 
dah, yalikuwa hayana haja ya kuua. lets hope watayakamata. r.i.p mdada.
 
Si rahisi siku hizi unachukua hela kwa siri tu halafu mtu atambue.
Siri iko wapi hapo? Ukienda benki utaona watu wana cash mamilioni na mamilioni wanaondoka nayo kwenye vifuko vya rambo wengine, mi nishaona mtu kapeba kiburungutu kama cha dola kama 20,000 CRDB town hapo hadi nikashangaa, sasa jambazi atashindwa vipi kwenda kumsubiri nje? Kwenye vi bureau de change navyo ni hivyo hivyo, watu wana cash mamilioni bila kuogopa, mi huwa nashangaa sana.

Tujifunze kutumia zaidi malipo ya hundi, ambayo zaidi ya kuwa na usalama kidogo, pia yana rekodi.
 
Yani inasikitisha sana

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom