Dar inawapotezea watu muda

Nilikaa miaka miwili na nusu mikoani lakini sikuwahi ona jambo la maana hela zenyewe hakuna, yani watu hawanywi hata soda aisee na wakinywa soda ni kwenye sherehe aisee, tangu nirudi Daslama nateleza tu kama maji...
 
Hiyo elfu kumi dar unaipataje kirahisi?
 
Hio ni wewe na mipangilio yako. Mimi naondoka saa mbili asubuhi saa tatu kasoro niko kibaruani. Kurudi hivyo hivyo 45mins tu.
inategemea na mahali unapokaa kuna watu wanachukua masaa hata matatu kwenye foleni... Dar kero tupu
 
Katika utafito wa NBS Mwanza ni moja ya mikoa yenye maisha ya dhiki kwa wakazi wake hapa nchini.
 
Jibu langu lilianza na 'hio ni wewe' maana yangu yeye ndio anaamka saa kumi alfajiri sio wote
inategemea na mahali unapokaa kuna watu wanachukua masaa hata matatu kwenye foleni... Dar kero tupu
 
Nilikaa miaka miwili na nusu mikoani lakini sikuwahi ona jambo la maana hela zenyewe hakuna, yani watu hawanywi hata soda aisee na wakinywa soda ni kwenye sherehe aisee, tangu nirudi Daslama nateleza tu kama maji...
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]hawanywi soda
 
siku hizi heshima pesa.... we rudi mkoani huna pesa uone kama kuna mtu atakuwa na time na wewe
 
U
Sitake kufanana na wengine mkuu.Wewe umemudu hayo maisha kutokana na aina ya shughuli unayofanya,pia bila shaka huko ulikuwa na vitu vingi ulivyosaidiwa na ndugu au wazazi.Kama ni biashara Dsm inashawishi zaidi kuliko mikoani maana wateja ni wengi zaidi na ongezeko la faida ni la haraka.
 
Dar kinachokera ni foleni na lile joto..Yaani muda wote akili iko juu juu tu huna muda wa kurelax...
Pole mkuu, joto kali ni kuanzia December, ila miezi hii na kurudi hadi wa sita hali sio mbaya. Foleni ni sifa ya jiji lolote kubwa si London,si New York....labda ukae huko huko mikoani na vijijini. Ku-relax ni mipangilio yako tu.
 
Mwanza nalo ni jiji kwani? Umeshajibiwa Kwa takwimu za NBS Mwanza wanaishi Kwa maisha ya dhiki hata Pato lake ni dogo ukilinganisha na Dar
 
Tatizo ni huyo mwenye kajumba anaposema mwenzie kapanga na maisha ye katoboa.Tena anaanzisha na thread kuwa watu waache kupanga waende kuishi kama yeye anavyoona inafaa. By the way kati ya vipofu mwenye chongo huonekana mfalme
 
Tatizo watu mmekariri maisha
 
Kumbe wengi sasa hivi mmeshajua hii kitu...Dsm unaweza ishi miaka mingi lkn usiwe na mafaniko hata kidogo!
Popote pale waweza ishi miaka nenda rudi na usiwe na mafanikio hata kidogo.Kuna sehemu Kijiji kizima wameshindwa kujenga choo cha zahanati.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…