Hakika umesema ya kweli, nilikaa miaka 8 bila bila, kodi, usafiri, chakula, kuamka na kurudi mida mibovu, joto lisilo rafiki na mtu. Ila tangu ning'atuke nashukuru kwamba maisha haya ya sasa ningeishia kuyaona kwa wengine tu! Sitaki kusema nina nini na nini, ila amini kuacha maisha ya Dar na kuamua kuja mkoa, hakuna hata rafiki aliye kubaliana nami, sasa 'gap' halizibiki tena labda awe fisadi tu! Ukweli mchungu, ila watu ambao tuliwaacha mikoani ndo huja mara nyingi kununua magari huku sisi tuliokua wa 'mjini' tunawakwepa. Mwenye macho haambiwi tazama.