Dar inawapotezea watu muda

Dar inawapotezea watu muda

Nimeishi Dar kwa takribani miaka 13,hakuna cha maana nilichokifanya,ila niliporudi mkoani ndani ya mwaka mmoja maisha yalikuwa tofauti kabisa. Niliacha kufikiria mawazo ya muda mfupi mfano nitakula nini kesho,kodi itakuaje na mengineyo ya kipuuzi..

Sasa hivi nawaza itakuaje baada ya mwaka au miaka kumi nitakuwa wapi. Hilo Dar linaishia kwenye maneno tu,maisha ya Dar yanamfanya mtu awe mtumwa,wana wengi wanaogopa kurudi mahome kwao kwa kuhisi watadharaulika.

Acha fikra potovu rudi ubadili namna ya kufikiri,huku mambo yanaenda ukitia nia.
Jpm alisema mnaita 500 jero mtaiita jina lake halisi.asantehh kwa kutupa mlejesho kwamba umerudi mkoani
 
Jpm alisema mnaita 500 jero mtaiita jina lake halisi.asantehh kwa kutupa mlejesho kwamba umerudi mkoani
Sikuondoka kipindi cha jpm,kipindi cha kikwete,halafu nimegundua tunatofautiana kudefine maisha,mimi nayaona mabovu wenzangu wanayaona mazuri,nadhani ni nature na upeo...tafsiri nyingi nazoziona za maisha ya chini kabisa....unaota kuwa na nyumba na gari moja au mawili mimi naota niwe msaada kwa watu zaidi ya 300 na kuendelea,ukiwa na upeo mkubwa utanielewa.
 
umekaa kwenye masofa ya mama mdogo hapo,unapumua tu hujui dunia inakokwenda,unategemea akili ifanye kazi kweli?
Jpm alisema mnaita 500 jero mtaiita jina lake halisi.asantehh kwa kutupa mlejesho kwamba umerudi mkoani
 
Hakika umesema ya kweli, nilikaa miaka 8 bila bila, kodi, usafiri, chakula, kuamka na kurudi mida mibovu, joto lisilo rafiki na mtu. Ila tangu ning'atuke nashukuru kwamba maisha haya ya sasa ningeishia kuyaona kwa wengine tu! Sitaki kusema nina nini na nini, ila amini kuacha maisha ya Dar na kuamua kuja mkoa, hakuna hata rafiki aliye kubaliana nami, sasa 'gap' halizibiki tena labda awe fisadi tu! Ukweli mchungu, ila watu ambao tuliwaacha mikoani ndo huja mara nyingi kununua magari huku sisi tuliokua wa 'mjini' tunawakwepa. Mwenye macho haambiwi tazama.
 
Hapa tunachanganya vitu viwili kwa wakati mmoja,,mtu anayetafuta maisha DAR,,wakati huo huo wazazi wake wanamijengo dar,,na mtu anayetoka mkoani,,kuja kutafuta,,,,huku wazazi wake wakiwa hawana asset yoyote dar,,hapo kuna tofauti kubwa ya maumivu yautafutaji,,,,,,chamsingi,,nikutokukata tamaaa,,maisha kokote
 
ubarikiwe

huko uliko mkuu, yani hapo dar kuna wajinga sijawahi ona , eti jitu linakuja huku linasema dar kuna magari mazuri na majumba mazuri wakati hapo anapolala kwenyewe ni patupu na mbanano,
unakuta mtu ana simu kubwa kama tv eti ni ya kuingia nayo instagram na wasap kumcheki mange kasema nini, sasa mtu kama huyo utasemaa ana akili kweli
 
Back
Top Bottom