Dar inawapotezea watu muda

Dar inawapotezea watu muda

Baba yangu Mkubwa Anaish Dar mwaka wa 28 huu ndo msomi zaid na mwenye kipato kikubwa zaid ndan ya familia ila ndo maskn zaid kwenye familia yao.

Sitak kuweka maelezo meng Jitahd hvyo hvyo tu unielewe
Tumekuelewa
 
nyinyi ni waoga wa maisha, maisha popote, kama umeamua kurudisha mpira kwa kipa ni mpango wako kivyako vyako, wengine tumetusua na tunaendelea kutusua hapa hapa bongo daslamu
Wanaotusua wanasemaga,umetusua una kiwanda cha nguo...au una nini cha kutuambia umetusua kwa dar,halafu pengine wakati sisi tunatoka dar nyie ndio mnaingia bado dar unaiona ya moto
 
Ninyi nyote kwa kifupi mawazo yenu ni finyu na uwezo wa kutoka ndani ya kundi la wajanja hamuwez, kwa kifupi mnarudi kwenye ule msemo wa kizamani kwamba jogoo wa shamba.....niwaulize mnawaza habari ya eti kodi ya nyumba, chakula maji, kwa hio huko mikoani kuna nyumba za bure? Kama kamji kadogo namna hii mnaona ni kupoteza muda inakuwaje ungetupwa jiji kama NY, Milan ama London ukaambiwa utafute connection mtoboe? Wasema Dar ni kupoteza muda lakini tambua nyumba nzuri kushinda zoote Tanzania iko Dar, viwanja vikal viko Dar, Tajiri namba 1 Tanzania yuko Dar, hata gari ya kifahari nchi nzima inaendeshwa Dar..nyie endeleeni kukusanya matembele huko na kujigamba mnamilik nyumba huko ambayo ukiileta dar itathaminishwa na ilioko tandale
Mkuu umesahau na mademu wakali na wasafi wapo dar
 
Ww maisha yalikushinda...
Sibishi babu,ndio maana huku niliko nimeyapatia...wewe kuingiza pengine 30,000 kwa siku inakupa ujeuri,hahhaa kuna watu wakawaida kabisa anaingiza hadi laki kila siku kama faida na inakaa tu bank,sasa 30 yako inakod,ina kuhonga,ina chakula unabakiwa na nini hapo
 
Ukiegemea kwenye hesabu za probability, uwezekano wa kutoboa ukiwa Dar ni mkubwa kuliko mkoani. Magari na majumba mazuri yako Dar. Mkoani mtu anayetembelea shangingi ni mkuu wa mkoa pekee, whats ur chance of getting one?
Halafu wewe wa zamani, kweli hao wenye hayo mashangingi dar wanapiga deal gani kama sio 90 parcent ni wa serikalini tena enz za jakaya...hujatembea muda kweli....halafu mbona kitu kidogo sana umezungumzia....nilidhani angalau mtu ana kiwanja chenye hati ekari 100/huko nyumba 20 kuendelea....
 
Siwezi kuingilia hapa, Muda ni mali kwangu, Dsm siwezi kuishi mateso na taabu nyingi,

Hivi unaishi kwenye nyumba ya kupanga una kaIST/PASSO na mtu alie mkoani mwenye chumba na sebule ya kwake na shamba na kiwanja zaidi, nani mjanja??
.DSM maisha magumu sana, Vijana wengi kazi yao ni kupamba mageto yao tuuuuu hakuna la maana zaidi
 
Siwezi kuingilia hapa, Muda ni mali kwangu, Dsm siwezi kuishi mateso na taabu nyingi,

Hivi unaishi kwenye nyumba ya kupanga una kaIST/PASSO na mtu alie mkoani mwenye chumba na sebule ya kwake na shamba na kiwanja zaidi, nani mjanja??
.DSM maisha magumu sana, Vijana wengi kazi yao ni kupamba mageto yao tuuuuu hakuna la maana zaidi
 
Baba yangu kazaliwa dsm mama yangu kazaliwa dsm mimi mwenyewe nimezaliwa dsm nimekua na kusomea dsm dsm ndio kama kijijini kwetu kwamaana mimi ni mtoto wa kizaramo kwa sasa nimetoka dsm naishi morogoro mwaka wa tatu sasa na jishughulisha na kilimo cha mabostani ya matunda na mboga mboga ni duka la kuuza na kukodisha baiskeri pia nimefanikiwa kujenga nyumbani dsm nyumba ya vyumba viwili sebule jiko choo na stoo napia kumfungulia mdogo wangu salon ya kiume.
 
Issue ni wewe umepoteza muda Dar ukiwa unashangaa shangaa, siyo Dar imekupotezea muda. Sasa ukiwa miji mikubwa kama NY, Tokyo, London au Jo-burg si ndiyo utafutwa kabisa kwenye ramani ya ulimwengu. Jipange kijana.
Kwani hayo majiji uliyoyataja yapo tanzania,tunazungumzia kwetu ndio maana ni dar na mkoani
 
Acheni upotoshaji na kuongea kwa kukariri,hivi unazijua systems za hayo maeneo unayoyataja?
huko hakuna ujanja ujanja,wala miundombinu yake sio mibovu kama ya hicho kijiji kikubwa,kule unafika mishe kwa wakati na kazi zinafanywa kwa kupata trainings,tena unaweza hata kufanya kazi mbili sehemu mbili tofauti bila shida,na si kazi zenu za viwandani,unamenyeka nguvu zako afu unalipwa elfu nne kwa siku afu unakuja kutamba hapa kuwa nipo dar napambana,huo ndio ujinga alioukataa mleta uzi,hana chuki na mtu,anajaribu kushare mazuri na tofauti aliyoi`experience baada ya kutoka dar,mtu unapoteza masaa 4 upo barabarani unaenda kibaruani,kibarua kisicho hata na tija zaidi ya kununua tecno na kuja kupost utumbo hapa,kinachozungumzwa na mtoa mada si kwamba mikoani ndio kila mtu kafanikiwa,ila anazungumzia possibility ya mafanikio mkoani ni kubwa kwa mtu mwenye nia ya kusogea mbele kimaisha ukilinganisha na nyie msio na cha maana mnachokifanya hapo zaidi ya kujipa matumaini ya kutoboa kisa magari mazuri yapo Dar,nimesikitishwa kuona kuna watu bado mnapima maendeleo kwa kuangalia majumba na magari bila kujipima maisha yenu binafsi yana unafuu gani kwako na kwa familia yako directly,hao wenye magari mazuri na nyumba nzuri wewe unanufaika nao vipi?ni aibu kwa mwanaume kuwa na fikra mfu kiasi hicho,toa hoja za kujenga mkuu...shame!
Afadhali bwana hadi nimetetemeka kwa kuwaelewesha vizuri mkuu,watu bwana....
 
Sibishi babu,ndio maana huku niliko nimeyapatia...wewe kuingiza pengine 30,000 kwa siku inakupa ujeuri,hahhaa kuna watu wakawaida kabisa anaingiza hadi laki kila siku kama faida na inakaa tu bank,sasa 30 yako inakod,ina kuhonga,ina chakula unabakiwa na nini hapo
ongeza sifuri moja...kisha kwenye tatu weka nne.....Kwa masaa 12
 
"Nimesema lazima uzeeke huna kitu" yaani mpaka unafika uzee usipokuwa makini huna hata pakuweka ubavu sijamaanisha kuwa utazeeka kwa shida ya kutafuta dar maana pesa zipo kila sehemu tatizo dar kila kitu cha kununua na gharama kubwa

Kwaiyo unataka vitu vya bure ?
 
Acha zako mkuu usitufanye mazuzu humu mimi nimekaa Dar miaka mingi , Tandale zile ni nyumba au slums we jamaa muongo sana , mitaa michafu , plan ya ovyo kabisa na kwa taarifa yako Dar es Salaam maeneo yaliyo staarabika ni machache mno mengi yapo nje ya mji asilimia 70 ya wakazi wa Dar wanaishi kwenye slums halafu nao wanatunisha mabega eti mi wa Dar , nonsense kabisa mwambie akuoneshe anapokaa sasa .......ptuuu

Nyie watu ni arrogant sana ila wengi wenu mnaishi maisha ya taabu sana

Ww unawachukia watu wa dar kutoka moyoni lakin wadar hawana time na ww wamkoan coz ww unajua wanakudharau lakin iyo ni hali uliyojiwekea ww kutokana na watu uliosoma nao shule za boarding na chuo
Dada dar ndio jiji la kwanza Tanzania
Iyo slums ya tandale inasamani sana kuliko iyo nyumba yenu mkoan coz land position iyokuwepo iyo nyumba ni dar karibu na mjin
Umeona zile slump za kipawa zilivyo kuwa mbovu lakin walivyofunja kwa kutanua airport watu walilipwa ela nyingi sana coz ni dar siyo mkoan sasa ww cheka nyumba ya mchikini kariakoo ilivyo kuwa mbovu ngoja auze utaona mpunga anaochukua ndio utajua kuna dar na mikoan
 
Back
Top Bottom