Dar inawapotezea watu muda

Dar inawapotezea watu muda

Sio kila mtu atakubaliana na wewe. FYI im not your typical Dar dweller. Kwahio hio typical mindset yako ni wewe na wenzio hainihusu ndio maana mawazo yako na yangu yanapishana.
Si matarajio yangu kuwa kila mtu akubaliane na hoja zangu, nimesema hizi ni mindset zetu watu wa dar nikiwa najua kabisa , the way unavyopinga kila kitu na kutetea ndivyo nimeishi hiyo Tabia kwa takriban miongo mitatu hapo dar naijua fika and you just belong to the same group.

Ona unavyotetea kuwa wewe huchukui muda kutoka na kurudi home , ona unavyotetea kuwa dar hakuna joto ati joto la dar ni miezi mitatu tu, ona unavyotetea foleni hata new York ipo, mi sijafika new York ,ila naamini hakuna foleni ya Massa mawili gari haisogei, kama foleni ya buguruni hapo.
 
Baada ya kutoka dar nikaja kugundua vijana wengi niliowaacha dar nikikutana nao wanachojua tu ni majina ya pombe kali mpya mpya+viwanja/club mpya+majina ya magari expensive lkn ukiwauliza zile ndoto kubwa kubwa mlizokua nazo wkt mnasoma wanakwambia maisha ni haya haya chief tule maisha tu.

Nadhani wanakua wameshaona kwa maisha ya dar ndoto hizo ni ngumu kufikiwa .
 
Maisha yana ma gap balaa wkt hapa kuna watu jiji limewashinda na wamerudi mikoani na wengine wanaona kuishi dar ni kama peponi lkn wakina Joseph Kusaga wameona dar ni kijiji cha wavuvi(according to bbc) wameenda kuishi Dubai huko na familia zao.

Hayo ndio maisha.
 
Huyo anaeingiza elfu hamsini kwa siku huyo si tajiri wa kutupwa.ndani ya wiki atakuwa kama na laki 3.kwa mikoani huyo anamaliza yote.tajiri namba 1 wa mji mzima.kiufupi maisha yawe ya mikoani au Dar. Ukiingiza 15 kwa siku wewe umetoka kimaisha.wengi huwa wanaishia kupata buku 5 siku ikiwa powa buku 10 kwa siku.Ukipiga dili ukalipwa 15000 au 20000 yani siku hiyo utachoka balaaa ni kazi ngumu sana.Kiufupi Tanzania yote maisha ni magumu sana.Labda uishi kijijini kabisa.Huko kuna angalau na ukiwa kijijini ukubali kuishi maisha ya ukijijini.Maisha yetu watanzania yanasikitisha sana hasa vijijini.Nimekaa morogoro.Mbeya,Dar,Songwe nimepita Njombe ,Iringa,pwani.Kwa kweli maisha ni duni sana. Yani tunaishi kwa neema tu.Dar kuna wabongo wachache wenye pesa.Ila sio pesa nyingi.Wanahela sana wenyenyumba za kupangisha Dar.Maana kodi wanakusanya kwa miezi 6.labda unakuta chumba 50,000.amepangisha vyumba nane anakuwa na million kadhaa ambazo zinasaidia kumtoa kimaisha.
Wala hata sio tajiri, ni chalii tu wa kawaida. Anakunja 50 safi ametegesha pool table zake 3 maeneo potential. Yuko zake katesh huko.
 
ukikimbia DAr wewe ni wa ajabu, Dar hata wauza mihogo kwenye foleni wanapata hela kuliko mwalimu wa huko kwenu sitimbi
Le mutuz nyenyenye nyenye kokobanga inamuweka mjini
 
Haihitaji rocket science kujua kuwa ktk miji mikubwa kuna fursa nyingi za kiuchumi kuliko ktk miji ya kawaida ilmradi uchekeche na kutumia vzr maarifa uliyonayo . Na hii sy kwa mujibu wangu wala wako ni kwa mujibu wa tafiti za kisayansi. Kwa population factor tu, ambayo Dar ndy inaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya watu around 5m+ basi ni indicator tosha ya kuwepo na economy diversification ambayo inatoa fursa mbali mbali. Yes mkoani unaweza fanikiwa, lkn ktk fursa za kiuchumi ambazo ni basic sana au kwa lugha rahisi sekta rasmi yani zile ambazo hazihitaji sophistication ya aina yyt ile. Wakati Dar kutokana na ukuaji wa technologia na wingi wa watu ambao ndy rasilimali kubwa, unaweza toka kwa kufanya biashara ya kawaida sana mfano tu " kufungua online used items shop" " ukafanya biashara ya delivery ya products mbalimbali kitu ambacho mkoa vinafanyika kwa uchache au hakuna kbs kwasababu ni ngumu kumshawishi mtu alipie extra amount ya elfu 3000 au zaidi ili umfanyie delivary ya kitu flan....kiafya ni salama zaidi kutibiwa ktk haospitali za Dar sabb ya uwepo wa madaktari bingwa wengi, wewe mwenyewe hapo ukiuumwa lazima uje Dar kupata huduma bora ya afya...na ndy sababu big cities kama New York , London, Tokyo, Moscow nk kuna idadi kubwa ya billionaires, hii ni alama kubwa kuwa kuna fursa.
 
Mtoa maada inawezekana unahoja,lakini sio kila jambo zuri bhasi litamfaa kila mtu,kuna watu mkoani hawakufanikiwa na dar imewatoa,lakini pia inategemeana na kazi au shughuli zako unazofanya ndio zitatathimini ukae dar au mkoa.
 
Hahah eti kuchonga miwa,ungechukua nafasi hii kuwaambia vijana wa mkoani wakitaka kuja dar kufanya biz waje na mtaji wa kuanzia kiasi gani,hahah.
Vijana wa mikoani waende tu Dar, ikiwachemsha warudi makwao. Fursa ziko over exploited na biashara ziko na intense competiton sana kwa Dar uzuri hutokosa wateja kabisa. Wajanja ni wengi na pesa ni nyingi. Biashara ili iwe na muonekano mzuri ni mamilioni ya pesa sasa wewe mwenye business ya kishamba unatoboeje?
 
Mtoa maada inawezekana unahoja,lakini sio kila jambo zuri bhasi litamfaa kila mtu,kuna watu mkoani hawakufanikiwa na dar imewatoa,lakini pia inategemeana na kazi au shughuli zako unazofanya ndio zitatathimini ukae dar au mkoa.
Hilo la aina ya shughuli mtu anayofanya unaeza kweli ikawa ni sababu,
Inaezekana tunabishana humu kumbe mtu Dar anafanya shughuli ambayo mkoani haina fursa , hawa tunaita the selected few,
Ila kama unazungumzia majority ya average Mtanzania , Dar sio rafiki kutoboa, utapoteza muda
 
Nilipomaliza mafunzo yangu ya kininja nilitamani kurudishwa Dar ili kiwe kituo changu cha kazi bahati mbaya sikurudishwa Dar nikaletwa mkoa unaolima mchele aisee huku nimejikuta nafaidi fursa nyingi mno tena ukija huku kijana uliepikwa na jiji la Dar huwezi kuteseka.
Hapo sasa ndipo utakubali kuwa Dar ni kila kitu...sababu umetumia akili za kidaslam kuona fursa mkoani...kwahy usingeishi Dar nakuhakikishia usingeona hizo fursa, akili ya "mwanadaslam" huwaza vitu vikubwa ambavyo kwa wa mkoani anaona haviwezekani. Kwahy point ya msingi hapa hata kama hukupata mafanikio Dar kwa hustle zako, basi Ile exposure uliyopata ukienda itumia sehemu nyingine inaweza kukutoa
 
Kwahiyo point yako nikuwaasa wana warudi mahome tu basi ?
 
Vijana wa mikoani waende tu Dar, ikiwachemsha warudi makwao. Fursa ziko over exploited na biashara ziko na intense competiton sana kwa Dar uzuri hutokosa wateja kabisa. Wajanja ni wengi na pesa ni nyingi. Biashara ili iwe na muonekano mzuri ni mamilioni ya pesa sasa wewe mwenye business ya kishamba unatoboeje?

Daah basi ngoja vijana waje wauze supu ya pweza+vumbi la mkongo tu hakuna namna tena.
 
Hapo sasa ndipo utakubali kuwa Dar ni kila kitu...sababu umetumia akili za kidaslam kuona fursa mkoani...kwahy usingeishi Dar nakuhakikishia usingeona hizo fursa, akili ya "mwanadaslam" huwaza vitu vikubwa ambavyo kwa wa mkoani anaona haviwezekani. Kwahy point ya msingi hapa hata kama hukupata mafanikio Dar kwa hustle zako, basi Ile exposure uliyopata ukienda itumia sehemu nyingine inaweza kukutoa

Baada ya kutoka dar nikaja kugundua vijana wengi niliowaacha dar nikikutana nao wanachojua tu ni majina ya pombe kali mpya mpya+viwanja/club mpya+majina ya magari expensive lkn ukiwauliza zile ndoto kubwa kubwa mlizokua nazo wkt mnasoma wanakwambia maisha ni haya haya chief tule maisha tu.

Nadhani wanakua wameshaona kwa maisha ya dar ndoto hizo ni ngumu kufikiwa .

Ukisoma hiyo post yangu ndio utajua vijana wa dar wameshakata tamaa na hizo ndoto kubwa kubwa.
 
Hiyo elfu kumi dar unaipataje kirahisi?
Easy tu mkuu, chukua machine yako ya kutengeneza bisi mpe kijana pale ferry anakuletea 15k kwa siku....ongea na taita pale maeneo ya posta omba uweke kijiwe cha shoe shine weka kijana toka Moshi au komaa mwenyewe kwa siku hukosi elfu 20k...unataka nyingine, haya fungua kibanda kipambe na picha nzr za juice, fanya branding ya glass za juice, tafuta mrembo mmj matata sana mvalishe polo shirt yenye nembo yako ya "athuman healthy juice" awe anazunguka maeneo jirani kusaka wateja kwa smile kwenye bashasha kisha weka maeneo watu wengi kama makumbo kituo cha mabasi, ubungo, au mbezi mwisho........sasa jaribu hayo niliyotaja mkoani kama hata utaweza ingiza elfu 5 kwa siku.
 
Nimeishi Dar kwa takribani miaka 13,hakuna cha maana nilichokifanya,ila niliporudi mkoani ndani ya mwaka mmoja maisha yalikuwa tofauti kabisa. Niliacha kufikiria mawazo ya muda mfupi mfano nitakula nini kesho,kodi itakuaje na mengineyo ya kipuuzi..

Sasa hivi nawaza itakuaje baada ya mwaka au miaka kumi nitakuwa wapi. Hilo Dar linaishia kwenye maneno tu,maisha ya Dar yanamfanya mtu awe mtumwa,wana wengi wanaogopa kurudi mahome kwao kwa kuhisi watadharaulika.

Acha fikra potovu rudi ubadili namna ya kufikiri,huku mambo yanaenda ukitia nia.
Tuliwaaambia Dar mkuje na vichwa (akili) ninyi mkabeba mizigo sasa mnarudi mlikotoka hoi......tuachieni jiji letu tusonge mbele. Hapa unaweza kuanzisha kijiwe tu na ukapiga pesa ndefu...kuuliza tu 500 na kupelekwa 1000
 
Back
Top Bottom