Dar: Aliyemuua mkewe na kuuchoma mwili kwa mkaa awatisha Wanahabari

Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
690
Points
1,000
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
690 1,000
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
=====

Hamis Said Luongo(38) ambaye ni mshtakiwa wa mauaji ya mke wake, Naomi Marijani katika eneo la Gezaulole Kigamboni ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania kuwa atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambacho mahakama hiyo haitakitarajia.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo Jumanne Agosti 13,2019 mbele ya Mahakama hiyo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa Luongo alinyoosha kidole na kuiomba Mahakama hiyo kuwa kichwa chake kimechanganyikiwa hivyo atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambapo Mahakama hiyo haitatarajia.

"Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu waandishi wa habari ambao wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama, sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama hii nitafanya kitu kibaya ambacho hamtakitegemea.”

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ndani nataka akili yangu itulie lakini hawa wapiga picha wananipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitawafanya kitu kibaya ambacho Mahakama haitatarajia," amedai

Baada ya kauli hiyo, Wakili Wankyo alimueleza mshtakiwa huyo kuwa kupigwa picha ni hali ya kawaida na washitakiwa wote wanaofikishwa mahakamani wanapigwa picha na yeye siyo mtu wa kwanza hivyo awape uhuru waandishi wa habari wafanye kazi yao kuwa huru.

"Lengo la waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwajuza wananchi hivyo awape uhuru wafanye kazi yao kuwa huru na kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani," amedai Simon.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ameshitakiwa chini ya Kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kosa hilo, mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
 
MKUYENGE

MKUYENGE

JF-Expert Member
Joined
Jun 26, 2019
Messages
3,270
Points
2,000
MKUYENGE

MKUYENGE

JF-Expert Member
Joined Jun 26, 2019
3,270 2,000
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
uyo bange inamdanganya
 
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2016
Messages
3,219
Points
2,000
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2016
3,219 2,000
Hana cha kupoteza. Kuna siku atawavulia nguo zote. Bado mtampiga picha?
Cha kupoteza ni uhuru aliokuwa nao.....sahivi hawezi hata kwenda kuulizia bei ya gunia la mkaa..Jela isikie tu...hata wahenga wanasema ugali ni mtamu ila sio wa jela....
 
B

Bilakwate

New Member
Joined
Aug 9, 2019
Messages
1
Points
20
B

Bilakwate

New Member
Joined Aug 9, 2019
1 20
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
Kashavurugwa huyo ameshammiss shetani huko jehanam mahakama ifanye faster imruhusu akamsalimie shetan mwenzake huko jehanam
 
A

Adrianinho

JF-Expert Member
Joined
Mar 20, 2013
Messages
392
Points
500
A

Adrianinho

JF-Expert Member
Joined Mar 20, 2013
392 500
Hapana asidharauliwe akipata upenyo kidogo tu... Anaweza kuleta majanga makubwa.... Kumbuka hana cha kupoteza kwasasa kwahiyo si ajabu anapanga kuua tena
Hata Mimi nimewaza hivyo huyu jamaa inabidi wawe makini nae sana hata huko gerezani inabidi awekwe mahabusu ya peke yake.
 
No Escape

No Escape

JF-Expert Member
Joined
Mar 7, 2016
Messages
5,774
Points
2,000
No Escape

No Escape

JF-Expert Member
Joined Mar 7, 2016
5,774 2,000
Hapana asidharauliwe akipata upenyo kidogo tu... Anaweza kuleta majanga makubwa.... Kumbuka hana cha kupoteza kwasasa kwahiyo si ajabu anapanga kuua tena
Ni kweli kabisa,huyu ni wa kumuangalia na kumchunga sana.....hiyo kauli ya kukata tamaa.
 
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2012
Messages
10,130
Points
2,000
Crocodiletooth

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2012
10,130 2,000
possibly a man eater...
cry over their cute daughter..!
 
doup

doup

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2009
Messages
2,026
Points
2,000
doup

doup

JF-Expert Member
Joined Feb 26, 2009
2,026 2,000
Lakini bado hajapatikana na hatia. Nishasikia kisa kimoja uko ulaya watu walifake mada na kumtunia ushahidi mtu asiye husika, kwa kutokosa umakiini mahakama ilimpiga kitanzi yule jamaa baada ya muda ilijilikana ailye uwawa siye bari alijitolea tu kuthibitisha mapungufu ya mifumo yetu.

Tusubiri tuone mwisho wake.
 
mtena

mtena

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2014
Messages
1,811
Points
2,000
mtena

mtena

JF-Expert Member
Joined Jan 24, 2014
1,811 2,000
Bado hawajamfungua kitabu vizur atakuwa mpole tu let's wait and see
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
15,755
Points
2,000
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
15,755 2,000
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
Jamaa anaamini sana uchawi itakuwa. Hajiulizi uchawi kama upo imekuwaje ameishia ndani
 
abdi ally

abdi ally

JF-Expert Member
Joined
Dec 4, 2018
Messages
1,178
Points
2,000
abdi ally

abdi ally

JF-Expert Member
Joined Dec 4, 2018
1,178 2,000
Hapana asidharauliwe akipata upenyo kidogo tu... Anaweza kuleta majanga makubwa.... Kumbuka hana cha kupoteza kwasasa kwahiyo si ajabu anapanga kuua tena
Kweli kabisa yaani hapo hukumu yake kunyongwa had kufa au maisha so Hana Cha kupoteza ashajua teyar hachoki hapo katika hyo kesi

Wakimpa upenyo atamniga mtu hapo na hata huyo hakimu anaesikiliza hyo kesi awe makin awakawiii kukurupuka hafla bin vu huyu hapa
 
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2008
Messages
9,995
Points
2,000
macho_mdiliko

macho_mdiliko

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2008
9,995 2,000
That's what should be done...!!!
Umesema kweli. Asidharauliwe. Anaweza kuftuka kama risasi kutoka kwenye kizimba, tahamaki, unakuta keshavunja shingo ya mpiga picha mmoja kama pingili ya muwa. Kwa watu wataalam muda wa sekunde 30 tu wanaweza kumuua mtu tena kwa mikono tu au kwa kutumia kifaa chochote kilicho karibu.
 
blackcornshman

blackcornshman

JF-Expert Member
Joined
Aug 25, 2016
Messages
2,423
Points
2,000
blackcornshman

blackcornshman

JF-Expert Member
Joined Aug 25, 2016
2,423 2,000
Lakini bado hajapatikana na hatia. Nishasikia kisa kimoja uko ulaya watu walifake mada na kumtunia ushahidi mtu asiye husika, kwa kutokosa umakiini mahakama ilimpiga kitanzi yule jamaa baada ya muda ilijilikana ailye uwawa siye bari alijitolea tu kuthibitisha mapungufu ya mifumo yetu.

Tusubiri tuone mwisho wake.
Mkuu kumbe mahakama za ulaya nazo zinapiga vitanzi.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
118,496
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
118,496 2,000
Kweli kabisa yaani hapo hukumu yake kunyongwa had kufa au maisha so Hana Cha kupoteza ashajua teyar hachoki hapo katika hyo kesi

Wakimpa upenyo atamniga mtu hapo na hata huyo hakimu anaesikiliza hyo kesi awe makin awakawiii kukurupuka hafla bin vu huyu hapa
Kesi yake haipaswi kucheleweshwa hukumu... Na akishahukumiwa fasta avishwe kitanzi kuepesha matatizo zaidi
 
Forum statistics

Threads 1,336,205
Members 512,562
Posts 32,530,421
Top