Dar: Aliyemuua mkewe na kuuchoma mwili kwa mkaa awatisha Wanahabari

Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
687
Points
1,000
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
687 1,000
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
=====

Hamis Said Luongo(38) ambaye ni mshtakiwa wa mauaji ya mke wake, Naomi Marijani katika eneo la Gezaulole Kigamboni ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania kuwa atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambacho mahakama hiyo haitakitarajia.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo Jumanne Agosti 13,2019 mbele ya Mahakama hiyo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa Luongo alinyoosha kidole na kuiomba Mahakama hiyo kuwa kichwa chake kimechanganyikiwa hivyo atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambapo Mahakama hiyo haitatarajia.

"Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu waandishi wa habari ambao wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama, sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama hii nitafanya kitu kibaya ambacho hamtakitegemea.”

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ndani nataka akili yangu itulie lakini hawa wapiga picha wananipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitawafanya kitu kibaya ambacho Mahakama haitatarajia," amedai

Baada ya kauli hiyo, Wakili Wankyo alimueleza mshtakiwa huyo kuwa kupigwa picha ni hali ya kawaida na washitakiwa wote wanaofikishwa mahakamani wanapigwa picha na yeye siyo mtu wa kwanza hivyo awape uhuru waandishi wa habari wafanye kazi yao kuwa huru.

"Lengo la waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwajuza wananchi hivyo awape uhuru wafanye kazi yao kuwa huru na kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani," amedai Simon.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ameshitakiwa chini ya Kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kosa hilo, mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
 
PTER

PTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Messages
5,901
Points
2,000
PTER

PTER

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2014
5,901 2,000
Hapana asidharauliwe akipata upenyo kidogo tu... Anaweza kuleta majanga makubwa.... Kumbuka hana cha kupoteza kwasasa kwahiyo si ajabu anapanga kuua tena
Na kweli akipata upenyo ataishangaza mahakama.
 
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined
Jun 23, 2012
Messages
10,974
Points
2,000
PATIGOO

PATIGOO

JF-Expert Member
Joined Jun 23, 2012
10,974 2,000
He is revealing his true inside....
Ndugu mshana
,Muuaji wa kikatili hivi mbona yuko salama hadi sasa...wauaji wa hivi mzimu wa marehem hua haumuachi salama...au ndo mwisho wake unakaribia
 
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2014
Messages
41,536
Points
2,000
mrangi

mrangi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2014
41,536 2,000
Huyu jamaa ni serial killer
Any way atawafanya nn waandishi aache mikwalaa, akumbuke yuko nyuma ya nondo tu na wakimleta mahakamani yuko Ndani ya bangili

Ova
 
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined
Sep 4, 2013
Messages
16,641
Points
2,000
FRANCIS DA DON

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Joined Sep 4, 2013
16,641 2,000
Kama hataki kupigwa picha muacheni
 
Himawari

Himawari

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2008
Messages
2,377
Points
2,000
Himawari

Himawari

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2008
2,377 2,000
Wakimwachia upenyo itakuwa upuuzi wao.

Huyo ni psychotic. Ameshaonyesha kasoro kichwani kwa kupiga mkwara huo mbele ya vyombo vya dola. Anatakiwa awekewe shackles za mikono na visigino.
Nashangaa anapelekwa mahakamani kama vile vibaka wa kuku ilihali jamaa anatuhuma za kumuua mkewe kinyama kisha kumchoma moto!,
 
GODZILLA

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined
Dec 26, 2014
Messages
2,689
Points
2,000
GODZILLA

GODZILLA

JF-Expert Member
Joined Dec 26, 2014
2,689 2,000
Wengi humu mtashangaa huyo jamaa akiachiwa huru! Acheni porojo.

Maana kila mtanganyika ana PhD ya mapenzi na mahaba! Wote mlishahitimisha kuwa jamaa ni muuaji aliyeua kwa wivu wa kimapenzi.

He will be acquitted! Mtahamaki vizuri.

Mnamkera na mapicha picha yenu. He deserves privacy!

Waandishi uchwara hawa! Mapicha picha ya nini!???
 
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2014
Messages
13,160
Points
2,000
tamuuuuu

tamuuuuu

JF-Expert Member
Joined Mar 10, 2014
13,160 2,000
Jamaa itakuwa amekula mafunzo flani si hivihivi
 
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined
Nov 18, 2012
Messages
2,783
Points
2,000
Idd Ninga

Idd Ninga

Verified Member
Joined Nov 18, 2012
2,783 2,000
Damu ya mtu huwa haipotei,taratibu inaanza kumnyonya hadi aishe kabisa.
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
118,437
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
118,437 2,000
Ndugu mshana
,Muuaji wa kikatili hivi mbona yuko salama hadi sasa...wauaji wa hivi mzimu wa marehem hua haumuachi salama...au ndo mwisho wake unakaribia
Tayari damu ya marehemu mkewe inamnukia unadhani anapata usingizi?
 
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Messages
118,437
Points
2,000
Mshana Jr

Mshana Jr

JF-Expert Member
Joined Aug 19, 2012
118,437 2,000
Huyu jamaa ni serial killer
Any way atawafanya nn waandishi aache mikwalaa, akumbuke yuko nyuma ya nondo tu na wakimleta mahakamani yuko Ndani ya bangili

Ova
mrangi huwa sidharau kitisho hasa cha mtu kama yeye.... Kumbuka bado yuko hai na bongo yake kwa sasa muda mwingi anawaza uovu
 
vipik2

vipik2

JF-Expert Member
Joined
Nov 24, 2011
Messages
1,638
Points
2,000
vipik2

vipik2

JF-Expert Member
Joined Nov 24, 2011
1,638 2,000
Wakimwachia upenyo itakuwa upuuzi wao.

Huyo ni psychotic. Ameshaonyesha kasoro kichwani kwa kupiga mkwara huo mbele ya vyombo vya dola. Anatakiwa awekewe shackles za mikono na visigino.
Ni kweli na nilishangaa sana mara ya kwanza aliletwa mahakamani bila pingu sijui ni ndugu yao? kama atawadhuru watu mahakamani hao Askari wawajibishwe kwa uzembe wao
 
DiasporaJay

DiasporaJay

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Messages
15,866
Points
2,000
DiasporaJay

DiasporaJay

JF-Expert Member
Joined Aug 27, 2016
15,866 2,000
Wanahabari nao wana kiherehere sana. Wakizidi washughulikiwe but sio kwa kuchomwa na magunia ya mkaa.
 
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2012
Messages
17,819
Points
2,000
stroke

stroke

JF-Expert Member
Joined Feb 17, 2012
17,819 2,000
Jamaa anaweza kuwa anazuga tu , ili imrahisishie kwenye kesi yake ya msingi
 
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Messages
2,965
Points
2,000
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2018
2,965 2,000
Labda hakimu angempatia nafasi ya kufanya
hicho kitu kitakachoishangaza mahakama
 

Forum statistics

Threads 1,335,859
Members 512,453
Posts 32,518,136
Top