Dar: Mtoza Ushuru wa Stendi ahukumiwa kwa kuomba Rushwa ya Tsh. 150,000

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Februari 15, 2024 kesi namba cc 3998/2024 imeamuliwa katika Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni ambapo imemtia hatiani Bw. MOSES JOHN ZIMBA (Mkusanya Ushuru Stendi ya Mabasi Bunju), kwa kosa la Kuomba na Kupokea Rushwa kinyume na kifungu cha 15(1)(a) cha Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa [CAP 329 RE 2019].

Mahakama imefikia uamuzi huo baada ya mshtakiwa kukiri kosa lake.

Ifahamike kuwa mshtakiwa alitenda kosa hilo la kuomba rushwa ya kiasi cha shilingi 150,000/ kutoka kwa kondakta wa daladala ili ampunguzie kulipa fine ya shilingi 300,000 kwa kosa la kutolipia ushuru katika stendi ya mabasi Bunju.

Baada ya Mahakama kumtia hatiani imemhukumu mshtakiwa kulipa faini ya shilingi laki tano (500,000) au kifungo cha miaka miwili (2) gerezani.

Kesi hiyo imesikilizwa mbele ya Mheshimiwa Janeth Kaluyenda na mshtakiwa amelipa faini.
 
Makonda alishawwambia maskini hawana haki ona Lowassa anaenda kuzikwa kwa Gharama kubwa za walipakodi pamoja na ufisadi wote aliotuumiwa na badala ya kushtakiwa yeye aliaamua tu kujiuuzlulu na kuendelea kula pensheni ambayo hakuichagua hata senti tano.
 
Dadeq, haitakiwi kuomba rushwa ndogo ndogo, sio kwa speed hii ya kuwapa adhabh hahah
 
Back
Top Bottom