Mahakama yakubali mshtakiwa mauaji ya mkewe apimwe Afya ya Akili

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,376
8,120
1694150437766.png

Upande wa utetezi katika kesi inayomkabili Hamis Luoga anayekabiliwa na shtaka la mauaji ya mkewe, Naomi Marijani umeiomba Mahakama mshtakiwa huyo akapimwe afya ya akili.

Wakili wa utetezi, Mohamed Majaliwa ameiomba Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, mshtakiwa apelekwe Hospitali ya Isanga mkoani Dodoma akapimwe afya ya akili kabla ya kuendelea na shauri hilo. Mahakama imekubali ombi hilo.

Luoga anadaiwa kumuua Naomi, kuuchoma moto mwili wake kwa kutumia magunia mawili ya mkaa na majivu yake alikwenda kuyafukia shambani kwake.

Wakili wa utetezi Majaliwa anayeshirikiana na Michael Kibindo, aliwasilisha ombi hilo jana mbele ya Jaji Mussa Pomo, shauri hilo lilipoitwa kwa ajili ya mshtakiwa kusomewa hoja za awali. Majaliwa alisema wanaomba mshtakiwa akafanyiwe uchunguzi kwa kuwa wana wasiwasi, kwani hata wanapozungumza naye hayupo sawa kiakili.

Alidai hawawezi kusikiliza mashahidi hadi hospitali itakapotoa majibu ya uchunguzi wa afya ya akili ya mshtakiwa na Jaji Pomo alikubali ombi hilo. Alisema shauri hilo litapangiwa tarehe baada ya majibu ya hospitali.

Awali, Wakili wa Serikali Dorothy Masawe alidai wanatarajia kusikiliza mashahidi 28 na watakuwa na vielelezo 15 katika kesi hiyo. Akimsomea mshtakiwa hoja za awali alidai kati ya vielelezo hivyo, saba ni vya nyaraka na vinane ni vitu halisi.

Alidai Mei 15, 2019 eneo la Gezaulole wilayani Kigamboni mshtakiwa alimuua kwa kukusudia Naomi.

Mshtakiwa anadaiwa Mei 19, 2019 aliripoti kituo cha polisi cha Mji Mwema kuwa mkewe Naomi na mwanaye wametoweka tangu Mei 17, 2019.

Inadaiwa alipohojiwa na polisi kituoni alikiri kumshambulia mkewe hadi kufa, baadaye alichukua mwili na kuupeleka kwenye kibanda na kuuchoma kwa mkaa.

Mshtakiwa anadaiwa katika mahojiano hayo, alieleza baada ya kuuchoma mwili alichukua mabaki ya majivu na kuyaweka kwenye mfuko. Kwa kutumia gari lake aina ya Subaru Forester aliyabeba na kuyapeleka shambani kwake eneo la Mlogolo wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

Wakili Massawe alidai katika mahojiano hayo mshtakiwa anadai alichimba shimo kwenye shamba lake na kuyafukia. Pia alipanda mgomba juu yake.

Baada ya maelezo hayo anadai vilichukuliwa vinasaba vya majivu kwenda kupimwa kwa Mkemia Mkuu wa Serikali, ndipo ilipobainika kuwa yalikuwa mabaki ya mwili wa Naomi.

MWANANCHI
 
Hii kesi jamaa atachomoka inaonekana anatembeza mpunga wa kutosha, kesi gani isiyoisha na kitu kipo wazi kabisa. Hapo majibu yanakuja ana matatizo ya akili mwisho wa siku anaachiwa huru au anahukumiwa miaka miwili au mitatu
 
Mimi nilivyoona Mke hatuelewanj na kila mtu analala chumba chake,halafu bado haridhiki anaendelea kunifanyia visa kila kukicha alarm ikalia kichwani kwamba kuna kitu kinakuja kutokea,nilitegea kaenda kazini na basi la kazini kwao(alikuwa Private Sector),nikawasha gari niliyomnunulia na yangu nikaenda kuzificha sehemu,nikarudi na Canter nikabeba vitu vyangu nilivyoona vya maana nikaondoka zangu na kwenda kupanga(kumbuka hapo tulikuwa tunaishi nyumba ya Serikali ninakofanya kazi),ofisini nikawaambia wachukue nyumba yao wasinikate kwenye Mshahara nimehamia kwangualiachia nyumba bila kupenda,huu ni mwaka wa 12 sasa naishi vizuri bila kelele
 
Miaka 12 hiyo ya kuishi bila Kelele umeoa tena ? Ama unaishi kibachelor
 
Hii kesi jamaa atachomoka inaonekana anatembeza mpunga wa kutosha, kesi gani isiyoisha na kitu kipo wazi kabisa. Hapo majibu yanakuja ana matatizo ya akili mwisho wa siku anaachiwa huru au anahukumiwa miaka miwili au mitatu
Hivi unafahamu mpunga wewe??sasa huyo jamaa ana mpunga gani wa kusema anatembeza kwa Majaji atoke??yule jamaa aliyesimamia MAUAJI ya Billionea Msuya yupo ndani mpaka leo akisubiri Hukumu ya Kunyongwa,licha ya kukata Rufaa Mahakama ya Rufaa lakini alishindwa.Na kumbuka ana pesa ya Madini hatari,pale Arusha ana vitega UCHUMI vya kutosha lakini havijasaidia yeye kutoka wakati hata eneo la tukio hakuwepo.
 
Hii kesi jamaa atachomoka inaonekana anatembeza mpunga wa kutosha, kesi gani isiyoisha na kitu kipo wazi kabisa. Hapo majibu yanakuja ana matatizo ya akili mwisho wa siku anaachiwa huru au anahukumiwa miaka miwili au mitatu
Kesi za MAUAJI si sawa na za Wizi wa Kuku,za MAUAJI huchukua miaka 5 na kuendelea mpaka kwisha,kwa hiyo usiseme Kesi gani isiyoisha,ndivyo zilivyo,si unaona ile ya yule Dada mdogo wake Bilionea Msuya aliyechinjwa Kibada!!!ni Kesi ya 2016 na ndio sasa inaendelea Mahakama Kuu Dar,piga hesabu hapo imepita miaka mingapi
 
Kesi imeisha hiyo,hapo dokta anapewa mlungura, anasema upo crazy unapelekwa sober house!! Miaka, mitatu wa bongo wameisha sahau,unarudi zako hm kula bata.
 
Mimi nilivyoona Mke hatuelewanj na kila mtu analala chumba chake,halafu bado haridhiki anaendelea kunifanyia visa kila kukicha alarm ikalia kichwani kwamba kuna kitu kinakuja kutokea,nilitegea kaenda kazini na basi la kazini kwao(alikuwa Private Sector),nikawasha gari niliyomnunulia na yangu nikaenda kuzificha sehemu,nikarudi na Canter nikabeba vitu vyangu nilivyoona vya maana nikaondoka zangu na kwenda kupanga(kumbuka hapo tulikuwa tunaishi nyumba ya Serikali ninakofanya kazi),ofisini nikawaambia wachukue nyumba yao wasinikate kwenye Mshahara nimehamia kwangualiachia nyumba bila kupenda,huu ni mwaka wa 12 sasa naishi vizuri bila kelele
Daah roho mbaya tu hiyo na Umasikini upo kwenye damu kwani ungemtengenezea mazingira mazuri ya yeye kuendelea kuishi ungepungukiwa nini unahadithia kuchukua gari aisee...
 
Mawakili wetu bwana,yaani mtu achukue gunia,achome mtu afukie majivu afu awe hana utimamu wa akili.
Ndio maana wale Mawakili wajanja wajanja wanashika ndege zetu kila wanapoamua anajifanya hana akili baada ya kukaa jela kwani hilo kosa alifanya wakati akili zipo au....
Mtu aside na akili anaweza kwenda kufukia majivu shambani ili yasionekane?
 
Back
Top Bottom