Dar: Aliyemuua mkewe na kuuchoma mwili kwa mkaa awatisha Wanahabari

Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
667
Points
1,000
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
667 1,000
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
=====

Hamis Said Luongo(38) ambaye ni mshtakiwa wa mauaji ya mke wake, Naomi Marijani katika eneo la Gezaulole Kigamboni ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania kuwa atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambacho mahakama hiyo haitakitarajia.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo Jumanne Agosti 13,2019 mbele ya Mahakama hiyo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa Luongo alinyoosha kidole na kuiomba Mahakama hiyo kuwa kichwa chake kimechanganyikiwa hivyo atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambapo Mahakama hiyo haitatarajia.

"Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu waandishi wa habari ambao wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama, sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama hii nitafanya kitu kibaya ambacho hamtakitegemea.”

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ndani nataka akili yangu itulie lakini hawa wapiga picha wananipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitawafanya kitu kibaya ambacho Mahakama haitatarajia," amedai

Baada ya kauli hiyo, Wakili Wankyo alimueleza mshtakiwa huyo kuwa kupigwa picha ni hali ya kawaida na washitakiwa wote wanaofikishwa mahakamani wanapigwa picha na yeye siyo mtu wa kwanza hivyo awape uhuru waandishi wa habari wafanye kazi yao kuwa huru.

"Lengo la waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwajuza wananchi hivyo awape uhuru wafanye kazi yao kuwa huru na kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani," amedai Simon.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ameshitakiwa chini ya Kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kosa hilo, mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
 
funzadume

funzadume

JF-Expert Member
Joined
Jan 28, 2010
Messages
9,398
Points
2,000
funzadume

funzadume

JF-Expert Member
Joined Jan 28, 2010
9,398 2,000
Huyo jamaa hasipuuzwe kwa alichosema
 
papason

papason

JF-Expert Member
Joined
Sep 14, 2010
Messages
2,973
Points
2,000
papason

papason

JF-Expert Member
Joined Sep 14, 2010
2,973 2,000
'naomi john' akaenda kuolewa na 'hamis said' kwa tamaa ya kuendesha ma-vogue na kuishi kwenye magorofa?? mwache yamkutee yaliyo mkuta kwa ujinga wake....
 
IDEGENDA

IDEGENDA

JF-Expert Member
Joined
Sep 15, 2013
Messages
1,201
Points
2,000
IDEGENDA

IDEGENDA

JF-Expert Member
Joined Sep 15, 2013
1,201 2,000
Kuna vitu unaweza kufanya ukajiona kama we mjanja kumbe ni mbugila mbugila tu,,!

Japo wanawake wana kero ila sasa hivi anajutia si bora kwenye ule ugomvi angekaa zake tu kimya ili maisha yaendelee
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
451
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
451 500
Mi naongelea huo mkwara alioupiga kuwa ataishangaza mahakama.
Usiogope mahakama nimuhimili.usijisahau ndomana walikataa kutoa kibali lisu akakamatwe ubeligiji,walijua serikali imechanganyikiwa haijielewi,dunia zima inajua anaumwa serikali haijui(kumbuka tunamihimili 3,(1)executive/dola(2)Parliament/bunge (bonge),(3)Judiciary/mahakama....,,,,,,sasa pamoja nakua nahiyo mihimili mitatu nimekupa hapo,nimuhimili mmoja tu unaojua lisu mgonjwa ...huko nikuchanganyikiwa ,mahakama hawawezi kumuazibu kwakauli hiyo kizimbani
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
451
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
451 500
We ni mdwanzi ...ndani ya mahakama lazima uwe kizimbani unavosikiliza kesi yako na pembeni kuna askari wa kukulinda...au unadhani ukiwa mahakamani unakuwa kama uko na mpenzi wako...sasa hapo unadhani atafanya nini...we ni maku eti!!! au unadhani akiwa hapo mahakamani atakuwa na gunia mbili za mkaa...
Matusi yann ,nisahihishe kwa fact kisheria,huo sio muhimili dola huo,ndomana ulivoambiwa naserikali kupitia wakili waserikali itoe kibali kumkamata ubeligiji serikali iligomewa,kwan mahakama ilijua serikali imechanganyikiwa..hatahuyo kachanganyikiwa kama serikali ambavyo imedata kuhusu lisu
 
kijana wa leo

kijana wa leo

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2011
Messages
2,691
Points
2,000
kijana wa leo

kijana wa leo

JF-Expert Member
Joined Nov 28, 2011
2,691 2,000
Sema mimi kunakitu sielewi kuhusu upelelezi kutokamilika, huyu jamaa kwenye mahojiano alikiri kumuua mkewe, akawaeleza police alivyomuua mkewe na hadi kwenda kumzika Shambani, police walifuatilia sehemu zote hadi wakaupata mwili kama walivyoelezwa na muuaji, kisha wakatutangazia ukweli wenyewe uliyokua. Sasa ni upelelezi gani huo unaoendelea?
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
451
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
451 500
Sema mimi kunakitu sielewi kuhusu upelelezi kutokamilika, huyu jamaa kwenye mahojiano alikiri kumuua mkewe, akawaeleza police alivyomuua mkewe na hadi kwenda kumzika Shambani, police walifuatilia sehemu zote hadi wakaupata mwili kama walivyoelezwa na muuaji, kisha wakatutangazia ukweli wenyewe uliyokua. Sasa ni upelelezi gani huo unaoendelea?
Kama jamaa anamkwanja na ameweka wakili msomi ,basi lazima serikali ijipange kwani kunatakiwa kue naushahidi wakutosha ,wamdomoni kwamtu maranyingi mahakama inaweza kuutumia fasta kama mwenyewe amekiri mubashara kizimbani ,ilakama amekubali kwahawa polisiccm .sahau kufungwa jamaa
 
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2017
Messages
1,769
Points
2,000
MakinikiA

MakinikiA

JF-Expert Member
Joined Jun 7, 2017
1,769 2,000
mmakonde wa ukweli huyo na awafanyie kitu mbaya si mnamsumbua yeye ameshakiri kuua na yeye apewe haki yake ya kifo tu anawashangaa mnavyoendelea kumnadi subirini akawabanike kama kitimoto
 
Papi Chulo

Papi Chulo

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Messages
2,835
Points
2,000
Papi Chulo

Papi Chulo

JF-Expert Member
Joined Jun 8, 2018
2,835 2,000
Kibongobongo utakuta anashinda hiyo kesi..

Kumbuka:
Hakuna lisilowezekana bongoland
 
Sakasaka Mao

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined
Sep 29, 2016
Messages
4,414
Points
2,000
Sakasaka Mao

Sakasaka Mao

JF-Expert Member
Joined Sep 29, 2016
4,414 2,000
Sasa ana uhakika gani kama atashinda kesi ya mauwaji ili aje apambane na wanahabari huku uraiani...nahisi atakuwa na mental-disorder
Yeye anadai hapohapo mahakamani anaweza 'kuwafanyizia' hao wanaomfotoa hadi mahakama isiteajabu!
 
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
26,090
Points
2,000
N

NAKWEDE

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
26,090 2,000
Pascal Mayalla kuweni makini
 

Forum statistics

Threads 1,334,263
Members 511,935
Posts 32,471,375
Top