Dar: Aliyemuua mkewe na kuuchoma mwili kwa mkaa awatisha Wanahabari

Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined
Jul 1, 2018
Messages
691
Points
1,000
Influenza

Influenza

JF-Expert Member
Joined Jul 1, 2018
691 1,000
Mfanyabiashara Hamis Said anayekabiliwa na kesi ya kumuua Mkewe Naomi Marijani kisha kumchoma moto ametoa vitisho ktk Mahakama ya Kisutu akidai atawafanyia kitu kibaya Wanahabari "Wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya Mahakama, sasa nitakuja kuishangaza Mahakama"
=====

Hamis Said Luongo(38) ambaye ni mshtakiwa wa mauaji ya mke wake, Naomi Marijani katika eneo la Gezaulole Kigamboni ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam nchini Tanzania kuwa atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambacho mahakama hiyo haitakitarajia.

Awali, Wakili wa Serikali Mwandamizi Wankyo Simon amedai leo Jumanne Agosti 13,2019 mbele ya Mahakama hiyo kuwa shauri lilikuja kwa ajili ya kutajwa na upelelezi haujakamilika.

Baada ya maelezo hayo, mshtakiwa Luongo alinyoosha kidole na kuiomba Mahakama hiyo kuwa kichwa chake kimechanganyikiwa hivyo atafanya kitu kibaya kwa waandishi wa habari ambapo Mahakama hiyo haitatarajia.

"Mheshimiwa nina kitu ambacho nataka nikueleze kuhusu waandishi wa habari ambao wamekuwa wakinipiga picha kuanzia chini hadi ndani ya mahakama, sasa nakueleza hivi nitakuja kuishangaza mahakama hii nitafanya kitu kibaya ambacho hamtakitegemea.”

"Kuna kesi ambayo inanikabili na sielewi hatima ya kesi yangu, hapa nilipo kichwa changu kimevurugika nina mawazo ya mtoto wangu na ninapofika hapa ndani nataka akili yangu itulie lakini hawa wapiga picha wananipiga picha sasa nawaeleza kuwa nitawafanya kitu kibaya ambacho Mahakama haitatarajia," amedai

Baada ya kauli hiyo, Wakili Wankyo alimueleza mshtakiwa huyo kuwa kupigwa picha ni hali ya kawaida na washitakiwa wote wanaofikishwa mahakamani wanapigwa picha na yeye siyo mtu wa kwanza hivyo awape uhuru waandishi wa habari wafanye kazi yao kuwa huru.

"Lengo la waandishi wa habari ni kutoa habari na kuwajuza wananchi hivyo awape uhuru wafanye kazi yao kuwa huru na kumbuka hii ni mahakama na hatujui kitu unachotaka kufanya ni kitu gani," amedai Simon.

Baada ya kueleza hayo, Hakimu Ally ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 27, 2019 kwa ajili ya kutajwa.

Mshtakiwa huyo ameshitakiwa chini ya Kifungu cha 196 cha Kanuni ya Adhabu, sura ya 16 kilichofanyiwa marejeo mwaka 2002.

Katika kosa hilo, mshitakiwa anadaiwa Mei 15, 2019 katika eneo la Gezaulole Kigamboni Dar es Salaam alimuua mtu anayeitwa Naomi Marajani.
 
data

data

JF-Expert Member
Joined
Apr 9, 2011
Messages
20,714
Points
2,000
data

data

JF-Expert Member
Joined Apr 9, 2011
20,714 2,000
Kauli hii isichukuliwe poa... Afungwe pingu mikononi na miguuni anapoenda mahakamani...

Atakuja kung'an'gana na pua ya mmoja wao na kuitafuna.

Be serious Mahakama.
 
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Messages
8,410
Points
2,000
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2018
8,410 2,000
Sasa ana uhakika gani kama atashinda kesi ya mauwaji ili aje apambane na wanahabari huku uraiani...nahisi atakuwa na mental-disorder
Soma vizuri amesema atafanya jambo la kuishangaza mahakama kwa Waandishi
 
Kweli kabisa
 
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2018
Messages
490
Points
500
K

kina kirefu

JF-Expert Member
Joined Dec 14, 2018
490 500
Sasa ana uhakika gani kama atashinda kesi ya mauwaji ili aje apambane na wanahabari huku uraiani...nahisi atakuwa na mental-disorder
Mbona unakurupuka nawewe,kasema atawafanya mbaya ndani yamahakama...sio vizuri kuchangia kitu hujakielewa
 
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2016
Messages
3,219
Points
2,000
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2016
3,219 2,000
Mbona unakurupuka nawewe,kasema atawafanya mbaya ndani yamahakama...sio vizuri kuchangia kitu hujakielewa
We ni mdwanzi ...ndani ya mahakama lazima uwe kizimbani unavosikiliza kesi yako na pembeni kuna askari wa kukulinda...au unadhani ukiwa mahakamani unakuwa kama uko na mpenzi wako...sasa hapo unadhani atafanya nini...we ni maku eti!!! au unadhani akiwa hapo mahakamani atakuwa na gunia mbili za mkaa...
 
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2016
Messages
3,219
Points
2,000
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2016
3,219 2,000
Soma vizuri amesema atafanya jambo la kuishangaza mahakama kwa Waandishi
Sasa we unadhani huyo muuaji akiwa hapo mahakamani wanamuangalia kama mahindi ya kuchoma...hiyo ni kupagawa siyo yeye hapo
 
upendodaima

upendodaima

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2013
Messages
3,562
Points
2,000
upendodaima

upendodaima

JF-Expert Member
Joined May 23, 2013
3,562 2,000
Uzuri wake ametoa onyo tayari,sasa huyo hakimu Simon anasema ni jambo la kawaidi tu kupigwa picha bila kuchukua tahadhari..

Atakuja afumue mtu kwa camera yake mwenyewe tuje tujazane hapa kusema R.I.P mwandishi wa habari.
 
JAKUGOTE

JAKUGOTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 19, 2013
Messages
212
Points
250
JAKUGOTE

JAKUGOTE

JF-Expert Member
Joined Nov 19, 2013
212 250
We ni mdwanzi ...ndani ya mahakama lazima uwe kizimbani unavosikiliza kesi yako na pembeni kuna askari wa kukulinda...au unadhani ukiwa mahakamani unakuwa kama uko na mpenzi wako...sasa hapo unadhani atafanya nini...we ni maku eti!!! au unadhani akiwa hapo mahakamani atakuwa na gunia mbili za mkaa...
Mkuu huna haja ya kutukana....kauli aliyoitoa haitakiwi ichukuliwe poa. Kwa mazingira yaliyopo mahakaman hata sekunde 2 tu zinatosha mtu kufanya jambo na kumuathiri mtu mwngne. Kumbuka huyo sasa hv ni kama mbogo aliyejeruhiwa hana cha kupoteza, yuko tayari kwa lolote. Unaweza ukakaa karibu tu akakurukia kichwa kimoja tu:) ukazima hapohapo. Yeye akaenda kuhukumiwa basi mchezo ukawa umeishia hapo
 
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined
Oct 1, 2016
Messages
3,219
Points
2,000
APEFACE

APEFACE

JF-Expert Member
Joined Oct 1, 2016
3,219 2,000
Mkuu huna haja ya kutukana....kauli aliyoitoa haitakiwi ichukuliwe poa. Kwa mazingira yaliyopo mahakaman hata sekunde 2 tu zinatosha mtu kufanya jambo na kumuathiri mtu mwngne. Kumbuka huyo sasa hv ni kama mbogo aliyejeruhiwa hana cha kupoteza, yuko tayari kwa lolote. Unaweza ukakaa karibu tu akakurukia kichwa kimoja tu:) ukazima hapohapo. Yeye akaenda kuhukumiwa basi mchezo ukawa umeishia hapo
Timing au sio...???
 
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined
Jan 12, 2018
Messages
8,410
Points
2,000
Ndumbula Ndema

Ndumbula Ndema

JF-Expert Member
Joined Jan 12, 2018
8,410 2,000
Sasa we unadhani huyo muuaji akiwa hapo mahakamani wanamuangalia kama mahindi ya kuchoma...hiyo ni kupagawa siyo yeye hapo
Wanao mwangalia nawao ni binadamu Lolote linaweza kutokea
 
Forum statistics

Threads 1,336,800
Members 512,722
Posts 32,551,291
Top