Dakta mwakyembe anatafuta pepo chafu la kumdhuru | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dakta mwakyembe anatafuta pepo chafu la kumdhuru

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by Divele Dikalame, Mar 16, 2011.

 1. D

  Divele Dikalame Member

  #1
  Mar 16, 2011
  Joined: May 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwakyembe anatafuta
  Pepo chafu la kumdhuru

  *Amesahau Mengi ni ‘Barrick’, Kilango hoi

  KUNA chembe ya kutaka nafasi ya 'u-wokovu' na hata 'ufia dini' ambayo inaelekea inagombewa na baadhi ya wanasiasa, hivyo wanachuana kuelezea hiki au kile wakidai wapo watu wanataka kiwafike, kwa mfano kupanga mauti yao, n.k. Wakati wa kampeni za uchaguzi ilisikika sana kuwa kuna 'ujumbe' wa kumhujumu Dk. Wilibrod Slaa, mgombea wa Chadema, kana kwamba katika rekodi yake ndefu ya padri katika Kanisa Katoliki, mradi wa maji Mbulu na usimamizi wa shughuli za Baraza la Maaskofu hapakuwa na 'data' za kutosha kwa kazi hiyo. Uhalisi wa suala ni kuwa Tanzania ni nchi ambayo bado inaendesha siasa kwa adabu, uvumilivu na kusameheana, ila wapo wanaotaka kuivuruga kila kukicha.

  Kundi la kwanza la wale wanaotaka kuiharibu nchi na mamluki wa nchi 'kutotawalika,' ambao sasa wana wimbo mpya, tuite 'kwaya' kuwa Tanzania iwe kama Misri, Tunisia au Libya. Bila kuorodhesha makosa ya viongozi hao waliopata matatizo inabidi kwanza tujiulize kama Rais Jakaya Kikwete yuko madarakani tangu mwaka 1969, mwaka 1981 au mwaka 1988 – halafu tugundue kuwa suala la kuwepo chembe ya 'Umisri' hapa ni fataki tupu. Hakuna mantiki yoyote inayozungumziwa, labda u-Jean Pierre Bemba wa kukataa matokeo ya uchaguzi, kuelekeza jeshi kuiteka Kinshasa. Hapo tunafika nyumbani, na mpango wa wale wanaokataa matokeo ni kutumia demokrasia kuandamana, wakipigwa waanze uasi.

  Hao wako katika upinzani wenyewe, lakini wapo baadhi ambao wamebakia chama tawala kwa midomo yao, ila hisia zao ziko mbali kabisa na nafasi hizo, mmojawapo akiwa Naibu Waziri, Dk. Harrison Mwakyembe. Amnenukuliwa kwa kirefu katika gazeti la kila siku la 'Mtanzania' kuhusu madai ya watu wanaotaka kumdhuru, ambayo amewakilisha Jeshi la Polisi na kuhojiwa kwa muda mrefu, na anatoa 'data' za kushtua. Ila ukizisoma hadi mwisho unagundua mambo kadhaa ambayo yanafafanua ni katika mazingira gani ambako madai hayo yametokea, na kwa nini yanaingizwa katika mfumo wa siasa, hivi sasa – yaani kuongezea matatizo ya ziada kisaikolojia wakati tuliyo nayo karibu tunashindwa kuyabeba.

  Tukubaliane na Dk. Mwakyembe jambo moja, kuwa inawezekana kabisa anao maadui, na tuongeze kuwa kwa mwanasiasa, hilo siyo jambo geni – ila anapotaka kuingia hadharani kuelezea nia za maadui zake, hapo kunahitaji uangalifu, kwani mara nyingi zaidi ni 'wasiwasi tu' unaotawala katika hisia. Ni chembe hii inayojitokeza katika mlolongo wa maelezo ambayo Naibu Waziri huyo anasemekana aliyatoa polisi, kwani jumuisho la 'maadui' wanaotajwa hapo kushirikiana wote kwa pamoja kwa kazi moja tu ya kumdhuru mbunge (na Naibu Waziri) huyo hauingii akilini. Yaani alikuwa anapiga kushoto, kati, kulia mradi tu kila anapoangalia wapo maadui – polisi, usalama wa taifa, mganga wa kienyeji, Al Shabaab...!

  Ingekuwa Dk. Mwakyembe anajifunza kuandika hadithi katika darasa la fasihi, haiyumkini mwalimu wake angemwambia kuwa 'nakala' ya hadithi yake ya kwanza (kama si ya pili au ya tatu) aliyotunga imejaa mno wahusika, ni 'overloaded,' aende akaiandike upya. Kimsingi kama polisi wana mpango wa kumdhuru mtu (si kuwa tunadhani ni hivyo) wasingehitaji usalama wa taifa, na kama yupo mtu binafsi anataka kumdhuru mbunge huyo, asingehitaji polisi. Iweje mtu ajaribu kushirikisha vyombo vya nchi katika mpango wa kihalifu, dhidi ya mtu ambaye mkuu wa nchi ana imani naye kwa kiwango hicho?

  Ni wazi kuwa hapa lipo suala la mantiki, la upana wa mpango wowote ule wa kumdhuru mbunge huyo – kwani si mara ya kwanza ameingia katika hatari ya kudhurika. Kuna wakati gari lake lilipinduka au kuingia katika hatari ya kubamizwa na lori zito, halafu akaambiwa 'akae kimya' kwani alikuwa amelala wakati tukio lilipojiri, naye akapinga kwa nguvu maelezo hayo. Kwa hapo wengi wetu tulimuunga mkono kwani haiwezekani mtu ahatarishiwe maisha yake halafu akae kimya katika kufafanua nini hasa kilichotokea; lakini hapo angalau watu walishuku adui mmoja, siyo mlolongo wa maadui na taasisi za nchi kama anavyodai hivi sasa. Ni hali hiyo ya kukusanya watu wengi kwa mpango huo inayotia shaka.

  Eneo jingine la udhaifu wa kile anachozungumza Dk. Mwakyembe katika maelezo yake ni kuwa kuna aina ya 'mgando' wa mawazo kuhusu nani adui yake katika siasa, kuwa bado hajaamka katika bumbuazi ya 'vita dhidi ya ufisadi' ya Agosti 2007 hadi Desemba 2009. Ilianzia na suala la Buzwagi ambako Zitto Kabwe aliadabishwa bungeni, halafu likafikia habari za mitandao kuhusu EPA na mengineyo, ndipo ikaanza 'Operesheni Sangara,' ambapo upinzani ulianza kuwaahidi samaki wakali ziwani kuwa miili mingi italetwa huko. Mungu apishe mbali lakini juhudi za kuwapa sangara miili mingi – hasa, si ajabu, ya wanaharakati – zinaendelea, kwani wanataka wajikusanye kiasi cha nchi 'kutotawalika' hivi punde!

  Kilichotokea mwisho wa mwaka 2009 ni kuwa baada ya kifo cha Mzee Rashidi Kawawa, ikawa bayana hapakuwa na mtu mwingine ambaye angeweza kushabikia 'vita dhidi ya ufisadi' kiasi cha kuhoji katika Kamati Kuu ya CCM kama rais aliyeko madarakani bado alikuwa anafaa kuwa mgombea wa CCM. Ni Mzee Kawawa ambaye kutokana na historia yake ya siasa ya Ujamaa walidhani atakuwa ngome yao, ili 'amfunge paka kengele,' lakini ufalme wa mbinguni ukawaelekeza wapigane vita vyao wenyewe na siyo kungoja 'Simba wa Vita' awatengenezee njia wapite. Alipoitwa kama kila mja atakavyoitwa, kundi lote hilo likaanza kusambaratika kwani wasingeweza kukusanyika Chadema au kwingine, waendeleze 'vita.'

  Uadui ambao Dk. Mwakyembe anazungumzia na kung'ang'ania kuwa wapo watu wanaotaka kumdhuru una sehemu mbili, ila yeye anaainisha moja tu, ambayo sasa imeshafifia. Sehemu ya kwanza ni ile ya siasa za kitaifa au makundi ya CCM ambako yeye na 'makamanda' wenzake wa 'vita dhidi ya ufisadi' waliunda kundi moja la kudaka hoja ya Chadema iwe ya CCM, kwani waliiona haipingiki miongoni mwa wapiga kura. Uadui unaotokana na makundi hayo ulianza kufifia taratibu mwanzo wa mwaka jana kwani harakati zao ziligonga mwamba, na kufikia Machi 2010 hapakuwa tena na mikutano ile ya 'vita dhidi ya ufisadi' bali maandalizi ya kugombea kuteuliwa jimboni. Hapo ndipo ncha ya pili inapoingia.

  Dk. Mwakyembe amekuwa na washindani kadhaa wa wazi kwa nafasi yake ya ubunge wa Kyela, mmoja akiwa na nafasi ya ukuu wa mkoa kwa muda mrefu, aliyesikitishwa na Dk. Mwakyembe 'kupandikizwa' kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam halafu Baraza la Kutunga Sheria la Afrika Mashariki, wakati yeye ni kada mwaminifu mkoani humo miaka yote. Tumliwaze kuwa hiyo hasa ndiyo demokrasia inavyofanya kazi, na si ajabu dukuduku hilo bado lipo – wakati mwingine alikuwa nasaba wa Dk.Mwakyembe naye akachukua fomu kuteuliwa watu wakampuuza, kuanza kumtupia madongo mjomba wake kwa kutaka tu madaraka. Kanuni za ustaarabu wa kisiasa zilifuatwa, lau kwa ngazi hiyo.

  Mahali ambapo Dk. Mwakyembe alielekea kukwama ni katika Kamati ya Siasa wilayani Kyela kwani wao walipokea taarifa (za huo usalama wa taifa ambao sasa anautuhumu mambo mazito) kuwa ni mchonganishi na hakisaidii chama katika kujenga imani kwa wananchi, na zaidi anasaidia upinzani. Licha ya kuwa taarifa ya usalama wa taifa kuhusu Dk. Mwakyembe haijawahi kuchapishwa, mwandishi wa habari anaweza akaandika ya kwake na ikafaa tu, kwani masuala yote hayo siyo siri. Ila ni suala tofauti kabisa kwake kuchupa kutoka hapo na kuanza kudai kuwa baadaye umesukwa mpango wa kuua!

  Ilipofikiwa tamati kuwa jina la Dk. Mwakyembe likatwe (hivyo akitaka ajiunge na wanaharakati wenzake Chadema agombee) na zikamfikia mwenyekiti wa chama, yeye akaweka 'veto' akihisi kuwa CCM ingewapatia wapinzani 'kada' mwingine mithili ya Dk. Slaa ambaye CCM ilizuia kuwa mgombea wake ndipo akahamia upinzani. Na siyo suala tu la kuhofia, kwani mitihani ya aina hiyo hutokea mara kwa mara katika mfumo wa siasa, ila kuangalia kina cha suala lenyewe, na pia kuwepo chembe ya msamaha, yaani kutokuendeleza sera za visasi, n.k. Hivyo Dk. Mwakyembe akarudishwa katika orodha hiyo na akapita kuwa mgombea, akasaidiwa kampeni na kushinda – sasa anatuhumu mpango wa kuua!

  Hata ingekuwa Dk. Mwakyembe amebaki tu mbunge na hakuingia serikalini, kusingekuwa na sababu yoyote ya kutuhumu vyombo vya dola – ambayo ni kumnyooshea kidole mkuu wa nchi au wasaidizi wake wakuu – kwa mpango kama huo, kwani suala kwao lilishamalizika. Isitoshe, kuna mlolongo wa watu ambao madai ya Dk. Mwakyembe yanasema nao wanaamdamwa wauawe – kwanza eti wawe bumbuazi kwa kulogwa na mganga fulani, ndiyo mauti iwafikie, ambayo ni kichekesho. Hivi labda Dk. Mwakyembe ni mgeni mno katika masuala ya ushirikina, pamoja na miingiliano yake na utawala wa maisha ya watu kutoka mbinguni, kujua kuwa wateule wa Mungu hawachezewi kijinga na watu baki tu?

  Tatizo ambalo linajitokeza katika kesi ya Dk. Mwakyembe – na siyo wengine anaowataja kama kina Anna Kilango au Reginald Mengi – ni kuwa kwa kusuka mipango yenye utata kwa kila mwenye kufuatia hali ya siasa, anatengeneza pepo la kumdhuru yeye mwenyewe. Anapodai kuwa hajapata ulinzi na baraka, msamaha kwa aliowatesa kwa madai ya kila aina wao wakayaweka kando wakasisitiza udugu, anachokonoa mwenyewe nguvu za giza zielekee kwake, kwani anakanusha kazi waliyofanya malaika kumlinda yeye, na malaika ni roho wa Mungu. Ni kile Waingereza wanaita 'self-fulfilling prophesies,' kuwa tabiri zinafanyika halafu zinajitimiza zenyewe, kwa sababu ya kuleta shauku – yaani kuwaminisha watu, kwa ulevi tu, ulevi tu, kuwa kuna mpango kabambe wa kumwondolea maisha yake!

  Kwa taarifa ya Dk. Mwakyembe, kwani inaelekea hata hasomi magazeti, anaishi katika hofu ile ile ya gari lake kupinduka wakati ule, na hajapona hata chembe – na sababu ya kutopona ni kutokusamehe, kwani anayebakiza kidonda moyoni hujiumiza mwenyewe; hiyo inafahamika kwa madaktari na pia wahubiri wa kila aina. Angekuwa anasoma magazeti, Dk. Mwakyembe angekuwa amesikia kuwa mwaka jana mwezi kama huu Reginald Mengi alikuwa mgeni wa heshima Barrick Gold akiwa tayari amenunua hisa baada ya kampuni hiyo kutangaza hisa zake London, zinunuliwe na wafanyabiashara wa hapa nchini. Alimwaga maji barafu kwenye uti wa mgongo wa 'vita ya Buzwagi' aliposema akiwa huko Barrick kwa ziara rasmi kuwa sekta ya madini ina sifa mbaya nchini kwa sababu haujakuwepo mpango kabambe wa kutoa elimu kuhusu sekta hiyo, na pia wanasiasa wachache wanaiandama kutaka rushwa!

  Sasa kama Dk. Mwakyembe anakuja leo anatuambia kuwa bado 'mafisadi' wana mpango wa kumdhuru yeye na Reginald Mengi, wakati yeye ni mjumbe wa Baraza la Mawaziri na Mengi ni mwakilishi maalum wa Barrick Gold, tumweleweje, kuwa amelewa?
  Halafu anamtaja Anna Kilango, ambaye kiu yake ya 'vita dhidi ya ufisadi' iliishia mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM ambako kada maalum Sofia Simba 'alimwaga mboga' kuhusu uhusiano wa familia yake na mfanyabiashara Jeetu Patel, enzi hizo 'vita dhidi ya ufisadi' haijaanza. Dk. Mwakyembe pia alishutumiwa kuwa hakueleza kuwa alikuwa na maslahi sekta ya nishati, akishindana na akina Rostam Aziz kwa mpango fulani kule Singida. Kwa jumla, hakuna aliye msafi hata mmoja wala wa kunyooshea kidole wengine, hivyo mpangilio wa katiba na demokrasia ndiyo unaohitaji kutumika, si madai ya 'mimi bora, fulani fisadi' wakati amekunja tu makucha, kama wale wanaoendesha kamari halafu wanataka wafike Ikulu kwa nguvu wawaokoe watu!

   
 2. REBEL

  REBEL Senior Member

  #2
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 15, 2010
  Messages: 164
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  kulikuwa hamna aja ya kumtaja dr.slaa na kumfananisha na bemba.hadithi yako inaboa inafanana kama imetungwa na kamati ya propaganda ya chama cha kijani na kuna(kucopy na kupaste kwingi)...to sum up my observation your story is boring and lack substance.
   
 3. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #3
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  nakushangaa unaona ajabu ipi mtu kusukiwa mpango na serikali kuuwawa?? hii si jambo la kwanza tokea duniani, wala tanzania na nchi majirani zake. Ukiona kina kitu cha kutia shaka katika maisha yako na nduguyo, paza sauti ili watu wawe macho na jamii ikusaidie. hiki ndo alichofanya dr. mwakyembe kuanika data alizosikia na uthibitisho wa data husika. dr mwakyembe si mjinga kiasi hicho unachotaka tukuamini kwa maelezo yako. Serikali ni "SIRI-KALI" katika nchi yeyote! Kuua mtu kwa msalilahi fulani ni kitu cha kawaida- na kwa msingi huo mwakyembe pia aweza kupangiwa kuuwawa kwa masilahi ya kundi fulani-si ajabu. Ndo maana mengi aliwa gundua hilo huko nyuma akapaza sauti yake hadhara mpango ukafa (aboted); mengi aliwahi toboa mpango wa polisi kumuhusisha mwanae madawa ya kulevya air port (mpango nao ukafa). Aliwataja vile vile watu hadharani polisi- na hakuna aliye weza kumshitaki na watu walihamishwa na kuondolewa katika nyazifa zao. majumuisho, usishangae wala kutaka watu tuamini kuwa dr mwakyembe ni mzushi-hii haingii akilini kabisa! Kuhusisha kwako dr. slaa katika mada yako inaoesha jinsi gani unataka yumbisha akili za watu huku---na huku... onesha msimamo wako vema
   
 4. M

  Marytina JF-Expert Member

  #4
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 7,034
  Likes Received: 48
  Trophy Points: 145
  hadithi njoo utamu kolea
   
 5. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #5
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Safi saaana
   
 6. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #6
  Mar 16, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Divele Dikalame

  Umeweka mambo wazi na kwa umahiri na uandishi unaomfanya mtu asichoke kukusoma. Hivyo ndivyo ilivyo.
   
 7. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 16, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  anythang in support by you is a crap.
   
 8. m

  matawi JF-Expert Member

  #8
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 29, 2010
  Messages: 2,055
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Acha kudumaa akili. Great thinker hawahitaji hadisi ndefu hivi andika kitu kifupi kinachoeleweka
   
 9. m

  masaiti Senior Member

  #9
  Mar 16, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 197
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hadithi njoo, uongo njoo. Anajitahidi kubwabwaja... pole

  to my side its a crap material.
   
 10. Mpasuajipu

  Mpasuajipu JF-Expert Member

  #10
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 22, 2010
  Messages: 838
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hivi wewe umesoma au umejifunza kuandika tu? unafikiri nani ana muda wa kusoma upupu wote huu ulioandika? Jifunze kusummarize habari siyo kupachika kila kitu humu.
   
 11. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #11
  Mar 16, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  Hiyo makala iliandikwa na gazeti la kiislam la annur la ijumaa iliypita,..sikosagi copy si kwa sababu ya habari zao ni za maana ila kujua ni crap gani mpya wameandika,.yani wao week in week out gazeti linawashambulia wakristo na chadema,..ni vizuri kujua hata mjinga anawaza nini asije akakucatch by surprise...
   
 12. Kichwa Ngumu

  Kichwa Ngumu JF-Expert Member

  #12
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 1,726
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  gazeti zima la uhuru umelipost soma mwenyewe
   
 13. M

  MAKAH JF-Expert Member

  #13
  Mar 16, 2011
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 1,598
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kihere here cha nini Ndugu Dikalame!! Mambo yapo kwenye vyombo vya usalama wa nchi - si tuwaachie wafanye kazi yao. Tutameza taarifa yao iwe vipi. Ndugu Dikamile au ndo MAKOVU ya kushindwa uchaguzi wa 2010????!!!!! Poleni sana.
   
 14. Mphamvu

  Mphamvu JF-Expert Member

  #14
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 28, 2011
  Messages: 10,708
  Likes Received: 937
  Trophy Points: 280
  Rai, An-Nuur, Mtanzania.... Maggid Mjenga....
  Nafikiria yangu tu kichwani, wallah hayana uhusiano na thread!
   
 15. M

  Mwikimbi JF-Expert Member

  #15
  Mar 16, 2011
  Joined: Mar 8, 2008
  Messages: 1,745
  Likes Received: 109
  Trophy Points: 160
  Mamluki mwingine wa rostam azizi, hivi anawalipa pesa tu au kuna kingine mnapewa? Manake sophia simba yeye hakuficha, alisifia kuwa mafisadi ni wanaume wa shoka. Sasa nyie wanaume wenzetu mafisadi ni wanaume wa shoka kwenu? Manake kwa stori hii ni lazima kuna utamu mwingine mnapewa na si pesa tu!!!!!!!!!!!!!!!!!1
   
 16. Gobegobe

  Gobegobe JF-Expert Member

  #16
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 245
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  [Qyeji, Al Shabaab...![/FONT][/B]

  Ingekuwa Dk. Mwakyembe anajifunza kuandika hadithi katika darasa la fasihi, haiyumkini mwalimu wake angemwambia kuwa 'nakala' ya hadithi yake ya kwanza (kama si ya pili au ya tatu) aliyotunga imejaa mno wahusika, ni 'overloaded,' aende akaiandike upya. Kimsingi kama polisi wana mpango wa kumdhuru mtu (si kuwa tunadhani ni hivyo) wasingehitaji usalama wa taifa, na kama yupo mtu binafsi anataka kumdhuru mbunge huyo, asingehitaji polisi. Iweje mtu ajaribu kushirikisha vyombo vya nchi katika mpango wa kihalifu, dhidi ya mtu ambaye mkuu wa nchi ana imani naye kwa kiwango hicho?[]
  Tofautisha hadithi na taarifa. Kilichotolewa na Mwakyembe ni taarifa ni siyo hadithi; au ndo sababu unafanya mzaha? Hapo kwenye bluu kama hutajali tafakari tena.
   
 17. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #17
  Mar 16, 2011
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  No thinking in this is just a crap. Ngoja mumguse muone cha moto.:angry:
   
 18. Mlangaja

  Mlangaja JF-Expert Member

  #18
  Mar 16, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 541
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Who on earth are you telling all this crap!
   
 19. N

  Ninaweza JF-Expert Member

  #19
  Mar 16, 2011
  Joined: Dec 14, 2010
  Messages: 7,187
  Likes Received: 1,189
  Trophy Points: 280
  Wewe mtoa mada ni mnafiki mkubwaaaaaa!
   
Loading...