Huu ni ukweli uliowazi. Al bashir wa nchi yetu ni ccm tu. Hakuna mwingine. Siku ccm ikianguka, huenda nchi yetu ikapiga hatua kubwa sana kimaendeleo. Hiki chama kimefanya blanda nyingi sana tokea kianzishwe kuliko mafanikio yake.
Kimewekewa mazingira ya chenyewe kuonekana ni chama bora sana kuliko hata Tanzania na watanzania wenye nchi yao.
Kipi ni kizuri mkuu AcT /Cdm
Ni kweli, na Mali za umma kuzifanya za ccm, Mfano zanzibar, pale kisonge, sasa hivi ccm wanajenga office kubwa, eneo la wazi la serikali walianza na kibanda sasa ni office ya ccm.chama cha mapinduzi kinamiliki mali kuzidi Serekali
Vip mishahara ya watumishi imeongezwa?labda liwe fundisho....kwako...huku kwetu hakuna watu wenye tabia za mtu unae mzungumzia
Kila nyota na wakati wake ndg,naunga mkono hoja
Ndugu umesahau msemo wa wahenga "mdharau mwiba.............."Wapinzani mwenyewe akina mbowe?
We kiumbe una matatizo kwa kichwa yako.Wewe boga nini? Unafikiri kila mtu ni shabiki wa siasa kama wewe? Chadema ni chama cha siasa Bali ni saccos ya kukopeshana magari.
We jamaa vp sijakuelewa au we ni miongoni mwa wanaosema "mimi sikuipigia kura ccm ila nilimpigia Magufuli au mimi sikumchagua Magufuli ila nilichagua ccm"Nyie ndio vipofu mkuu! Mnawaza kumtoa Magufuli badala ya kuwaza kuitoa ccm
[emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120][emoji120]Kweli dunia hadaa ulimwengu shujaa.
Nimemuona aliyekuwa akiabudiwa kama Mungu hana tena la kufanya zaidi tu ya kuwa mpole kama hua.
Wapambe wake wote hawapo tena. Wapiga vigelele na mapambio wote wametimua mbio. Al-bashir yuko peke yake hana tena Yale madaraka . Leo anaweza kuwa mfungwa kama wafungwa wengine.
Tunaposherekea sikukuu hii ya pasaka naomba tukio hili la Al-bashir liwe funzo kwetu. Tuishi maisha ya kutenda haki. Madaraka hutoweka kama kivuli ndipo nyakati za aibu na mateso hutamalaki.
Mwache kwanza aonje machungu ya dunia.Hivi huyu Albushiri bado yupo hai? Si WAMDIDIMIZE JAMBIA la anuzi kama ambavyo lile jambaz lingine tutakavyo lisokomeza Msumari wa nchi sita baada ya kumuopoa kwenye chemba la maji taka.
Ninachoipendea AFRICA yangu ni kimoja tu.
Hatutamaliza hata miaka miwili utashangaa maandamano tena, aliyepo anaboronga, wakati huo bashir yuko sehem salama anacheka kwa dharau.
Ajenda yetu ni kujenga nyumba za Maaskari, msitutoe kwenye lengo.
Huwa viongozi wengi hasa Africa hawajifunzi. Omari Ali Bashiri kwa sasa yuko pekee yake, ni kama hakuwahi kuwa na wapambe ingawa ukweli ni kwamba alikuwa na Wapambe wengi mno. Je wako wapi kwa sasa? mbona yuko pekee?
Mugabe Pia alikuwa mmoja ya Viongozi walio kuwa na wapambe hasa kutoka Chama chake cha ZANU-PF ila Dakika za mwisho alijikuta yuko pekee bila wale wapambe wake.
Kuna mifano mingi sana lakini JE HAWA WAPAMBE HUWA WANA POTELEA WAPI?
WAPAMBE WAPAKA MAFUTA VIONGOZI WAO HUWA WANAPOTELEA WAPU PINDI MISUKO SUKO INAPO ANZA KWA KIONGOZI WAO?
Umenikumbusha riwaya pendwa ya KULI 'lakini yana mwisho'