Dah! wanawake mtatuua kwa mateso sana

Dah! wanawake mtatuua kwa mateso sana

Habari wakuu

Japo sio swala jipya ila hata hii ni yenyewe[emoji22]

SITOMWAMINI MWANAMKE TENA

Nimeamua kulielezea hili kuhusu wewe mwanamke tuliyedumu ktk mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja. Sio siri kwa sasa umenipa wakati mgumu sana ktk mapenzi na sikutegemea kama ungenifanyia jambo gumu hivi.

Nakumbuka tulipoanza mahusiano yetu na uliponithibitishia huna mtu kabsa kimapenzi nikajikuta nakupenda tena moyo wangu ulishafika tamati kwako ulionyesha mapenzi ya dhati kwangu sikujua kama mwenzangu ulikua unatafuta njia ya kutoka.

Nakumbuka Ulikubali kwenda kunitambulisha kwenu na nilipokelewa vzr na ndugu zako nilifurahi sana kwa kua nilijua sasa nakaribia kupata mke. Lkn nilishangaa kila ninapokwambia nataka kuleta barua ulikataa na kuniambia bado itanijulisha.

Kwakua tulishafikia muda kdg ktk mapenzi yetu lkn kilichonishangaza kingine hukutaka kabsaa tukutane bila kutumia condom. Hii ilinipa maswali kdg ila sio mbaya nilijipa moyo mpaka tutakapofunga ndoa. Kwakua nashukuru mungu hela ya mboga na kuvaa sikosi Maana nimeajiriwa kwenye kampuni moja binafsi.

Siku hiyo ulinambia nikununulie vitu vya ndani upelekeke kwenu Maana wazazi wako wanapata shida vitu ni vya zamani halafu vimechoka.nikakununulia kitanda godoro sofa TV nikamalizia na fridge tukapeleka kwenu.

Baada ya miezi miwili kupita ukaniomba nikupe milioni moja ili ufanye biashara ikabidi nichukue mkopo wa milioni mbili kazini. Nikakupa laki nane ili uanze na hiyo biashara cha kushangaza kupita wiki tu ukawa hupatikani kwenye simu nikija kwenu naambiwa umesafiri tena nashangaa bila kuniaga!!

Kuna siku nilikupigia tena simu akapokea mwanaume akanitukana sana yaani ni mtu ambaye una mahusiano nae mda mrefu kabla yangu daaah we mwanamke una roho ngumu sana. Kwanini ulinificha na kuniaminisha mimi ndo wako ili tuje kuoana!!

Ila namshukuru sana mdogo wako siku nilipoenda kwenu tena ndipo akaniita pembeni na kunieleza kila kitu. Kumbe kwangu ulifanya njia ya mafanikio tu lkn uliyempenda ulikua nae. Yaan vitu nilivyonunua mimi umeenda kupanga chumba unaishia na mwanaume uliyempenda. Pia pesa niliyokupa uliyoniomba kwa nia ya biashara umempa huyo mwanaume kaongezea kanunua bodaboda yote nimeambiwa.

Nakupigia simu unamijibu nyodo na kejeri. Ila sawa mi huu mkopo nitaulipa ila namuachia mungu kwa uliyonifanyia. Umenifanya niyachukie mapenzi na nisimuamini mwanamke yeyote sasaivi. Chozi langu namuachia mungu yeye ndo atahukumu. Najua huu ujumbe lazima ukufikie lkn nikwambie tu mi nakutakia kila la kheri

cc: joanah
usilie mkuu alafu matatizo yako usimwachie Mungu yamalize mwenyewe, kubaliana na hali then songa mbele. usiropoke mengi ili moyo ukitulia usijutie uliyosema pia.
 
my Formula: Ukitaka kujua mpenzi uliyenae ana kupenda au hakupendi..Try to Push her away from you" subiria kakosea siku moja usimsingizie KOSA hakikisha kweli kakosea...Mmaindi kinoma kinoma JITIE huelewi mbele wala nyuma yani unajua kabisa haka kakosa ni kakuongea yaishe ila hakikisha unakua MBOGO bin FARU then tell her we ARE DONE.

Asee akikubali mmalizane wala usipomuona anarudi kuomba samahani kila siku zinavyoenda we kaa ujue Huyo HAKUA WAKO muache aende hata kama ulikua una mjaribu.

Kama anakupenda SHE will try/do all possible alternatives kuhakikisha mna solve yanaisha..as how we did to them na mwanamke aliekupenda ki ukweli hawezi kukubali umuache simple just like that kwa kosa analoamini kweli amelifanya,lazima ashuke atafute hata watu wamuombee msamaha.

Ukionamwanamke anafanya hivyo MSAMEHE na ujue ni wako huyo,asipofanya akiwa ni type ile (siwezi lazimisha mapenzi) Muache aende.

Mapenzi/mahusiano yanataka MAJARIBU hakikisha una mjaribu Mpenzi wako..MUNGU mwenyewe anatujaribu sembuse sisi binadamu ndo tusijaribiane? mpaka umekidhi vigezo nikakuita MKE aseeee ntakua nimekupitisha kwenye majaribu MOTO MOTO.

ONYO :

usimjaribu mpenzi wako akashinda jaribu ulilompa ukajisahau kumsahaulisha na kumpa zawadi...mimi nikishatoaga TEST zangu akishinda huwa ni mwendo wa surprise...usikae ukajiachia ktk mahusiano as if huyo ulonae n dada ako mmezaliwa tumbo moja...darasani kuna mitihani sasa iweje wewe unakaa na mpezni wako mwaka mzima hujampa hata ka QUIZ mpe quiz moto moto akili ipashike na hakikisha akifaulu una mpa ZAWADI tena sio za midoli zawadi zawadi kweli.
[emoji23][emoji23][emoji23] siku zote nikionaga comment yako lazima nifungue kusoma maana siku zote unaandikaga vitu vizuri hata kama sikubaliani na ulichoandika ila the way unawasilisha mtu anavutiwa kusoma. Tuje kwenye hoja yako, mimi hata kama sikupendi hata siku moja sikubali kuachana huku nikiwa mimi ndio mwenye makosa, yaani hata kama nna mpango wa kukuacha nitafanya juu chini tumalize tatizo ambalo naona mimi ndio mwenye makosa kwa hiyo unaweza kunitangazia kibuti leo nikaomba msamaha hata kwa machozi, ukanisamehe yakaisha halafu baada ya tukio kusahaulika nakutafutia kijikosa nakuacha[emoji23][emoji23][emoji23] au nisikutafutie hata kosa nikakuacha kwa amani na upendo.
 
Lakini udhaifu huo huwapata wanaume zaidi.
Hasa wakati wa kusimamia kucha, akitandikwa maswali sawasawa wakati huo, kuyakwepa ni muhali, labda awe na taaluma ya upepelelezi.

Utasikia anajitambulisha nyadhifa zake zote, ukwasi anaomiliki na asilimia ya upendo alionao rohoni mwake.

Ataungama yote kuliko anayoweza kuyaungama kwa muumba wake!

Sasa huo udhaifu ukimpata kichuna aliyetuliza akili, utachunwa hadi mifupa.

Kwa upande wa wanawake, anaweza kuigiza umemkoleza hadi kutoa chozi la maji kabisa, kumbe anakusanifu kwa ajili ya kutimiza lengo lake alilokusudia!
Ndivyo ilivyo wanaume hujisahau hata kama ana mkewe na anamficha kwa kila kitu ila mchepuko unamwagiwa yote subili sasa siku yamgeukie anavyotukana wanawake unajiuliza kati yake na hao mjinga nani na mwerevu nani [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] acha wajifunze kwanza
 
Duuuuh,wanaume tuache kuhonga sana bhn....jali mke na sio demu......pia usjar demu kiasi cha kukopa mkopo duuuh.....hii Kali......
Mm nawaosha tu K bhc......mbele kwa mbele
 
NIKIPOKEA MSHAHARA HUA NAWAZA FUNGU LA KUMI(sijawahi jutia maana hurudi mala dufu)
PILI WAZAZI WANGU.... NIKIWAPA HUWA WANANIAMBIA AHSANTE MWANETU MUNGU ATAKUZIDISHIA... HUA NAITIKIA AMINA.......

MKUU (WANAWAKE) HUA NAWAHESHIMU SABABU NI MAMA ZETU ILA MSIPA WA MAPENZI ULIKATIKA ZAMANIIIII...
 
1 Hawaeleweki.... Utasikia mume wangu ananipenda ila sina hisia nae
2 utasikia nmeolewa ila simpendi mume wangu
Hua nawaza nikija kuowa mim noah itakuaje
Atakuwaje
 
Yaani Pole sana aisee.

Wanaume wenzangu wanaangamia kwa kukosa maarifa. Mungu katuagiza kuishi nao kwa akili za hali ya juu ila wanaume wengi wanatumia nguvu nyingi na mali nyingi wakidhani huo ndiyo itaongeza upendo wasisalitiwe! !!!

Pesa na nguvu usivitangulize mbele kwa mwanamke ukasahau akili. Means, usilizamie penzi maana hujui akili na moyo wa mwenzako unawaza nini!
Msihadaike na maneno ya mdomoni! !!!
Habari wakuu

Japo sio swala jipya ila hata hii ni yenyewe[emoji22]

SITOMWAMINI MWANAMKE TENA

Nimeamua kulielezea hili kuhusu wewe mwanamke tuliyedumu ktk mahusiano kwa muda wa mwaka mmoja. Sio siri kwa sasa umenipa wakati mgumu sana ktk mapenzi na sikutegemea kama ungenifanyia jambo gumu hivi.

Nakumbuka tulipoanza mahusiano yetu na uliponithibitishia huna mtu kabsa kimapenzi nikajikuta nakupenda tena moyo wangu ulishafika tamati kwako ulionyesha mapenzi ya dhati kwangu sikujua kama mwenzangu ulikua unatafuta njia ya kutoka.

Nakumbuka Ulikubali kwenda kunitambulisha kwenu na nilipokelewa vzr na ndugu zako nilifurahi sana kwa kua nilijua sasa nakaribia kupata mke. Lkn nilishangaa kila ninapokwambia nataka kuleta barua ulikataa na kuniambia bado itanijulisha.

Kwakua tulishafikia muda kdg ktk mapenzi yetu lkn kilichonishangaza kingine hukutaka kabsaa tukutane bila kutumia condom. Hii ilinipa maswali kdg ila sio mbaya nilijipa moyo mpaka tutakapofunga ndoa. Kwakua nashukuru mungu hela ya mboga na kuvaa sikosi Maana nimeajiriwa kwenye kampuni moja binafsi.

Siku hiyo ulinambia nikununulie vitu vya ndani upelekeke kwenu Maana wazazi wako wanapata shida vitu ni vya zamani halafu vimechoka.nikakununulia kitanda godoro sofa TV nikamalizia na fridge tukapeleka kwenu.

Baada ya miezi miwili kupita ukaniomba nikupe milioni moja ili ufanye biashara ikabidi nichukue mkopo wa milioni mbili kazini. Nikakupa laki nane ili uanze na hiyo biashara cha kushangaza kupita wiki tu ukawa hupatikani kwenye simu nikija kwenu naambiwa umesafiri tena nashangaa bila kuniaga!!

Kuna siku nilikupigia tena simu akapokea mwanaume akanitukana sana yaani ni mtu ambaye una mahusiano nae mda mrefu kabla yangu daaah we mwanamke una roho ngumu sana. Kwanini ulinificha na kuniaminisha mimi ndo wako ili tuje kuoana!!

Ila namshukuru sana mdogo wako siku nilipoenda kwenu tena ndipo akaniita pembeni na kunieleza kila kitu. Kumbe kwangu ulifanya njia ya mafanikio tu lkn uliyempenda ulikua nae. Yaan vitu nilivyonunua mimi umeenda kupanga chumba unaishia na mwanaume uliyempenda. Pia pesa niliyokupa uliyoniomba kwa nia ya biashara umempa huyo mwanaume kaongezea kanunua bodaboda yote nimeambiwa.

Nakupigia simu unamijibu nyodo na kejeri. Ila sawa mi huu mkopo nitaulipa ila namuachia mungu kwa uliyonifanyia. Umenifanya niyachukie mapenzi na nisimuamini mwanamke yeyote sasaivi. Chozi langu namuachia mungu yeye ndo atahukumu. Najua huu ujumbe lazima ukufikie lkn nikwambie tu mi nakutakia kila la kheri

cc: joanah
 
NIKIPOKEA MSHAHARA HUA NAWAZA FUNGU LA KUMI(sijawahi jutia maana hurudi mala dufu)
PILI WAZAZI WANGU.... NIKIWAPA HUWA WANANIAMBIA AHSANTE MWANETU MUNGU ATAKUZIDISHIA... HUA NAITIKIA AMINA.......

MKUU (WANAWAKE) HUA NAWAHESHIMU SABABU NI MAMA ZETU ILA MSIPA WA MAPENZI ULIKATIKA ZAMANIIIII...
Nimejifunza mkuu
Kumbe mapenzi sasa hayapo kbsa ckujua
 
[emoji23][emoji23][emoji23] siku zote nikionaga comment yako lazima nifungue kusoma maana siku zote unaandikaga vitu vizuri hata kama sikubaliani na ulichoandika ila the way unawasilisha mtu anavutiwa kusoma. Tuje kwenye hoja yako, mimi hata kama sikupendi hata siku moja sikubali kuachana huku nikiwa mimi ndio mwenye makosa, yaani hata kama nna mpango wa kukuacha nitafanya juu chini tumalize tatizo ambalo naona mimi ndio mwenye makosa kwa hiyo unaweza kunitangazia kibuti leo nikaomba msamaha hata kwa machozi, ukanisamehe yakaisha halafu baada ya tukio kusahaulika nakutafutia kijikosa nakuacha[emoji23][emoji23][emoji23] au nisikutafutie hata kosa nikakuacha kwa amani na upendo.
Asante Khantwe kwa hilo.

Ninachoamini ni Mwanamke akikupenda kweli kweli hawezi kukubali eti umuache wakati fika anajua yeye ndio mwenye kosa,hapo ata tafuta hadi marafiki zako wamuombee msamaha....na staki kuamini upate shida zote hizo kuomba msamaha alfu uje nawewe umtafutie tu sabbu mwenzako umuache 🤣 🤣 🤣 sidhani.

Kama ulitaka kumuacha naamini alivyokwambia bwana mimi na wewe basi ilitosha kabisa kua ticket ya kumuacha ila kwakua unampenda huwezi muacha😜

Tayari kwamimi ntakua nishajua unanipenda so ntakusamehe na kwa kua halikua lengo langu kutaka kukuacha bali lilikua kama JARIBU lazima ntakupiga brain wash na surprise ya maana hata kama ulikua na mpango wa kuniacha baada ya kukusamehe unasahau😂😂😂
 
Lakini udhaifu huo huwapata wanaume zaidi.
Hasa wakati wa kusimamia kucha, akitandikwa maswali sawasawa wakati huo, kuyakwepa ni muhali, labda awe na taaluma ya upepelelezi.

Utasikia anajitambulisha nyadhifa zake zote, ukwasi anaomiliki na asilimia ya upendo alionao rohoni mwake.

Ataungama yote kuliko anayoweza kuyaungama kwa muumba wake!

Sasa huo udhaifu ukimpata kichuna aliyetuliza akili, utachunwa hadi mifupa.

Kwa upande wa wanawake, anaweza kuigiza umemkoleza hadi kutoa chozi la maji kabisa, kumbe anakusanifu kwa ajili ya kutimiza lengo lake alilokusudia!
Kweli kbsa tunakuaga wanyonge cna
 
Hukukosea kumuamini ila next time muogope kama ukoma mwanamke ambae hamjamaliza mwaka katika mahusiano lakini haoni shida kukwambia Vocha imeisha,shida hii mara shida ile mara hiki mara kile..Muogope na kaa nae kwa makini aina hiyo ya viumbe.

Mwanamke akikupenda from deep inside hutomuona akikuomba hata sent yako,yupo radhi umuite aanze kukaa kwa mawazo ila sio afungue mdomo wake kukwambia...yani wanawake wakiwa na wapenzi zao hawasemi kitu huwa wana kua kama watoto..MPAKA UMUULIZE "babe what's wrong with you,something isn't ok" atazuga yupo sawa UKIMKAZIA lazima atakwambia tena sio akwambie ili umpe hela au msaada atakupa ile taarifa kama taarifa akiwa hategemei anything from you.

ila ukiona kenge lako hujaliuliza kitu lenyewe lishakwambia,mzee tia X.hata kama ni kuja home kwako anaweza akawa hana nauli,ukimuita kamwe hatokwambia hana nauli utaona atavyo fight na atakuja TU kumbe nauli ukute kakopa,utakuja kugundua siku nyingine kabisa kua alikopa au baada ya kuskia anadaiwa na rafikia ake.

ila wale wanaokuchana "baby ningekuja ila nauli sina" mzeee tia X hamna mwanamke hapo....when a woman love hata huhitaji mtaalamu kugundua Utaona action zao hata kama dem kwao n maskini ila utapenda zile fighting zao...i love girls with true love achana na huyo Nguruwe.

Vuta kiti tulia mwezi au mwaka unaeza usiishe litarudi tena kukuomba msamaha...na ulivyonyweshaga limbwata UTAMSAMEHE....
Dah! Mkuu nmekuelewa sana,itanijenga zaidi maishan japo makovu hayatokwisha mapema
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787]mwingine alitaka kumhonga nchi mwanamke...!!!? Waka-time? [emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Jamaa kanfanya nmecheka cna kma mazuri
 
Back
Top Bottom