Dah! kwahiyo wadau Mzee Yusuph ndo basi tena na taarab yake!

NIMEONA

JF-Expert Member
Aug 4, 2019
3,865
5,683
Hasikiki kabisa huku mtaani, japo nilimuona katika TV kama mwezi au miezi miwili hivi iliyopita akihojiwa. Licha ya kulirejesha jina la zamani la Jahazi (maana alirudi na Safina) katika bendi bado mirindimo haisikiki kabisa huku mtaani.

Nini hiki jamani ili wengine wajifunze?
 
Hasikiki kabisa huku mtaani, japo nilimuona katika TV kama mwezi au miezi miwili hivi iliyopita akihojiwa. Licha ya kulirejesha jina la zamani la Jahazi (maana alirudi na Safina) katika bendi bado mirindimo haisikiki kabisa huku mtaani. Nini hiki jamani ili wengine wajifunze?!!!!
Alirudi kwa muanyezi akaacha nyimbo...... maisha yakawa nadhani hayaendi akarudi na kukuta mashabiki walishamtosa....
 
Aliamua kumrudia mola na kuacha mziki wa kidunya...ila akakaa njaa akaona ugali ni wa muhimu kuliko Quran, maana huwezi kulisha familia mafungu ya Quran......ile anarudi kwenye ugali wake, akakuta mashabiki wameshamwaga mboga.

Waswahili wanasema
Mtaka yote kwa pupa hukosa yote
 
Hasikiki kabisa huku mtaani, japo nilimuona katika TV kama mwezi au miezi miwili hivi iliyopita akihojiwa. Licha ya kulirejesha jina la zamani la Jahazi (maana alirudi na Safina) katika bendi bado mirindimo haisikiki kabisa huku mtaani. Nini hiki jamani ili wengine wajifunze?!!!!
Yani wanaume wazima tukae hapa kujadili taarabu? Hebu tuheshimiane kidogo.
 
Hasikiki kabisa huku mtaani, japo nilimuona katika TV kama mwezi au miezi miwili hivi iliyopita akihojiwa. Licha ya kulirejesha jina la zamani la Jahazi (maana alirudi na Safina) katika bendi bado mirindimo haisikiki kabisa huku mtaani.

Nini hiki jamani ili wengine wajifunze?
Ana nyimbo mpya kwani
 
Njaa imemfanya amkane Mola arudi kwenye Bidaa
Neno Bidaa umetumia kimakosa hapa, ulipaswa utumie neno dhambi

Bidaa sio dhambi ila bidaa ni jambo ambalo limebuniwa (invented) kwamba linahamasishwa kuwa ni jema kufanya ilhali halina ushahidi

Bidaa sio dhambi persee, na mara nyingi hufanywa kwa mlengo wa dini

Sasa kuimba ni dhambi na halifanywi kwa mlengo wa dini hivyo ni dhambi moja kwa moja
 
Mzee alipoamua kuacha muziki na kufanya ibada, ilikuwa ni sawa na kurudi kijijini. Yaani kumrudia Mola ni kuondoka mjini, na huko kijijini kwa Mola hakuna vitamu.

Baada ya kukaa sana huko kijijini kwa Mola, akaona isiwe tabu ngoja aondoke arudi mjini kwa shetani kwenye vitamu.

Ndio maana akarudi na wimbo "Nimerudi Town" kwenye Vitamu.
 
Hasikiki kabisa huku mtaani, japo nilimuona katika TV kama mwezi au miezi miwili hivi iliyopita akihojiwa. Licha ya kulirejesha jina la zamani la Jahazi (maana alirudi na Safina) katika bendi bado mirindimo haisikiki kabisa huku mtaani.

Nini hiki jamani ili wengine wajifunze?
akapotelee mbali huko, hivi inakuwaje mwanaume mwenye mbegu kabisa unaimba taarabu? unalegeza sauti na vidole juu.
 
Aliacha taarabu kwa mbwembwe sana na kuwataka mashabiki wavunje CD walizonunua ati hataki kushea nao dhambi(utadhani pesa aliwasaidia kutafuta)karudi kakuta mashabiki walishamsahau zamaaniii
Alipata vijimilioni vyake mia kadhaa akaona hazitaisha hadi kufa kwake. Baada ya miaka miwili mitatu hela zikaisha na njaa ikamnyemelea. AKASEMA KULIKO KUFA HAPA KWA NJAA NI BORA NIRUDI "MSITUNI"
 
Back
Top Bottom