Mzee Yusuf: Mtoto ni wangu ndio, ila sijui wapi na Lini nilikutana na huyo Mama yake

Quimica

JF-Expert Member
Feb 21, 2018
1,029
1,254
Hii nayo Ituepuke Vijana wote wapambanaji

Huwez kutaka Kufanikiwa kimaisha Bila kuwa na Familia Au Mwanamke Wa uwakika

Vijana wote wanaojitambua Wanatamani Kutulia na Familia Zao na Wengi Wanawaza Ndoa , na hata Wakisalitiwa Watatulia nakutafuta mahusiano mapya Yanayoeleweka wala Hawatabadilika heti kuanza Kulipiza kisasi kwa kulala na kila mwanamke.

Hili la kulala na kila mwanamke mpaka unasahau Ni ulimbukeni Wakisasa

Hii kwa mzee Yusuph ni Aibu.

=====

Moja kati ya habari kubwa zilizo-trend miezi kadhaa iliyopita ni habari ya msanii nguli wa Taarab, Mzee Yusuf kuhusiswa kwamba amemtelekeza na kumkataa mtoto wake.

Mtoto huyo alijitokeza kwenye vyombo mbalimbali vya habari na kujitangaza kama mtoto wa Mzee Yusuf. Licha ya kufanana kuanzia pua, meno, mdomo na vingine vingi, Mzee Yusuf alikataa kata-kata akisema mtoto huyo siyo mtoto wake.

Lakini moja kati ya mahojiano aliyoyafanya na Ayo TV huko Zanzibar hivi karibuni, Mzee Yusuf ameamua kukunjua nafsi na kukubaliana na matokeo baada ya kukumbuka michezo aliyoicheza miaka ya 2002.

"Mara ya kwanza nilipaniki baada ya kusikia kuna ishu kama hiyo lakini nikatulia, nikatafakari alafu nikasema hii ishu niipe heshima yake.

"Awe wangu ni mtoto awe si wangu ni mtoto, tupo katika hatua za mwisho ili kujihakikishia kama ni mtoto wangu na kama si wangu nijue nachezaje na nasaidia vipi. Sina asilimia mia kwamba ni Kiki, sasa hivi tunawasiliana vizuri tunapigiana na kutumiana meseji"

"Kwenye maisha hujui nini kitakutokea mbele, mwaka 2002 aliozaliwa yule mtoto, niliposikia kwamba alizaliwa 2002 imetosha kuelewa kwamba kuna jambo fulani linatakiwa kutokea.

"Kwa sababu mwaka 2002 wakati nazindua album yangu ya (Mwenye Wivu Ajinyonge) nilikuwa na hekaheka nyingi, jina ndiyo lilikuwa linakuwa huenda kweli nilisababisha mambo japo sikumbuki nilikutana na huyo mwanamke wapi mi binadamu na kipindi hicho nilikuwa kijana mambo mengi."

Screenshot_20230918_230632_WhatsApp.jpg
 
Kuna mambo mawili yanaweza sababisha mwanaume asitamani wala kuwaza kutembea na wanawake wengi.

1. Ukosefu wa Nguvu za kiume
2. Ukosefu au upungufu wa pesa

Ila Ni ndoto ya kila mwanaume kutembea na wanawake wazuri kadri iwezekanavyo.

Kama unabisha,
Week offer ya threesome na warembo kadhaa mezani, afu uone Hadi wakina mtoa mada mate yanavodondoka

Cc: mzabzab
 
Umeanza visingizio Sasa,

Usitutoe Kwny mjadala brother,

Wee jikite kwny hoja yako ya kutofanikiwa kwa sababu ya wanawake.

Nami ntakupa hoja zangu kua Unaweza kufanikiwa Bila kujalisha hao wanawake.

Na mifano mingi TU ntakupa
Ni ngumu kukubadilisha mindset hata nikikuelezea hoja zangu ni ngumu kuziamini,tuishi hivyo
 
Back
Top Bottom