GAZETI
JF-Expert Member
- Feb 24, 2011
- 5,292
- 6,773
Ni rafiki yangu ambaye tulisoma wote shule ya msingi, tumekutana huku Dar akaniomba nimsindikize sehemu kupeleka barua ya posa kule Manzese kwa familia moja hivi ya kizaramo. Kabla barua haijafunguliwa yalianza kuulizwa maswali na shangazi mtu. Moja ya maswali hayo yule Jamaa aliulizwa kazi yake akasema ni MENEJA AJIRA WA TAZARA jambo lililosababisha mle ndani watu watabasamu kwa kificho na kusitisha hata mlolongo wa maswali yaliyokuwa yanafuata. Jamaa mimi nafahamu kazi yake ni kukata nyasi kwa ajili ya wafugaji wa ng'ombe na mbuzi ingawa appearance yake hususani kile kitambi na suti aliyovaa siku hiyo inaweza kumfanya mtu aamini anachokizungumza. Kwa bahati mbaya siku moja alikuwa amebeba nyasi hizo, ile anatokea barabarani tu shangazi mtu, mama na ndugu mwingine nao wanapita eneo hilo alazimika kujifunika zile nyasi ili asionekane, na kweli hakuonekana. Sasa wakuu vipi nikiitoa hii siri kwa wahusika maana mama mdogo wa yule binti tunafahamiana.