Dah, Aibu hii sijui nifichue hii siri!!

Dah, Aibu hii sijui nifichue hii siri!!

Najiuliza nitaweka wapi uso wangu wakigundua kuwa hakuwa mkweli
na mimi nilikuwa nafahamu hilo, kwani mama yake mdogo ni jirani yangu.
Swali dogo la kizushi.....

Wakati mnaanza safari kuelekea huko alikuwa hajakutonya kuwa anaenda kudanganya? Manake uongo mkubwa kama huo timu nzima lazima mshirikishwe.

Sasa maadam alikushirikisha, ilikuwaje tena ukakubali kuwa kwenye msafara?

Swali la nyongeza:

Dunia hii ya sasa mpaka mtu aende kuchumbia huyo mchumbiwaji alikuwa hajui jamaa anafanyia wapi kazi? Basi atakuwa mburula mwenye PhD. Kuna tofauti kubwa sana kwa karibu kila kitu kwa mkata nyasi dhidi ya Meneja mwajiri!
 
Tatizo ni kwamba lazima ukweli utakujakujulikana tu.......Sasa sijui atasingizia alikuwa demoted? ...
Situation kama hii ni ngumu sana...
 
Hicho ndo kiherehere, utoe siri ya mwenzio umeulizwa?
Na ukitoa hiyo unayosema siri halafu jamaa akaruhusiwa kuoa au akakataliwa kuoa wewe utafidika nini?

Sasa ndo umefanya nini rafiki mbona unaanza kuniadhir au ulidhan sipatikani huku kwenye forum

Sent from my BlackBerry 9700 using Jamii Forums
 
Swali dogo la kizushi.....

Wakati mnaanza safari kuelekea huko alikuwa hajakutonya kuwa anaenda kudanganya? Manake uongo mkubwa kama huo timu nzima lazima mshirikishwe.

Sasa maadam alikushirikisha, ilikuwaje tena ukakubali kuwa kwenye msafara?

Swali la nyongeza:

Dunia hii ya sasa mpaka mtu aende kuchumbia huyo mchumbiwaji alikuwa hajui jamaa anafanyia wapi kazi? Basi atakuwa mburula mwenye PhD. Kuna tofauti kubwa sana kwa karibu kila kitu kwa mkata nyasi dhidi ya Meneja mwajiri!
Mkuu mi nilikuwa sifahamu chochote, wakati tunarudi yule binti alitusindikiza nikamsikia
akimwuliza jamaa "Hivi hukuniambia kuwa uko TRA?"
akasema hapana nilisema Tazara.
 
Manzese na TAZARA si mbali ni daladala mbili tu au hata mdogo mdogo mtu anafika! Ina maana huyo mchumbiwa naye hajua kazi ya mume mtarajiwa? Kama anaijua na ameridhika nayo kwanini usumbuke au umeuzimikia mzigo?

Lakini kama nafsi inakusuta ni vema ukajitoa kabisa kushiriki katika mchakato huo ila kwa vile hakuna aliyekuuliza juu ya ukweli wa kile alichojibu katika swali aliloulizwa, wewe chapa lapa.

Lakini pia mshauri jamaa apeleke maombi ya kazi hata ya kukata nyasi kandokando ya reli ya Tanzara, anaweza kufanikiwa na siku moja akapandishwa cheo hadi kufikia hapo alipojipimia.
 
Back
Top Bottom