Daftari la mauzo linapendeza lakini ukweli ni kwamba hakuna faida. Mzigo niliojumua 3.8M na kuuza 8.2M umenipa faida ya laki 1 tu

Mkuu huo mzigo wa 3.8m unauza mwaka mzima??..kama hutojali tuambie ni bidhaa gan hzo tukushauri...maana wengne huo mzigo wanauza ndani ya mwezi tu
 
Pia Mzunguko wa hela kule ni mdogo tofauti na huku town.

Imagine DSM hapa fedha inayozunguka Kwa Siku ni zaidi ya 35B Kwa mujibu wa ripoti ya BoT ya Mwaka 2017 so hopefully kwasasa Mzunguko unaweza kufikia 200B na zaidi
Kijijini kwa biashara hapafai. Labda uende sehemu za machimboni au vijiji maarufu kwa kilimo cha mazao ya biashara. Ila hivi vijiji vya kawaida watu wanajilimia kwa ajili ya msosi ni pagumu sana.
 
Kwa hayo mahesabu unakubalije kuwalipa tra 250000. Tra unawalipa kutokana na biashara ilivyo. Mambo ya msiba usiyaingize kwenye biashara.
Mimi niliandikiwa na tra kulipa 100k kwa mwaka yaani biashara nilipoianza Tu, sijui hata itakuwa na uchangamfu UPI kwakweli nilijieleza kuwa ndo naanza na eneo nililokuwapo halina mzunguko wa watu kwa Aina ya biashara Ile niliishia kukosa fedha za Kodi kulipa tra kwa miaka mitatu.

Sasa nalipia nini tra wakati biashara unakaa ofsini unasubiri wateja hata mwezi mzima huoni mteja?!, mwezi unaofata unapata mteja mmoja au wawili haupati tena yaani nikifunga hesabu ya mwaka mzima nimeambulia chini ya laki moja kwa mwaka.

Nasema uhalisia lakini tra hawajui biashara wao ni kupanga Tu ovyo. Kilichonifanya nianzie tra ni kwamba niliwahi ifanyia hiyo biashara mkoa mwingine na ilikuwa vyema ila niliicha baadae na kufanya mambo mengine sasa Hali ilivyokuwa ngumu nilizama tena kwenye hiyo biashara mkoa mwingine sikuwa na mtaji Wa kuiiweka mjini ila ndo hivyo.

Bado sijaripoti tra sijui nitawaelezaje ushauri 😀
 
Ni hesabu nilizopiga katika duka langu dogo nililoweka binti wa kazi mwaka jana, Nimehitimisha biashara ilikuwa inapiga nondo / kujitekenya / BREAK EVEN.

Biashara hii mzigo wa dukani sio wangu hadi pale tu nitapouza, nisipouza naweza kuurudisha, mzigo ukiisha naenda kuchukua mwengine, hivyo sina closing stock

Siku ya jumapili duka hufungwa hivyo kwa mwaka zinabaki siku 261, kuna siku 8 nje ya jumapili binti hakufika, hivyo duka lilifunguliwa kwa siku 253 .

thamani ya mzigo kwa bei niliyouza 8,245,000
thamani ya mzigo kwa bei niliyojumlia 3,867,000
FAIDA YA MZIGO BILA GHARAMA 4,378,000

GHARAMA ZA BIASHARA KWA MWAKA
Frem (laki 1 na nusu miezi 12) - 1,800,000
mshara 100,000 miez 12 - 1,200,000
chakula+usafiri+choo, elf 3@siku -759,000
tra kodi - 250,000 (haikuwa fair kabisa)
jiji, ulinzi, taka - 18,000
misiba, waombaji - 27,000
umeme - 71,000
leseni - 80,000
JUMLA YA GHARAMA - 4,205,000

FAIDA YA MZIGO - GHARAMA ZA BIASHARA = 173,000

Na Hapo niliwakwepa Fire na Service Levy, wangenitoza ningeambulia Sifuri au hasara
Kuna Kitu kinamiss kwenye Hesabu zako.Rudia Tena maelezo.Huo Mzigo wa Milion 3.8 ni manunuzi uliyofanya jumla mwaka mzima?na Je Hiyo Milioni 8.2 ni mauzo uliyofanya Jumla Mwaka mzima?
 
Mimi niliandikiwa na tra kulipa 100k kwa mwaka yaani biashara nilipoianza Tu, sijui hata itakuwa na uchangamfu UPI kwakweli nilijieleza kuwa ndo naanza na eneo nililokuwapo halina mzunguko wa watu kwa Aina ya biashara Ile niliishia kukosa fedha za Kodi kulipa tra kwa miaka mitatu.

Sasa nalipia nini tra wakati biashara unakaa ofsini unasubiri wateja hata mwezi mzima huoni mteja?!, mwezi unaofata unapata mteja mmoja au wawili haupati tena yaani nikifunga hesabu ya mwaka mzima nimeambulia chini ya laki moja kwa mwaka.
A
Nasema uhalisia lakini tra hawajui biashara wao ni kupanga Tu ovyo. Kilichonifanya nianzie tra ni kwamba niliwahi ifanyia hiyo biashara mkoa mwingine na ilikuwa vyema ila niliicha baadae na kufanya mambo mengine sasa Hali ilivyokuwa ngumu nilizama tena kwenye hiyo biashara mkoa mwingine sikuwa na mtaji Wa kuiiweka mjini ila ndo hivyo.

Bado sijaripoti tra sijui nitawaelezaje ushauri 😀
Kwani ww unataka uwalipe hao TRA kiasi gn?
 
Biashara inataka bidhaa inayoisha dukani,irudishwe hapo,Kwa Maelezo Yako inaonekana ulikuwa unauza TU,mpaka mwaka ukaisha bila kuongeza na kurudisha bishaa iliyoisha,Kwa mfano umeuza maji dukani yakaisha,inakubidi ukaongeze hayo maji yaliyopungua dukani ,usisubiri mpaka uuze bidhaa nyingi ndio ukaongeze bidhaa,maana ukisubiri uuze bidhaa nyingine ndio ukaongeze bidhaa ,Kuna wateja unawapoteza wanaohitaji bidhaa ambazo tayari zimeisha dukani. jitahidi bidhaa inayoisha dukani iagizwe ili kuzungusha mtaji.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu mnafanyaje tathmini Bila kuingia kwenye biashara yaani nadharia au hisia embu nifafanulie maana Niko kwa njia panda
Tathmini inafanyika Kwa kuingia sokoni na kuangalia ni biashara ipi ina wateja na inaweza kutoka Kwa urahisi.

Unaweza kujifunza kupitia biashara za wenzako zinazofanana na yako

Mara nyingi tathmini huusisha hali ya Soko, wapi unapopata bidhaa zako iwapo zitaisha, aina ya biashara unayotaka kuifanya, aina ya delivery utakayotumia kuwafikia wateja wako n.k
 
Back
Top Bottom