Dada zetu kubalini kuambiwa ukweli

Onyix

JF-Expert Member
Jan 15, 2014
671
1,000
Leo katika kupeana salamu za Eid Mubarak.. Nikawasiliana na rafiki angu wa kike wa miaka mingi toka form one mpaka sasa kila mtu ana maisha yake... Katika salam za hapa na pale na hatujaonana kama mwaka hv..

Akanialika kwake nikapate chai na chakula cha mchana, basi nikaona sio tabu na vile kitambo hatujaonana nikajikokota mpaka kwake ni mbali kidogo... Kufika pale nikapokelewa vzuri na bidada mpaka ndani..

Kwa kuangali tu nikaona kama bimdada ametoka kuoga sasa maana alikua amejifunga kitenge, kilicho nishtua yule dada zamani alikua na rangi yake nzuri "black beuty" lakn leo nilivyomuona usoni ni mweupe lakin mgongo, vidole, miguu ni "black"..

Basi nikajikaza mwanaume nikaandaliwa chai pale sasa mimi huwa nna kichefuchefu flani hv nikisikia mafuta hasa huwa nayasikia kwa wahudumu wa Bar.. Nadhani ndo ya kujichubua hayo..(sina uhakika lakin maana hata siyajui) ila harufu niliisikia mpaka kwenye kikombe cha chai..

Ile chai ikanishinda kabisa nikajishaua nitakunywa baadae tupige kwanza story. Katika story nikamwambia live kwanini unanichubua akakataa kata kata akasema ndo alivyo hivyo.. Nikampa ushauri pale nikamsema sana anajiaribu kwa kujichubua..

Basi maneno yakamchoma.. Kapandwa na hasira akaanza kutoa maneno pale mwisho wa siku urafiki wetu akauvunja akasema nisimfatirie maisha yake.. Basi nikafukuzwa pale chai na pilau likaingia "shubiri"..

Swali kwa Dada zetu kubalini kuambiwa ukweli.. Unakuta kidada kinakwambia " I need some who can tell me the truth" havijui kama ukweli unauma ukiwaambia wanakasirika..

Acheni kujichubua jamani na ile harufu mnayotoa ya mafuta ya kuchichubua mkitoka jasho si ndo balaa
Eid Mubarak wadada wote mlio tunza rangi zenu.
 

Ndondocha mkuu

JF-Expert Member
Feb 17, 2014
1,501
2,000
Leo katika kupeana salamu za Eid Mubarak.. Nikawasiliana na rafiki angu wa kike wa miaka mingi toka form one mpaka sasa kila mtu ana maisha yake... Katika salam za hapa na pale na hatujaonana kama mwaka hv.. Akanialika kwake nikapate chai na chakula cha mchana, basi nikaona sio tabu na vile kitambo hatujaonana nikajikokota mpaka kwake ni mbali kidogo... Kufika pale nikapokelewa vzuri na bidada mpaka ndani.. Kwa kuangali tu nikaona kama bimdada ametoka kuoga sasa maana alikua amejifunga kitenge, kilicho nishtua yule dada zamani alikua na rangi yake nzuri "black beuty" lakn leo nilivyo muona usoni ni mweupe lakn mgongo, vidole, miguu ni "black".. Basi nikajikaza mwanaume nikaandaliwa chai pale sasa mimi huwa nna kichefuchefu flani hv nikisikia mafuta hasa huwa nayasikia kwa wahudumu wa Bar.. Nadhani ndo ya kujichubua hayo..(sina huhakika lakn maana hata siyajui) ila harufu niliisikia mpaka kwenye kikombe cha chai.. Ile chai ikanishinda kabisa nikajishaua ntakunywa badae tupige kwanza story. Katika story nikamwambia live kwanini unanichubua akakataa kata kata akasema ndo alivyo hivyo.. Nikampa ushauri pale nikamsema sana anajialibu kwa kujichua.. Basi maneno yakamchoma.. Kapandwa na hasira akaanza kutoa maneno pale mwisho wa siku urafiki wetu akauvunja akasema nisimfatirie maisha yake.. Basi nikafukuzwa pale chai na pilau likaingia "shubiri"..

Swali kwa Dada zetu kubalini kuambiwa ukweli.. Unanikuta kidada kinakwambia " I need some who can tell me the truth" havijui kama ukweli unauma ukiwaambia wanakasirika.. Acheni kujichubua jamani na ile harufu mnayotoa ya mafuta ya kuchichubua mkitoka jasho si ndo balaa Eid Mubarak wadada wote mlio tunza rangi zenu.
 

Attachments

  • IMG_20170626_102547.jpg
    File size
    177 KB
    Views
    32

MKWEPA KODI

JF-Expert Member
Nov 28, 2015
28,744
2,000
Kwani papuchi nayo imechubuliwa, acha mambo ya mikoani we Jamaa mbona mambo ya kawaida hayo huku dar
 

Septemba11

JF-Expert Member
Jan 18, 2013
612
1,000
Aiseeeeee, kumbe weupe dili bwana, nina zaidi ya rafiki toka chuo kikuu alikuwa na keusi balaaah ila sikuhizi nayeye anarangi ya mtume hah hah hah japo namuonaga kwa vipicha vyake akiviposti!!
 

ELI-91

JF-Expert Member
Aug 24, 2014
3,591
2,000
Huyo dada atajisikia vibaya wiki nzima, umemharibia sana siku yake. Wanawake hawapendi sana umkosoe kosoe kwenye masuala yanayohusu mwili wake. Jifunze kuwa gentleman badala ya ku focus kwenye vitu vinavyo kukera focus kwenye vinavyokuvutia hata kama ni vichache, kisha umsifie kwenye hivyo vitu.
 

sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
617
1,000
Tabia nyingine ambayo hawataki kuambiwa ukweli ni kuomba omba pesa hovyo..Hata akikualika atataka ulipe bill ilhali hajui mfukoni una ngapi..Tabia za hovyo sana afrika
 

Jc Simba

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
302
500
Kwa kweli kuna mifuta ambayo hata inakuondoa kwenye mood moja kwa moja maana harufu inakua mbaya .

Kiuhalisia wadada wanajiharibu na hayo matakataka ya Kongo wanajichubua na kuharibu ngozi zao halisi.

Nafikiri ni wachache sana ambao hupendeza na kuvutia wengi haya madawa huwaharibu mno na mbaya wanapoteza mvuto MTU anakua na rangi mbili mbili.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom