Wauza Magali kwenye yard muache madharau
Kuna wakati furani nikiwa nasubiri vidola vyangu kutoka kwenye Biashara Yangu huko nje....basi jioni ya jumanne nikapata sms kutoka mwanachi bank pale magomeni kuwa dola zangu zipo account basi nikapitia hapo nikatoa hapo Kama usd 16000 nikabadiri Kama Mia 3 hivi kumaliza heka heka za home nikaenda zangu bar kusukutua koo baada ya ukame wa muda mrefu nikiwa bar nikapata kampani ya Mshkaji mmoja hivi mmoja ya maongezi yetu yalikuwa Ni Magali Na mmoka ya gali lilikuwa linasifiwa kwenye maongezi nayo Ni Toyota blevis basi story hizi zikawasha moto kwenye Moyo wangu basi nikaenda kulala Akili Yangu yote IPO kwenye Brevis niliomba kuche niende show room kununua hiyo gali basi niliamka Kama saa mmoja hivi Nikachukua mpunga wangu nikala pensi Na makobaz nikaelekea magomeni mikumi kwenye show room mmoja hivi Karibu Na kituo nikagonga nikaingia nikaulizwa Nina Shida gani nikajitambulisha nimekuja kununua gali hiyo jamaa akaanza kucheka akaniuliza tena unataka nini ? Nikamjibu nimekuja kununua gali jamaa akanifukuza Nikamwambia tatizo nini akaniambia unataka gali la kuchezea watoto au gali gali...nikamjibu gali akanifukuza wakati natoka Kuna jamaa nikapishana nae mlangoni akamuuliza nimefanyaje mpka ananifukuza akasema mpuuzi analeta Habari za pombe...eti kaja kununua gali yule jamaa akaniita akaniambia mwana njoo kaniingiza mule ndani tena akaniambia chagua kaka...huku wote wakiwa attention Na Mimi...basi nikamwambia naitaka hii nikamuonyesha Brevis nyeupe akaleta funguo akanifungulia kila mahala baada ya kukagua nikamuuliza bei gani jamaa akasema mil 13 nikamwambia sawa nakupa wapi akaniongoza kwenye kiofisi humo humo yard basi jamaa akastaajabu nazama mbele natoa midola nawalipa HeLa yao ghafla mambo yalibadirika nikaamza kuitwa bosi mara Mkubwa njoo huku Na heshima kibao nikimiminiwa....
Ushahidi brevis yenyewe hiyo hapo