Dada wa mapokezi Avic Town hajui huduma kwa wateja

Leo naona ni siku ya kutoa kero.Kuna hizi ATM za mabenki ambazo kipindi cha holiday hawaweki pesa basi unazunguka mpaka unachoka.Hivi ya mabenki yana akili kweli?
CRDB wanaongoza kwa tabia hii, yawezekana wamesharidhika sana.
Ndivyo ilivyo kwa ofisi nyingi sana. Zamani nilifikiri ni ofisi za umma tu, kumbe hata private pameoza sana, poor customer care.
 
Kuna hii bar hapa Kimara kona. Ma baa medi wanadharau watu Sana hadi uwape soda ndio achangamke. Vinginevyo utaendelea kupiga miayo.
Kuna siku bana nimetulia zangu bar ya jiran na home sa kumi kumi hivi nacheki game ya chelsea na Man u huku nakula zangu malta duh kuna baamedi mmoja akaniletea dharau moja kubwa sana "unakuja kujaza siti tu masaa yote hyo unakunywa malta moja tu halafu hiyo inaleta nzi na nyuki kwanza inashibisha tu haulewi wala nini kujaza tumbo tu" daah nilipandwa na hasira kipind kile bia sh 2000 nikaagiza bia 5 nikazimwaga kwenye maua halaf nikamuuliza umeridhika au unataka nikaku****** nikupe hela ya kununulia chu** ndio uniheshimu? huyooo nikasepa zangu sikuangalia nyuma.
 
Yan kuna siku nilienda bank ya KCB, kilichotokea muhudumu aliniangalia balaa, nilivovaa Na huduma niliyokuwa nahitaji Ni tofauti,
ndo hivo
 
Oceanrod hosp je! Bora hata ingekua ya kulipia na sio bure! Manes hawana kauli kabisa cjui kama n wote lkn sijawah kukubahatika....poor customers care
 
Pole bwana mkinga nawafahamu nyinyi mnamihela tatzoo ndo hilooo
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
Ha ha ha hii kali
 
Mkuu umenikumbusha mbali, mwaka 2009 niliwahi kwenda duka la mariedo pale benjamin mkapa tower, kuna mdada pale na haka kaumbo kangu kama sijala mwezi mzima akawa ananitazama kama vile niliyepotea njia.
Nikawa namuuliza bei ya vitu mbalimbali ananijibu kama vile tuna ugomvi.
Mwisho akaona naanza chagua akawa ananitazma kwa hasira.
Nilipochukua bahasha ya kaki yenye michuzi nikaweka kaunta kumlipa maana nilichagua vitu vingi ndipo akaanza nikenulia na kunichekea sana.
Tatizo people judge other people kwa mavazi na vitambi.
Wengine hata tule vipi afya ilishaweka mgomo
Mwiso wake akakuomba namba au?
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
DAA NIMECHEKA BALAA 😡😡😡😡😡😡😡😡
 
Nafikiri tuna tatizo kubwa sana la "Mikataba ya Huduma kwa Wateja" katika maeneo mengi ya kazi.
Hili suala liliwahi nikumba nimeenda pale AVIATION HOUSE-Kitunda;nilikuwa nimeenda kusajili kindege cha kampuni yetu pale,tulikuwa tumekikodisha toka nchi fulani ya Afrika sasa tunataka kubasilisha kitu inaitwa "Basement" ili tuanze kufanyia kazi Bongo.

Sasa nimefika pale reception namkuta dada anaelekea kwenye umama hivi,ninamuuliza "fulani" atakuwa ghorofa namba ngapi na chumba namba ngapi?Nimeelekezwa kwake nije nifuate taratibu za Ukaguzi ili nisajili ndege "yangu" hapa Bongo.....Yaani lile neno kusema "ndege yangu" na jinsi nilivyo,ni kama vikamchefua sana yule mhudumu...Maana akiniangalia nina pensi ya kiwindaji,safari boot na short sleeve double pockets.Mwili usio na shukrani sina cha kitambi wala rangi ya pesa...Alinipokea vibaya sana,yaani kunipa ile pass alinipa kwa mashaka sana....Nikajiuliza sana,hivi kwani mimi nafananaje!?Ilibdi nikajiangalie hadi kwenye kioo nyumbani
ULIKOSEA UNGESEMA NDEGE YA KAMPUNI, UMEMCHEFUA KUSEMA NDEGE YAKO WAKATI YEYE ANAJUA NI YA KAMPUNI
 
Aiseeee hata wale watu wa parking za kwenye malls na magorofa ya kibongobongo wana zereu hatari.Kuna siku mtu wa mbele yangu alipewa parking mbaya tu ya kuzunguka nyuma ya jengo wakati mimi niklikuwa nyuma yake nikaonyeshwa parking nzuri.Alafu ile nashuka ananiambia hii gari ndio inastahili kupack hapa.Nilimtolea jicho nikamwambia acha dharau hakuamini.
 
Nimeenda avic town kuangalia bei za nyumba nijaribu kulinganisha na gharama za ujenzi duh dharau niliyoipata nadhani bado tunahitaji kuajiri wageni katika sekta zetu, pale mapokezi nimekuta wadada wawili nauliza bei za nyumba wananijibu nyumba ya chini kabisa inaanzia milioni 120 nikaomba nionyeshwe ilivyo ......akagoma huku akinishangaa muonekano wangu, nadhani alitegemea aje raia wa kigeni we dada kaa ukijua siku hizi hela tunazo sisi wananchi wa kawaida wapiga dili wote wameishiwa kama unakumbuka leo walikuja dada mmoja amevaa baibui na mtandio na mwingine amevaa suruali ya jeans na top ya pink......usidharau watu kutokana na muonekano
Tatizo la kuajiri vihawara visivyokuwa na qualification ya sales /marketing basi vinajiona ndio vyenye mali ....stupid.
 
Nimeenda avic town kuangalia bei za nyumba nijaribu kulinganisha na gharama za ujenzi duh dharau niliyoipata nadhani bado tunahitaji kuajiri wageni katika sekta zetu, pale mapokezi nimekuta wadada wawili nauliza bei za nyumba wananijibu nyumba ya chini kabisa inaanzia milioni 120 nikaomba nionyeshwe ilivyo ......akagoma huku akinishangaa muonekano wangu, nadhani alitegemea aje raia wa kigeni we dada kaa ukijua siku hizi hela tunazo sisi wananchi wa kawaida wapiga dili wote wameishiwa kama unakumbuka leo walikuja dada mmoja amevaa baibui na mtandio na mwingine amevaa suruali ya jeans na top ya pink......usidharau watu kutokana na muonekano
Kabisa reception wadada huwa na dharau Mimi huwa naondoka bila kuaga halafu naenda tena siku nyingine nikiwa na namba ya boss wao .kuna eneo hizi Tira wale Wa vyeti vya kuzaliwa ,Nhif wale wa bima
 
Nafikiri tuna tatizo kubwa sana la "Mikataba ya Huduma kwa Wateja" katika maeneo mengi ya kazi.
Hili suala liliwahi nikumba nimeenda pale AVIATION HOUSE-Kitunda;nilikuwa nimeenda kusajili kindege cha kampuni yetu pale,tulikuwa tumekikodisha toka nchi fulani ya Afrika sasa tunataka kubasilisha kitu inaitwa "Basement" ili tuanze kufanyia kazi Bongo.

Sasa nimefika pale reception namkuta dada anaelekea kwenye umama hivi,ninamuuliza "fulani" atakuwa ghorofa namba ngapi na chumba namba ngapi?Nimeelekezwa kwake nije nifuate taratibu za Ukaguzi ili nisajili ndege "yangu" hapa Bongo.....Yaani lile neno kusema "ndege yangu" na jinsi nilivyo,ni kama vikamchefua sana yule mhudumu...Maana akiniangalia nina pensi ya kiwindaji,safari boot na short sleeve double pockets.Mwili usio na shukrani sina cha kitambi wala rangi ya pesa...Alinipokea vibaya sana,yaani kunipa ile pass alinipa kwa mashaka sana....Nikajiuliza sana,hivi kwani mimi nafananaje!?Ilibdi nikajiangalie hadi kwenye kioo nyumbani
[emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
Alikuwa anahofia vitz mzee. Alijua nayo ni ya mkopo pengine[emoji85]
 
Back
Top Bottom