Dada wa mapokezi Avic Town hajui huduma kwa wateja

Dada wa mapokezi Avic Town hajui huduma kwa wateja

Alikuwa anahofia vitz mzee. Alijua nayo ni ya mkopo pengine[emoji85]
Jamaa aliniboa sana acha Bodaboda wacheke...[emoji1] [emoji1] [emoji1] habari mbaya ni kwamba ile shell ishavunjwa. Sasa wanauza kokoto na mchanga
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
[emoji23][emoji23][emoji23]Hii yako kali natamani nikuone unafanana na mtoto aliyeiba gari kwao au house boy,, maana vitz siyo ya kupigiana kelele hvo
 
Mi

Mimi nashindwa kuelewa hivi kwanini wahudumu wasipewe mikataba inayowafukuzisha kazi pale wanapokosa good customer care? kwenye mahoteli ni zero,ukija mahosipitali nako zero yaani ujinga ujinga tu!
Hili nalo nikama sifa moja wapo ya kuwa mfanyakazi kutoka Tanzania
Na wakinyimwa ajira na kupewa wageni wanaanza kulialia eti haki yao na wakiajiriwa ndio wanafanya utumbo wa namna hiyo
 
Nimeenda avic town kuangalia bei za nyumba nijaribu kulinganisha na gharama za ujenzi duh dharau niliyoipata nadhani bado tunahitaji kuajiri wageni katika sekta zetu, pale mapokezi nimekuta wadada wawili nauliza bei za nyumba wananijibu nyumba ya chini kabisa inaanzia milioni 120 nikaomba nionyeshwe ilivyo ......akagoma huku akinishangaa muonekano wangu, nadhani alitegemea aje raia wa kigeni we dada kaa ukijua siku hizi hela tunazo sisi wananchi wa kawaida wapiga dili wote wameishiwa kama unakumbuka leo walikuja dada mmoja amevaa baibui na mtandio na mwingine amevaa suruali ya jeans na top ya pink......usidharau watu kutokana na muonekano
Pole mkuu me nakumbuka nilikagua mpaka vyooni nyumba za class zote,
 
..tatizo Lipo Avic Town umelileta JF,kwann tusiamini wewe ndo una tatizo??
 
Nafikiri tuna tatizo kubwa sana la "Mikataba ya Huduma kwa Wateja" katika maeneo mengi ya kazi.
Hili suala liliwahi nikumba nimeenda pale AVIATION HOUSE-Kitunda;nilikuwa nimeenda kusajili kindege cha kampuni yetu pale,tulikuwa tumekikodisha toka nchi fulani ya Afrika sasa tunataka kubasilisha kitu inaitwa "Basement" ili tuanze kufanyia kazi Bongo.

Sasa nimefika pale reception namkuta dada anaelekea kwenye umama hivi,ninamuuliza "fulani" atakuwa ghorofa namba ngapi na chumba namba ngapi?Nimeelekezwa kwake nije nifuate taratibu za Ukaguzi ili nisajili ndege "yangu" hapa Bongo.....Yaani lile neno kusema "ndege yangu" na jinsi nilivyo,ni kama vikamchefua sana yule mhudumu...Maana akiniangalia nina pensi ya kiwindaji,safari boot na short sleeve double pockets.Mwili usio na shukrani sina cha kitambi wala rangi ya pesa...Alinipokea vibaya sana,yaani kunipa ile pass alinipa kwa mashaka sana....Nikajiuliza sana,hivi kwani mimi nafananaje!?Ilibdi nikajiangalie hadi kwenye kioo nyumbani
Mkuu umenichekesha sana eti " pensi ya kama ya muwingaji", Anyway ni kweli customer care kwa nchi bado sana sijui huwa wanasomea chuo gani maana kila ofisi iwe private or government kuna poor reception na malalamiko ni mengi, Sasa huwa najiuliza mabosi wa ofisi hizo kwa nn huwa hawalifanyii kazi tatizo hili maana limeoya mizizi ofisi nyingi
 
Jamaa yangu ni mkandarasi hana majivuno kavaa simple na mwembamba alitaka akanunue pavement blocks za mradi zingegharimu kama zaid ya 80m. Akakutana na vidada vikamchangamkia namna wangefanya yeye apate chake na wao pia chao maana wanajua mahesabu kwani pavers huwa mara nyingi zinabaki baada ya kazi. Mshikaji akasema hapana atanunua anazohitaji na kulipa. Pale pale hawakumkopesha wakaanza kumdhihaki...ooh unakuta kijitu kimemaliza Chuo kinajifanya kiadilifu utakufa maskini. Yaan walichukia sana hao Dada. jamaa akalipia mzigo akasepa. The guy is worth billions wealth wakati hao wadada anaweza waajiri. Hii ndo hali halisi ukiwa na mwonekano simple kumbe millionaire.
Yaani nchi hii sisi wembamba halafu tunavaa simple watu wanatuchukulia poa sana.
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
Duh mkuu polee...people sucks
 
Watoa huduma za mbele ya ofisi ... huwa tunawaita Gate Keepers, ili mambo yako na siku yako isiharibike ni vema sana nasi wateja tukajaribu kujiangalia the way we are. Sometimes they are very rude ila ni vema tujue huwezi kuwa 100% muda wote ...
 
Nakumbuka day moja dadaangu mmoja yupo ktk finance flan alinidirect pale Brela kwa mtu mmoja ili anipe mwongozo wa kusajili kampuni yetu binafsi, sasa akanambia ukifika njoo ghorofa flani chumba namba flani, daa c nikapanda nikagonga kile chumba nikaingia nikawaona wadada na wanaume wamekaa meza moja wamezunguka nikasalimia hakuna aliyeitikia nikauliza mr Kobelo nimemkuta? Hakuna aliyeitikia daa nkasimama sekunde kadhaa nkaona najidhalilisha nkafungua mlango nkatoka,mara jamaa akaja akanikuta pale nje akanikaribisha chumba kilekile basi akawaambia huyu mdogo wangu anataka hiki na hiki wale wakaanza kutabasamu ss mimi hasira zikawa zipo juu sana kwa dharau zao za mwanzo jamaa akasema nimpe dada mmoja maelezo ili amisaidie kuandaa memorundum,yule dada akaja akajifanya kunipa maelekezo kinafiki nikamsikia mwisho akataka kazi yakuandaa nimpe yy sasa nikamwambia asante kwa ufafanuz kazi hii kuna rafiki yng mwanasheria ataifanya ntampa yy hela, akabembeleza nkamchinjia baharini, nikamuaga bro yule nkasepa nkamgeukia nkamwanbia 'sentano yangu hupati'
 
uliyatafuta mkuu ndege ya kumpuni ukasema yako unazani huyo mmama roho haimuumi?? na usikute kakuzid umri sasa anajiuliza umepitia njia gan kufanikiwa kuliko yeye mwenye umri mkubwa hapo ndo tatizo linaanza
Mkuu santos mtn hivi vikampuni ni kujifichia tu;ili watoto wasije filisiwa utakavyowaachia.
Sasa "wivu" wa nini kindege chenyewe ni C207 cha kuendea porini na safari za ufukweni na familia.Ni kama bajaji tu,tofauti ni kuwa hiki kinapita angani kingine nchi kavu.Nafikiri concern sio "ndege yangu" ni ile "Huduma kwa Wateja"
 
Yaani nchi hii sisi wembamba halafu tunavaa simple watu wanatuchukulia poa sana.

Shida iko wapi chief? Nawaza umeamua kuvaa simple ili wakuchukulie poa japo unaweza kuvaa kinyume na simple. Wanaotishwa na vitambi ni majehu.
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
Hahahaa!, kuna tukio linaloendana na hili limewahi kunitokea....kipindi nilivaa shati ambalo halijapigwa pasi. Binadam kazi sana!, hahahaa! CC wote wanaojiita ma bishop
 
Watu wana dharau sana.

Siku moja natoka Bagamoyo niko na Vitz. Naangalia mshale wa Petrol inaelekea kukata. Niko pale JKT karibu na njia panda ya kwenda Kunduchi nikaingia shell. Kulikuwa na foleni kidogo, nikasogeza gari nikafungua tank nikamwambia muhudumu jaza full tank. Jamaa akaanza dharau, utalipa? Nikamjibu kwanini nisilipe, tukarushiana maneno pale mwisho wake akajaza. Nikampa pesa yake nikaondoka. Sasa sijui alikuwa anahofia nini
pole sana nimecheka sana daaaaa
 
Nimeenda avic town kuangalia bei za nyumba nijaribu kulinganisha na gharama za ujenzi duh dharau niliyoipata nadhani bado tunahitaji kuajiri wageni katika sekta zetu, pale mapokezi nimekuta wadada wawili nauliza bei za nyumba wananijibu nyumba ya chini kabisa inaanzia milioni 120 nikaomba nionyeshwe ilivyo ......akagoma huku akinishangaa muonekano wangu, nadhani alitegemea aje raia wa kigeni we dada kaa ukijua siku hizi hela tunazo sisi wananchi wa kawaida wapiga dili wote wameishiwa kama unakumbuka leo walikuja dada mmoja amevaa baibui na mtandio na mwingine amevaa suruali ya jeans na top ya pink......usidharau watu kutokana na muonekano
Watanzania tuna matatizo sana tena sana una kuta hiyo kazi wangepewa wakenya basi wangekimbilia huku kwenye mitandao kusema ooooh AVIC TOWN wanapendelea sana raia wa kigeni. Tatizo watanzania tunapenda kuchezea sana kazi na hatupendi kutimiza majukumu yetu tumejaa dharau kupita kiasi na hasa mabinti/wasichana wana hili tatizo...
Watu kama hao ulikosea kutowapa vipande vyao na kuhakikisha umemuona boss wao... mimi huwa siwakwepeshi watu kama hao....
 
Back
Top Bottom