Dada kaanza kampeni mapema mno!

KENZY

JF-Expert Member
Dec 27, 2015
26,213
56,849
Kaanza mapema mno na hakika anaogopa upepo unaomtikisa!,Tena zaidi anaogopa upepo wakaka yake maana inaonekana upepo wa kaka ni mkali zaidi unampa shida,madira yake yanapeperuka huku na kule!.

Hakika dada hawezi kuvaa viatu vya kaka vimemshinda ndio maana ameanza kuviponda!.. niwaambieni yule mzazi wa kijani aliemzaa dada na kaka sasahivi ameharibikiwa kwani hawana sera tena zaidi ya kupondana wenyewe!,Moto unawaka tena moto wakijani.

Dada unamlaumu kaka kwani hujui sahivi hayupo..? Wakati akiwepo wewe si ulikuwa msaidizi wake..! Jua Kila anguko lake ni lako pia!,picha yake ilikuwa kubwa nawe tengeneza yakwako pasipo kukanyaga picha ya kaka! Adui zako sio waliokufa bali waliohai!.

Umefanya upatanisho na adui zako kwa kuingia mtegoni sasa umekosa adui umeanza kugusa visivyojitetea!. Sasa ni hivi kama alivyopita nawe utapita ila fahamu haya,hata Kama leo Kaka atasemwa vibaya ila hataacha kukumbukwa kwani toka katika ukuaji wake kazi zake nzuri zinafahamika. Asingeweza kukaa miaka kumi na bwana yule kama asingefanya vyema!. Ukweli huonekana dhahiri dada.

Ulipo ndipo kipimo kilipo sasa ni muda wa kufanya kazi na sio masimango,uzuri wa mtu hauji kwa kumponda mwengine tena ambae hawezi kusema!. wanaokupigia makofi hivi sasa wanakudanganya maana usitegemee uliozaliwanao wakakusaliti wakati wanajua umeshika sufuria la pilau na wanataka wazijaze sahani zao!. Tena wanataka ulegeze mikono ili wazijaze vizuri! Kaka yako alikaza mikono kwani alijua tabia za ndugu zake!.

Sisi unaotuona jamaa wa koo nyengine ndio tunaolima na kujaza wali hilo sufuria!,piganeni,gombanieni lakini msijisahau tunawaona na wewe ndio tunakuona vizuri zaidi.

Nikukumbushe ule muda bado haujafika,kazi ya mikono yako itakuja kuhesabika kushinda kazi ya mdomo.
 
Dada wapambr wanamjaza upepo. Simba wa Yuda alikuwa kiongozi sahihi kwa wakati sahihi na alipenda Nchi yake na watu wake na kuitetea kwa nguvu zake zote.

Nilimsikia Dada akisema anampango wa kuingiza TPA ubia na watu. Aache JPM aiongeze kina kisha aiuze? 2025 ndipo CCM watajua hatutaki matani.
 
Nchi ina zaidi ya watu millioni 60, ninachojiuliza ni mshika remote ana nguvu na akili nyingi kiasi gani kuwazidi hawa wote?

Na je, kama jaribio lake (lao?) la kwanza kumweka mtu wao lilishindikana 2015 litawezekana nyakati hizi ambapo hekaheka nchi inazopitia zimewafungua zaidi watu macho? Nawazaga tu
 
Dada hajiwezi..ameenda kuazima mamruki kutoka agosm ili wamsaidie..ila kaenda chaka mana wale jamaa ni madalali wa rasilmali za nchi..hawana uchungu na wananchi..mwisho wasiku lawama zote kwakwe..

Dada hakubariki kafeli pakubwa kama angejua 2025 angekaa pembeni tu..mana anenda kujitafutia aibu ya maisha.

#MaendeleoHayanaChama
 
Dada wapambr wanamjaza upepo. Simba wa Yuda alikuwa kiongozi sahihi kwa wakati sahihi na alipenda Nchi yake na watu wake na kuitetea kwa nguvu zake zote. Nilimsikia Dada akisema anampango wa kuingiza TPA ubia na watu. Aache JPM aiongeze kina kisha aiuze? 2025 ndipo CCM watajua hatutaki matani.
Hakuwa mtu sahihi alikuwa muuaji na katili sana mwizi wa ubabe huku akiwahadaa wajinga wajinga kwamba yey ni kiongozi wa wanyonge alikuwa muongo ndio maana anapendwa na wasio ma elimu
 
Mkiwamaliza wakinzani wenu ndipo mtaanza kutafunana ninyi kwa ninyi.Kazi yetu ni kuwasogezea kuni na kuwanolea visu vilivyo butu tu.😂😂😂😂😂
 
Kaanza mapema mno na hakika anaogopa upepo unaomtikisa!,Tena zaidi anaogopa upepo wakaka yake maana inaonekana upepo wa kaka ni mkali zaidi unampa shida,madira yake yanapeperuka huku na kule!.

Hakika dada hawezi kuvaa viatu vya kaka vimemshinda ndio maana ameanza kuviponda!.. niwaambieni yule mzazi wa kijani aliemzaa dada na kaka sasahivi ameharibikiwa kwani hawana sera tena zaidi ya kupondana wenyewe!,Moto unawaka tena moto wakijani.

Dada unamlaumu kaka kwani hujui sahivi hayupo..? Wakati akiwepo wewe si ulikuwa msaidizi wake..! Jua Kila anguko lake ni lako pia!,picha yake ilikuwa kubwa nawe tengeneza yakwako pasipo kukanyaga picha ya kaka! Adui zako sio waliokufa bali waliohai!.

Umefanya upatanisho na adui zako kwa kuingia mtegoni sasa umekosa adui umeanza kugusa visivyojitetea!. Sasa ni hivi kama alivyopita nawe utapita ila fahamu haya,hata Kama leo Kaka atasemwa vibaya ila hataacha kukumbukwa kwani toka katika ukuaji wake kazi zake nzuri zinafahamika!.
Asingeweza kukaa miaka kumi na bwana yule kama asingefanya vyema!. Ukweli huonekana dhahiri dada.

Ulipo ndipo kipimo kilipo sasa ni muda wa kufanya kazi na sio masimango,uzuri wa mtu hauji kwa kumponda mwengine tena ambae hawezi kusema!.. wanaokupigia makofi hivi sasa wanakudanganya maana usitegemee uliozaliwanao wakakusaliti wakati wanajua umeshika sufuria la pilau na wanataka wazijaze sahani zao!. Tena wanataka ulegeze mikono ili wazijaze vizuri!,Kaka yako alikaza mikono kwani alijua tabia za ndugu zake!.

Sisi unaotuona jamaa wa koo nyengine ndio tunaolima na kujaza wali hilo sufuria!,piganeni,gombanieni lakini msijisahau tunawaona na wewe ndio tunakuona vizuri zaidi.

Nikukumbushe ule muda bado haujafika,kazi ya mikono yako itakuja kuhesabika kushinda kazi ya mdomo.
Kwa Nini mafanikio ya Kaka hamsemi ni yake pia.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom