D Voice ndio future ya muziki wa bongo: Wasanii wa kibongo kazini kwao kuna kazi

sinza pazuri

JF-Expert Member
Aug 16, 2014
2,525
7,377
20231117_115659.jpg

Msanii wa kizazi cha leo na kesho aliyetambulishwa recently na lebo namba moja Africa ya WCB Wasafi.
Kwa jina anaitwa D Voice aka Jini aka London Boy au Temeke Boy.

Huyu ndio future ya muziki wa bongo kwa ujumla. Ndio anaenda kuibeba mabegani industry ya muziki wa bongo ni suala la muda tu.

Anakipaji kikubwa sana cha kuimba ana vocal hadimu mno kama unamsikia Issa Matona alafu kama unamsikia Misambano alafu kama unamsikia TX Moshi kwa mbali kama Kassim Mganga.

Anaweza imba kila aina ya muziki lakini nguzo yake kubwa ni muziki wa pwani haswa singeli na lebo inajaribu kutafuta biashara ya singeli nje ya mipaka so dogo atarajie kutembea sana kulitafuta tobo.

Dogo anaandika sana, ameshaandika hitsongs nyingi za singeli za kina mzee wa bwax kina meja kunta na mabongofleva wengine kibao. Ukisikiliza album yake utasikia skills za uhandishi uloshiba na fleva.

Ana star look kitu ambacho ni muhim sana kwenye sanaa na hajapoa kash kash za showbiz anaziweza ni ishu ya muda tu. Umri wake pia ni mdogo kuendana na walaji wakuu wa muziki wa sasa.

Kila la heri mdogo wetu nakutakia mafanikio katika safari yako ya kuwa big supastaa duniani.

Nakushauri tu endelea kuonesha nidhamu kwa kila mtu na kubwa uache tabia yako ya mishangazi ushajipata sasa.

Bongofleva tumepata zawadi kubwa sana, shukran sana kwa Diamond Platnumz na pia kwa Zuchu kwa kuiona hii almasi kwenye mchanga.
 
View attachment 2816392

Msanii wa kizazi cha leo na kesho aliyetambulishwa recently na lebo namba moja Africa ya WCB Wasafi.
Kwa jina anaitwa D Voice aka Jini aka London Boy au Temeke Boy.

Bongofleva tumepata zawadi kubwa sana, shukran sana kwa Diamond Platnumz na pia kwa Zuchu kwa kuiona hii almasi kwenye mchanga.
Hadimu = adimu, uhandishi = uandishi. Wewe chawa jifunze kuandika
 
View attachment 2816392

amu kwa kila mtu na kubwa uache tabia yako ya mishangazi ushajipata sasa.

Bongofleva tumepata zawadi kubwa sana, shukran sana kwa Diamond Platnumz na pia kwa Zuchu kwa kuiona hii almasi kwenye mchanga.
Kwa jinsi nilivyo sikiliza ile album jana naweza sema hii ni sajili ya kitapeli kama ya simba sc kwa ayubu
 
Nidhamu, kuto kukata tamaa ,kujituma, kuwa flexible na kukubali ushaur mzuri, majivuno , kuridhika na kiburi Cha mafanikio hupoteza wengi.....

Yupo vizuri ila hamfikii RICO DALLAS (DALLAS) kukosa connection na watu wa kukuongoza unaweza kua na kipaji na usifike popote...
 
Nidhamu ndio upoteza wasanii wengi na vijana wengi. Kipaji sio kila kitu nidhamu ndio imefanya Diamond awe hapo alipo.
 
Back
Top Bottom