UKWAJU WA KITAMBO
Member
- Feb 6, 2024
- 40
- 50
ELIMU KWA WASANII WA BONGO
Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere aliwahi kusema kipindi cha harakati ya kugombania uhuru kuwa elimu ndio ufunguo na msingi wa kila kitu. Nukuu ya Mwalimu ilisema, "Hakika vita vya sasa sio vya mashoka wala upindi na mshale... Msishangae ndugu zangu, najua mnajiuliza! Vita vya sasa ni kujikomboa na umaskini na ujinga, na kufanya hivyo hatuna budi tusome. Elimu ndio ufunguo wa maisha yetu sote."
Maneno hayo yaliyozungumzwa miaka 50 iliyopita bado yanafanyiwa kazi na wasanii wetu wa Swahili Hip Hop.
Wasanii wamekuwa mfano mzuri kwa jamii yetu, na hivyo basi wanasisitiza kushikilia ndoto yako ya elimu kwani ndio ufunguo wa kila kitu.
Ni suala lisilopingika kwamba elimu ya darasani ina nafasi yake katika uendeshaji wa maisha, ingawa inaweza isiwe na mchango wa moja kwa moja katika sanaa ya muziki wa Bongo Fleva. Wasanii wengi wa Bongo Fleva wameishia darasa la saba. Baadhi yao wamebahatika kuishia kidato cha nne, na wachache sana wana elimu ya kidato cha sita au na chuo kikuu. Hali kadhalika, wasanii wengi (zaidi ya 90%) nchini Tanzania hawana elimu ya muziki au sanaa. Kukosekana kwa elimu hiyo kunachangia wasiwe na maarifa ya ziada ya kuweza kusimama vizuri katika muziki wao.
#FUNGUKA.
Nitajie majina ya wasanii wenye kisomo Bongo ..