CV ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Stephen Werema

CV ya Mwanasheria mkuu wa Serikali Jaji Stephen Werema

Mwaka 2011 nilishawahi kusema huyu mtu uwezo wake ni mdogo sana na nikasema kuna haja ya kupitia kwa kina hukumu alizotoa akiwa jaji.Ni lazima atakua alitoa hukumu kandamizi au zenye upendeleo

Tukileta CV yake ili ikamilike nadhani na nukuu zake alizowahi kutoa ziwekwe ili kuitendea haki CV hii nzito iliyosheheni usomi na experience!
Mkuu hapa nakuunga mkono, maana hata wahadhiri CV zao zinaonyesha machapisho na tafiti walizofanya au kushiriki. Kwa Jaji, judgement alizozitoa ni sehemu ya achievement, zingepaswa kuonyeshwa kwenye CV yake (sina uhakika lakini kama wanasheria wana huu utaratibu, maana ni profession yenye mikwara sana na members wa hii profession wana rigidity ya ajabu)
 
Huyu pamoja na hiyo cv hana uwezo kama alionao chenge.Kuna mambo anafanya unaweza kumshangaa.
 
Wanaoitwa wasomi Tz... wengi wao miaka mingi darasani, uwezo mdogo kichwani.

Naunga mkono hoja yako mkuu! Nilimwambia Le mutuz kuwa wasomi wa bongo hawana tofauti na wasiosoma coz hawana msaada wowote kwa jamii inayowazunguka. Alinikejeli coz nae ni miongoni mwao waliokaa darasani ila wako hoi kiufaham!! Mfano mzuri, mtazame prof Muhungo, kweli madudu anayofanya kwenye wizara husika utadhubutu kumwita prof!? Pili, mtazame prof Sifuni Mchome, anachokitendea wizara ya elimu mpaka kuifanya Tz kuwa ya mwisho duniani kwa kuwa na viwango vya chini vya ufaulu, utadhubutu kumwita prof??!! Ndo maprofesa wetu hao, "vichwa vikubwa, ubongo wa mende"!!
 
CV za kusoma ni mbwembwe hasa hasa kwenye mfumo Elimu ambao lengo lake ni kutoa msomi mwenye mawazo tegemezi. Refer kwenye objectives and aims of "Colonial Education", hata baada ya uhuru mfumo haukabadilishwa bali tulibadilishiwa content tu, mbaya zaidi tukakewekewa "Unyerere." So sishangai kwa CV hii bado Werema akawa hivyo alivyo ni mfumo, kuna watu wana uwezo wa "kufaulu" mitihani lakini IQ yao ni ndogo sana. Na viongozi waliotufikisha hapa wote wana CV zilizotukuka lakini wameboronga mwanzo mwisho.
So kwa Werema and etal tusishangae madudu ndivyo walivyo, mfumo uliwabeba na sasa na hizi Division 5 watafyatua Kina Werema, Mulugo wakutosha.
 
Kaka Nyani Ngabu, simchukii wala simuonei Mwanasheria Mkuu wa Serikali Jaji Werema. Ni kweli alifanya mtihani wa uwakili na alifeli. Ni ukweli. Ushahidi nitauweka hivi karibuni. Ngoja nipekue mafaili husika. Vilevile, kwa taarifa tu miaka hiyo waliposoma digrii ya Sheria akina Werema pale Mlimani ilikuwa miaka mitatu na sio minne. Miaka minne ilianza kama sikosei kwa waliodahiliwa kusoma digrii ya sheria mwaka 2000.
 
Mkuu Ben

Huyu mtu mimi nakumbuka kesi mbili (sikumbuki wahusika) alizotoa hukumu ya kifo zilitenguliwa baada ya rufaa. Alipaswa kuwa DRC anawafukuza M23 sio AG an bungeni.

Na alishawahi kusema anapenda vita zaidi...Refer mjadala kuhusu baraza la usalama wa Taifa katika mjadala ulioletwa na wizara ya Utawala Bora
 
Alishawahi kusema bungeni na nanukuu " kazi ya kichwa si kufugia nywele tu" sasa leo ndio nimemwelewa bw. Fredrick Werema.
 
Angalia LLM yake ya America. siyo makosa yake ni makosa ya elimu yake. Uk asingeweza kusoma huyo. kwa kichwa chake kisingehimili masomo kule. America ni saizi yeka.

Inategemea na chuo! USA kuna vyuo wanatoa elimu bora mno lkn AG wetu elimu yake bado ni dhaifu na hakustahili kuwa AG

Technically Werema ana LLB ya UDSM tu maana hiyo LLM ya hicho chuo cha USA ni elimu ya hovyo hovyo sana!
 
Ndio hivyo tena vyeo vya kuteuliwa hata paka anaweza teuliwa, kawaida sana hapa TZ shamba la bibi
 
Umeleta hii CV ya nini?

Nahisi ametuletea tuangalie kile kinachotokea bungeni in relation to CV yake yaani yale anayoongea bungeni yapo directly proportional na CV yake au yapo inversely proportional na CV yake, Return Of Undertaker embu njoo ujibu hoja ya Maundumula maana mie nimeona hivyo au ni tofauti, tupe ufafanuzi tafadhali
 
Last edited by a moderator:
Ndio hivyo tena vyeo vya kuteuliwa hata paka anaweza teuliwa, kawaida sana hapa TZ shamba la bibi
Ni kweli mkuu ila miaka hii anaachiwa mtu mmoja kutengeneza timu yake wakati those days system ndio ilikuwa inaangalia nani anafaa though kuna maeneo mengine mkulu mwenyewe anahusika
 
Last edited by a moderator:
Na alishawahi kusema anapenda vita zaidi...Refer mjadala kuhusu baraza la usalama wa Taifa katika mjadala ulioletwa na wizara ya Utawala Bora

Huyu ni mula vita ni vita
 
ni jaji na pia ni mwanasheria mkuu wa serikali ila jana matumizi ya neno "shall" na "may" kwa mujibu wa sheria za nchi yamempga chini.
 
Back
Top Bottom