Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,884
- 6,885
Hakuna haja ya kutokwa na povu hii thread ni mpya JF kuna members wapya wanaitaji mijadala kama wewe ulijadili siku nyingi kaa pembeni waachie members wapya hii ndio maana ya forums...halafu nikukumbushe acha kulia lia JF sio mali ya Chadema.
Riz@ nikusaidie kidogo kuelewa:
Chuo cha St. Urban University, Rome, ambacho huchukua wahitimu kutoka vyuo mbalimbali duniani, wanafunzi kutoka vyuo shiriki hasa Seminary huwa kama ifuatavyo:
Vyuo vingi nchini Tanzania kama Kipalapala Major Serinary, Peramiho Major Seminary, Segerea Major Seminary na sasa Morogoro Religious Major Seminary baadhi ya wanafunzi huchukua kozi za moja kwa moja na kufanyia mitihani ya St. Urban University, Rome na kupata shahada za awali, na waendapo huku ni kudeal na PHD tu.
St. Urban University, Rome mfumo wake wa elimu si kama Chuo cha kibongo mlimani au Dodoma Univ. Kule Rome mtu akianza kupiga mbizi kama hakatishi ataendelea hadi kieleweke kupata PHD, si kama bongo, wale jamaa wana mfumo wao.
Kwa taarifa tu kujiunga na chuo kile kuna qualifying test, hata kama una PHD za Marekani au wapi lazima upige hiyo qualifying test yao kupima uwezo wako. Pale haingii mtu kwa kuangalia sura au anatoka wapi ila bongo lifanye kazi. Ujue ni chuo pekee duniani kutoka mataifa yote na hivyo anayetia mguu pale ujue amechujwa vya kutosha.