Baada ya kuangalia kipindi cha Straight Talk Africa, ambapo Mh. Tundu Lissu na Balozi Wilson Masilingi walihojiwa, nilishangazwa na jinsi Balozi wetu huko Marekani alivyopwaya na kupata tabu kujielezea kwa Kimalkia na pia kushindwa kudhibiti jazba zake.
Nilidhani pengine ni Kimalkia tu kinamsumbua huyu ndugu yetu, lakini nikagundua kuwa tatizo sio lugha kwani kwenye mahojiano mengine yaliyofanyika kwa kiswahili katika VOA Swahili, hali ni ile ile.
Mbaya zaidi kwenye hii interview ya pili, hata kufuata taratibu ndogo tu za midahalo ya kistaarabu hakuweza.
Haya yote yamenipa hamu ya kufahamu safari ya kiongozi wetu huyu na ni jinsi gani ameweza kufika katika nafasi kubwa kama hiyo pamoja na mapungufu hayo.
Hivyo basi, nawaomba wenye ufahamu juu ya elimu na uzoefu wa Balozi Wilson Masilingi atuhabarishe.