Current four star Generals in Tanzania

Thanks

Nikumbushe hao 2 waliopanda vyeo ni kina nani?
 
Bado hajapandisha, amewapa ubalozi ili kuwatoa jeshini to create room ya kupandisha wawili ambapo mmoja lazima atakuwa ni wa dini fulani ili angalau the next CDF awe wa dini nyingine.
P
Haya mambo ya dini hadi jeshini?
mbona Lt General aka Chief of staff ni muislam ila kapewa ubalozi...km angetaka si angempromote huyo huyo kutoka Lt General to Full General na kua CDF huyu mwingine akisfaafu? Unless useme kua this time around ni zamu ya wazanzibari kidogo it make sense...
 
It depends, hata ungekuwa wewe, ukasoma bandiko kama hili
Unaweza kuingia hasira na kujiuliza ni hawawezi au kuna systematic errors za kutokea by a coincidence tuu hakuna Mzanzibari aliyewahi kuwa mkuu wa Jeshi lolote si la mgambo, polisi, uhamiaji, zimamoto, Idara ya usalama wala JWTZ yenyewe!. Tena enda ikawa Mwanamke. The highest rank iliyowahi kushikwa na mwanamke jeshini kwetu ni Maj. Gen. Zawadi Madawili, its about time tutende haki kwa wote.
P
 
are you saying mwanamke apewe nafasi ya juu ili tutimize usawa wa kijinsia?
Hizo nafasi ni nyeti sana.. hachaguliw mtu kwa jinsia. anachaguliwa kwa experience na uchapa kazi
 
Niongezee swali hivi jenerali na meja jenerali yupi mkubwa?
Jenerali ndiyo mkubwa ni four star General, anafuatiwa na Lieutnant General ambaye ni three star General halafu Major General ambaye ni two star General then Brigadier General ambaye ni one star General...
 
Mkuu,

Huwezi kuwa na majenerali wawili au zaidi kwa wakati mmoja wakiwa bado wako kwenye utendaji hai wa jeshi kutasababisha ukosefu wa nidhamu maana jenerali kwa mjibu wa ngazi ya mamlaka ya jeshi likiwa haliko vitani ndio cheo kikuu cha kutoa amri utekelezaji wa suala lolote. Endapo pakiwa na majenerali zaidi ya mmoja kwa wakati mmoja na mmoja akaona mwenzie anafanya kwa maoni yake ndivyo sivyo kisha akatoa amri kwa vikosi kwenda kinyume ni rahisi kusababisha uasi.

Kitu cha kwanza jeshi ni

1. NIDHAMU na UTII kwa kuzingatia mtiririko wa mamlaka na wajibu

2. KUFANYA KAZI KWA JUHUDI NA MAARIFA
3. KUTHAMINI na KUITETEA TANZANIA kwa GHARAMA ZOZOTE
4. UZALENDO na UPENDO kwa WANANCHI ambao ndio CHANZO cha JESHI hilo
 
are you saying mwanamke apewe nafasi ya juu ili tutimize usawa wa kijinsia?
Hizo nafasi ni nyeti sana.. hachaguliw mtu kwa jinsia. anachaguliwa kwa experience na uchapa kazi
No sisemi mwanamke apewe nafasi ya juu, bali tuko sawa, kwanini wanawake wasitendewe haki sawa hadi jeshini?.
P
 
Sasa nimejua kwa nini tulipokua JKT serengeti wakati mwingine walikua wanawaita Madawili
 
mkuu, hatutaki 'woke' culture hapa kwetu, mambo ya kumpa mtu cheo kisa mwanamke hatuyataki kabisaaaaaa........
 

Mkuu, nadhani unalalamika prematurely. So far ni watu wangapi wamewahi kuwa wakuu wa kila jeshi katika taifa letu? Kwa kufuata proportional representation, Wazanzibari au wanawake can actually go for a few centuries before one them becomes a CDF, kwa sababu ya uchache wao. That’s just the nature of the beast. Hakuna sababu ya kufanya siasa za viti maalumu jeshini.
 
Hizo ni hisia zako tu!

Mbona nchi zingine zina majenerali zaidi ya mmoja na hakuna ukosefu wa nidhamu unaofanya hayo majeshi yasiweze kutekeleza majukumu yake?

Hujaandika kwa kujua! Umeandika kwa kuhisi lakini ukajifanya unaandika kama unajua ilhali haujui!!!
 

The most plausible reason ni kwamba jeshi letu ni dogo. Ukamanda wa kijeshi unakwenda kwa idadi ya askari.

Jeshi la Marekani lina askari zaidi ya million moja, chini ya 11 combatant commands. Pamoja na hayo, lina 45 active-duty 4-star generals tu!
 
The most plausible reason ni kwamba jeshi letu ni dogo. Ukamanda wa kijeshi unakwenda kwa idadi ya askari.

Jeshi la Marekani lina askari zaidi ya million moja, chini ya 11 combatant commands. Pamoja na hayo, lina 45 active-duty 4-star generals tu!
👍
 
Muundo wa jeshi la Tanzania hauna ulazima wa kuwa na majenerali zaidi ya mmoja. Ni jeshi lenye watumishi wachache na kamandi chache ukilinganisha na mataifa mengine yenye kamandi nyingi hasa idara za kisayansi zilizopo jeshini.

Kwa hiyo JWTZ linaundwa na idadi maalumu( limited in number) ya maafisa wa juu, maafisa wa Kati na makamanda wa vikosi na wapiganaji.
 
No sisemi mwanamke apewe nafasi ya juu, bali tuko sawa, kwanini wanawake wasitendewe haki sawa hadi jeshini?.
P
hatuko sawa. ndio maana hata jeshin wao wana separate pass marks ( na ziko low ukilinganisha na za mwanaume ) na wanaume.
kuna vikosi wao hawapo kutokana na maumbile yao... uwezo wao.

unataka haki sawa. not jeshini.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…