Current four star Generals in Tanzania

Hizi ndizo insignias za British system nilizoongelea kwenye post #284. Za kuanzia brigadier general hadi general hazitumiki tena; zimekuwa replaced na za American system zinazoonekana kwenye post #279.
Hizo za Kimarekani zimeanza kutumika lini?
 
Huwezi kuwa na mabrigedia elfu moja wakati brigedi unazozijua 10

Vyeo vina limit na vigezo husika , ila kufika ukanali sio ishu sababu hata ukanali pia ni uanafunzi
Kwanini maafisa wengi wanazungushwa sana na kustaafu kwenye kanali. Hawafiki kule juu.
 
..huenda hali hiyo inatokana na mtizamo wa amiri jeshi mkuu wa wakati husika.

..nadhani kila amiri jeshi mkuu hupenda kuteua cdf na cos, kuliko kurithi walioteuliwa na watangulizi wao.

Cc PTER, Emiir
haswaa, nadhan ndio mana akiingia tu madarakan huwa anamwondoa CoS aliyepo ili alete CDF wake (ila at that time anampa nafasi ya CoS ili asafishe macho kidogo,)........
 
kwa uelewa mdogo kwa haraka haraka sababu ni ukubwa wa Jeshi, maana Jeshini kila Cheo kina idadi ya Askari wanaotakiwa kuwa chini yako, Jeshi letu ukubwa haujafikia kuwa na uhitaji wa kuwa na more than one Four Star Generals, ndo mana tunae mmoja tu ambae ndo huwa CDF huyo huyo. angalia historia yetu hata wkt JWTZ inaanza miaka ile CDF hakua Four Star General kutokana na ukubwa wa Jeshi kwa kipindi kile. lakini angalia hata nafkiri Seychells wao CDF wao wala sio General kama sijasahau, hiyo ni kutokana na ukubwa wa Jeshi lao
 
hujui kuwa IGP atampigia saluti General Mabeyo?
Na ipo wazi mmoja ni General mwingine ni Inspector General na kikawaida cheyo kinachotanguliwa na kitu mfano Lt. Gen, Maj. Gen, Insp. Gen n.k ni kidogo kwa kile chenyewe ambacho ni Gen hivyo Sirro lazima aanze kutoa heshima.
 

Hata wakati wa hayati John Magufuli alimpandisha cheo Salum Kijuu ambaye alikwisha kuwa amestaafu jeshini kutoka Brigedia Jenerali mpaka kuwa Meja Jenerali baada ya utendaji wake mzuri katika nafasi ya Mkuu wa Mkoa wa Kagera.

Kingine, Meja Jenerali Mstaafu Salum Kijuu aliyekuwa RC Kagera na Brigedia Jenerali Mstaafu Maganga aliyekuwa RC Kigoma walikuwa wakivaa magwanda ya kijeshi hata mara baada ya kuwa wamestaafu utumishi wao jeshini ila walivaa hasa pale Rais alipokuwa anafanya ziara katika mikoa yao.
 
Na ipo wazi mmoja ni General mwingine ni Inspector General na kikawaida cheyo kinachotanguliwa na kitu mfano Lt. Gen, Maj. Gen, Insp. Gen n.k ni kidogo kwa kile chenyewe ambacho ni Gen hivyo Sirro lazima aanze kutoa heshS

Na ipo wazi mmoja ni General mwingine ni Inspector General na kikawaida cheyo kinachotanguliwa na kitu mfano Lt. Gen, Maj. Gen, Insp. Gen n.k ni kidogo kwa kile chenyewe ambacho ni Gen hivyo Sirro lazima aanze kutoa heshima.
licha ya hivyo vyeo vya kipolisi ukifanya conversion kuja vyeo vya military huwa ni vidogo
 
Majenerali kwao kustaafu ni (kupumzika) tu, lakini wakati wowote wakihitajika wanaweza kurudi. Na ndio maana wakawa wanaonekana ndani ya mavazi kama kawaida. Na pia huhudumiwa na Serikali hadi kufa kwao.
 
Jeshini hakuna cheo kinaitwa General Mstaafu, Makosa kuwa-address hivyo
 
Uchangiaji wako umesadifu username yako[emoji1474]
 
Unakosea, Jeshini hakuna cheo cha sijui Meja Jenerali Mstaafu n.k, waite tu Meja Jenerali Salum Kijuu na Brigedia Jenerali Maganga, ila ukitaka ijulikane kuwa wamestaafu ongezea neno Mstaafu baada ya majina yao na sio baada ya cheo, hivyo sema Meja Jenerali Salum Kijuu (Mstaafu) na Brigedia Jenerali Maganga (Mstaafu).
 

Hapa kidogo umeyumba mkuu, iko hivi
Kinaanza kutajwa cheo linafuatia neno mstaafu ndipo linatajwa jina lake. Na kama ni mfumo wa maandishi kinaanza kutajwa cheo linafuata neno mstaafu kwenye mabano ndipo linatajwa jina lake.
 
Hapa kidogo umeyumba mkuu, iko hivi
Kinaanza kutajwa cheo linafuatia neno mstaafu ndipo linatajwa jina lake. Na kama ni mfumo wa maandishi kinaanza kutajwa cheo linafuata neno mstaafu kwenye mabano ndipo linatajwa jina lake.
Hapana wewe ndie umekosea, nlichoandika mimi ndio sahihi, cheo cha kijeshi hakistaafu wala hakifi ndo maana kuna watu walipandishwa vyeo na wkt walishastaafu utumishi jeshini, sasa ukiweka neno mstaafu baada ya cheo utashindwa kukipandisha cheo cha juu yake baadae, hivyo mie niko sahihi, wewe ndie iko wrong na sio kosa lako ni makosa ambayo yamezoeleka hadi watu mnahisi ndio usahihi kumbe sio
 
Hapa chief unapotoka, tena unazidi kupotoka. Kuna utaratibu wake kuandikwa hivyo na sio kama unadhani inakuja tu.
Kiutaratibu wa kuandikwa kwa Jina na cheo cha Muhusika uko hivi.
Akiwa kwenye utumishi:
1. Madaraka yake
2. Cheo chake,
3. Jina lake,
*Kama ana elimu ya juu ya kiraia inatangulia kabla ya jina lake

Nje ya utumishi
1. Aliyekuwa (madaraka/hadhi yake)
2. Cheo chake, (Mstaafu)
3. Jina lake
*Kama ana elimu ya juu ya kiraia inatangulia kabla ya jina lake

Na kwa rais
1. Hadhi yake
2. Mamlaka/madaraka yake
3. Elimu ya juu
4. Jina lake

Mfano:
1. Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na,
2. Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi,
3. Dkt,
4. John Pombe J. Magufuli

Kuunganisha
1.Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na 2. Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi 3. Dkt 4. John Pombe J.Magufuli.

Kamili:
Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Dkt, John Pombe J.Magufuli.

Mfano mwingine huu hapa kwenye picha
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…