CUF waishambulia CHADEMA

CUF waishambulia CHADEMA

Nickname, that's called politics, mara nyingine lazima usimamie unachokiamini hata kama utachukiwa na wengi kama matokeo ya imani yako. Lakini ni wangapi kweli wanaoichukia CHADEMA? Mimi na watu wengine wengi sana tunaipenda CHADEMA! Mimba ya CUF itatoa "Si riziki". Subiri uone!
 
kama yepi ?

kukubali vyama viwili kuunda umoja na kuviona vyengine kwa kua na uwakilishi mdogo si wapinzani ?


chadema mtulie muache makeke


ngoma yataka matao
Kama matao yenyewe ni CUF basi hakuna haja ya kucheza hiyo ngoma.
 
Huyu hamad rashid hajui maana ya kumachua kwani amejengwa kwa misingi ya mawazo mgando. Leo hii watu wapo serious na mageuzi yeye analeta siasa za znz (siasa legevu) za mguu sawa mguu legeza. Kwanza ngoma ya upinzani jamani mnavyoiona kina tundu, wa kuongozwa na mtu mzembe mzembe kama huyu hamad? naomba mtutake radhi sisi tuliochagua chadema.
Pili- hamad anataka chadema wasuluhishwe na mbatia(kibaraka) wa cc.hem mtu ambaye amefungua kesi dhidi ya matokeo ya mdee,haamini wadada tena wadogo wamemtoa jasho la maana mpaka wazee wamemuonea soni na kumpa moyo.
Sasa mtu anayekufungulia kesi utaungana naye vipi? huu ndo unafoki ccm waliouzoea na cuf wanataka kuambukiza vyama vyote
 
Inasikitisha tunapoongelea mambo ya msingi watu wanakimbilia udini udini utafikiri kama ni waumini wa kweli!
Tukumbuke pia tulishaambiwa sio wote wanaokuja kwa gia ya upinzani ni wapinzani wa kweli,nafikiri mmeliona hilo wenyewe mara kibao.
Pia hii ndoa ya CUF kuolewa na CCM inabadilisha mwelekeo wa upinzani kwa upande wa CUF,hapo iko wazi na inatakiwa kama wapinzani wanashirikiana na CUF wawe makini na mienendo yao kwani wakicheza vibaya chama chao kinaweza kufa au kikatumiwa na ccm kuua upinzani.Kingine inaonyesha wazi CUF hawakupendezwa wao kupigwa kikumbo na chadema,sasa tukiangalia hayo na mengine mengi utaona wazi kwamba bora Chadema waendelee kivyao vyao,itakuwa uwendawazimu eti kumshirikisha Mrema kwenye kambi ukategemea mambo yaende sawa na ndio maana utasikia Chadema hawakutaka vyama vingine zaid ya CUF inaeleweka walimaanisha nini haikuwa lazima kutaja majina ya mbunge gani hawamuhitaji.
 
...CCM na CUF wameklubaliana Unyumba pasipo ndoa na CUF kama mwanamke malaya ametaka unyumba na Chadema lakini Chadema hawataki kwa sababu CUF kawekwa kinyumba na CCM ili apate kujengewa nyumba yake huko Unguja. Lakini kuwepo sababu hizo Chadema hawataki tena mahusiano na CUF pamoja na kwamba Chadema wanajua sababu ya CUF kukaa na CCM hivyo kuhofia matokeo ya relation baina yao.

Sasa mimi nasema hivi huu ni wivu wa kijinga ikiwa Chadema anafahamu fika kwamba CUF anafanya umalaya wa kisiasa ili afanikishe sera zake ndani ya utawala wa CCM. Na maadam mbaya wa Chadema ni CCM strategically Chadema anatakiwa kumuumiza CCM kwa kila nafasi anayopata na moja wapo ni hii ya kushirikiana na CUF na vimada wake wote ktk baadhi ya maswala. Nikirudi ktk mfano wangu pale juu, mtu yeyote mwenye mahusiano na ametumia fedha na muda wake kumjenga, akisikia kuna mhuni anapiga kwa pembeni pasipo gharama itamuuma zaidi na pengine kuwa na wasiwasi zaidi na mahusiano baina yao.

Kwa maana hiyo Chadema kama chama wanatakiwa kuwa na mbinu za kuwaangusha CCM na mojawapo ni kuendelea ushirikiano na CUF pale inapohitajika kukidhi haja za Chadema kama ilivyokuwa toka mwanzo. CCM wanajulikana ni mafisadi tena ktk hili ndio kabisa wamemchukua mke wa mtu na kumweka kinyumba..Chadema wasifanye hasira kama kweli mufaka huo ndio unawauma zaidi basi wafikishe mashataka yao mahakamani ili kupata sheria. Lakini tunapoendelea kudai kwamba CUF nbdio walikuwa hawataki ushirikiano hali Chadema ndio tumewapa nafasi hiyo kwa masharti nadhani ni bora tuwe wakweli. Tukubali kwamba Chadema imekataa ushirikiano na CUF kwa sababu CUF imetaka vyama vingine vishirikishwe lakini hili halikubaliki na Chadema na kwa sababu zifuatazo.

Again, nashindwa kuelewa kwa nini tuwakaribishe CUF ktk ushirikiano na tuwaache wengine hali CUF amekaa vibaya zaidi ya NCCR -Mageuzi au TLP ukichukulia muafaka uliopo baina ya CUF na CCM. Wakuu zangu sintapenda kuendelea na ubishi huu lakini utetezi wa wana Chadema hauna mantiki hata kidogo ikiwa Chadema waliwafuata CUF kisha leo tunasema hatuwataki CUF kwa sababu ya ushirika wake na CCM...Je, Chadema hawakuona ubaya wa mahusiano hayo toka mwanzo kabla hawajawafuata CUF?

Nazidi kuwaumiza vichwa!

Kwa kutumia mfano wako wa Mwanamke Malaya CUF, Huoni kwamba CHADEMA ikiwa na uhusiano na huyu mwanamke malaya (CUF), Unajiweka katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa maradhi ya Ukimwi(UFISADI) alionao Mume wa CUF ambae ni CCM? Sote tunajua CCM inaugua huu ugonjwa wa UFISADI ambao hauna kinga wata Tiba, Sasa iweje ushauri Chadema kuwa na uhusiano na Mwanamke Malaya(CUF) ambae ana uhusiano na Mgonjwa CCM?

Huoni kwamba hii itakua ni tiketi ya kujitakia ya kuambukizwa haka ka-ugonjwa?

Hii ni akili kweli?:nono:
 
Hakika nawaambia.
CUF hawajui lolote juu ya ndoa yao na CCM bali CCM wanajua fika wanachokitaka ktk ndoa hii.
Hamad naye kama zuzu anachekelea tu na ku'dance tune ya CCM.
Hamad akajifunze kutoka Kenya.
Akina Odinga wameunda serikali ya kitaifa lakini dhamila ya mapinduzi ipo pale pale hawadanganyiki na vijivyeo.
Niliwategemea sana CUF kule Zanzibar labda wangetuonyesha mfano kwa kuleta mapinduzi halisi kumbe zilikuwa njaa tu zile.
Nisije nikatukana, ngoja niishie hapa.
 
Hivi tatizo la CUF ni nini?
Hivi hawa CHADEMA SI NDIYO WALISEMA WAKIPEWA RIDHAA NA WANANCHI WATAUNDA
SERIKALI YA UMOJA WA KITAIFA?
Sawa ridhaa ya kambi ya upinzani wameipata kwanini wameshindwa kuunda kambi ya upinzani yenye sura ya kitaifa angalau kuonyesha kwamba walichokua wakikihubiri kwenye majukwaa ndiyo hicho wangekifanya?Kwani huu Muafaka wa CUF NA CCM UMEANZA LEO?Kwahiyo sioni sababu ya kuwaita CUF ni CCM B kwavile wametekeleza kile walichokubaliana na CCM ktk vikao walivyofanya na wala haikuwa siri.Afadhali huyo Hamadi ametoka hadharani na kueleza tatizo ambalo lina ukweli ndani yake kwasababu hakuna kiongozi mwenye dhamana kutoka chadema amelikanusha.kwanini chadema badala ya kujenga umoja wao wanaona ni bora wao peke yao kwa vile wanamajority ni haki yao lkn inadhoofisha kambi ya upinzani kwani sasa badala ya wao kupambana na adui yao CCM wameongeza maadui ndani ya bunge,Unajua ni rahisi tu kusema vyama vingine ni maamluki kwa kiujumla au kusema vyama vingine ni wabinafsi lkn wewe usiwe mbinafsi umefanya nini kuonyesha kwa vitendo kwamba si mbinafsi?Kama mambo yataendelea hivi kuna hatari huko mbeleni, watanzania wanafuatilia kwa makini kile walichowapa kama mwanzo wa uaminifu wao kwenu CHADEMA.Hivi kama haya anayoyasema Hamadi kuviunganisha vyama vingine ktk ushirikiano kuna ubaya gani?Au ndiyo lile bifu la ni wadogo ni sawa na sisimizi bado linaendelea.wapinzani futeni bifu zenu na onyesheni kujali umoja kwani umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.
Nyie mlishaungana nao sisi hatuwataki hao.
 
Kwa kutumia mfano wako wa Mwanamke Malaya CUF, Huoni kwamba CHADEMA ikiwa na uhusiano na huyu mwanamke malaya (CUF), Unajiweka katika mazingira hatarishi ya kuambukizwa maradhi ya Ukimwi(UFISADI) alionao Mume wa CUF ambae ni CCM? Sote tunajua CCM inaugua huu ugonjwa wa UFISADI ambao hauna kinga wata Tiba, Sasa iweje ushauri Chadema kuwa na uhusiano na Mwanamke Malaya(CUF) ambae ana uhusiano na Mgonjwa CCM?

Huoni kwamba hii itakua ni tiketi ya kujitakia ya kuambukizwa haka ka-ugonjwa?

Hii ni akili kweli?:nono:
Haya nakupa jibu kwa lugha hiyo hiyo:-

Sasa ulimtongoza wa nini kama unaogopa Ukimwi hali ukijua fika anatembea na CCM. Je, nia yako ilikuwa kulala naye tena?..
Kisha nachokisema mimi, sio lazima utembee naye kimwili ni urafiki na mahusiano ya mazungumzo pengine utamsaidia yeye na maradhi yake na pia kujua baadhi ya matatizo yake ikiwa ni pamoja na kukutonya wote walioambukizwa ukimwi na huyo CCM usije wavaa wewe kimapenzi..
 
Juzi wakati Mhe. Mohamed Habi Mnyaa alipokuwa anatangaza nia yake ya kujiondoa katika kinyanganyiro cha unaibu Spika alitamka wazi wazi kwamba anajiondoa kufuatia maridhiano kati ya CUF na CCM (Zanzibar) na anaweka jina lake kwenye kinyanganyiro cha Ubunge wa SADC. Kama ilivyotegemewa wabunge wote wa CCM walimpigia Mnyaa kura na amepita. Hivi sasa CUF na CCM lao ni moja. CUF wana bifu na CHADEMA kwa vile chama chao "is on the decaying trend" huku Tanzania Bara kiasi cha kupitwa na NCCR-Mageuzi katika viti vya ubunge. Prof. Lipumba amekosa kupta hata kura Milioni moja katika uchaguzi hata katika maeneo yanayowaunga mkono CUF! The writting is on the wall. CUF kitabaki chama cha visiwani.
Yaani Lipumba alishindwa hata kwao Tabora? Sasa atatwambia nini?:rip:cuf
 
Jazba zote hizi kuhusiana na hii mada hazina tija kwa Chadema.
Matokeao ya viongozi wa chama kuwa hostile kwa vyama vingine vyote (CCM, CUF, NCCR, TLP) si mazuri.
Very soon tutaanza kujiuliza tulidondokea wapi?...
Kwa mwenendo huu.... I'm afraid our dear Chadema is heading into a ditch..... take my word.

View attachment 17250View attachment 17251
Dua la kuku hilo wewe mwana CCM
 
Kwani mwanamke (CUF) anaruhusiwa kuwa kwenye ndoa mbili kwa wakati mmoja?
 
ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.

Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.

Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.

Amewataka viongozi wa Chadema wawe ‘matured’ na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.

Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).

Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.

Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.

Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.

Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.

Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010

who the hell is cuf?? huyo rashid ni mnafiki sana katika chaguzi zote huko nyuma walikuwa hawamtambui salmin amour (1995) na karume (2000 & 2005) leo wameolewa na sisiemu ndo wanawageuka chadema, wanafiki wakubwa, warusi kwa zenji hatuwahitaji huku bara kwanza ndo wamejaa udini mtupu!
 
Wakuu zangu hili sio swala la kupuuza hata kidogo. Chadema acheni uchu wa madaraka kuunda kambi ya Upinzani na haitawasaidia chochote zaidi ya kujenga fitna zaidi.
Kweli kabisa Chadema kulingana na katiba inayo haki ya kufanya kila kitu watakavyo isipokuwa mjue tu kinachozungumziwa zaidi na katiba ni jinsi ya kumpata kiongozi wa kambi hiyo ya Upinzani, kuliko uundwaji wa kambi yenyewe.

Vipengele vyote vinazungumzia nani atakuwa kiongozi wa kambi hiyo lakini haikatazi chama kuunda umoja na vyama vingine kwani maana ya kuunda kambi hiyo ni kutoa fursa kwa vyama vingine vipate nafasi ya kuzungumzia hoja walizokuwa nazo dhidi ya chama tawala. Kinyume cha vyama hivyo havitakuwa na nafasi hiyo isipokuwa kuuliza maswali ya nyongeza tu.

Leo hii wakuu zangu nimeamka vibaya na hakika sipendi kuzungumza mengi isipokuwa nasema Mkuu wangu Mbowe, ile tabia ya kuwatumia watu kisha ukawaacha mataani iache.. sii nzuri hata kidogo na wala sii uungwana kwa sababu siasa sio biashara ni maelewano ambayo yanahitaji uaminifu na makubaliano ambayo hayawezi vunjika mara tu unapofanikiwa na kutaka kuvuta asilimia yote 100 wewe.

Hizi tabia za kusema CUF wana wivu ni tabia za kishenzi tu, ni tabia zisizokuwa na shukranii kutofikiria ulitoka wapi na leo umefika wapi ukasahau kwamba pasipo ushirikiano wa mwenzako pengine usingefika hapo ulipo. Alichozungumza Rashid ndiyo hali halisi na sioni sababu kwa nini watu mlitaka afiche hali ndicho kilichotokea hadi kutokuwepo ushirikiano baina ya vyama kuunda kambi ya Upinzani. Sasa kama Chadema mnafikria mnaweza kwenda solo baada ya mafanikio mloyapata uchaguzi huu, sawa endeleeni kufurahia matunda hayo lakini amini maneno yangu malipo yake yatakuja jitokeza muda sii mrefu... Itakula kwenu.
Mkandara huwa ninakuelewa na kukubaliana nawe kwa mambo mengi. Lakini samahani kwa hili sintakubaliana nalo na nasikitika kwamba unambebesha lawama Mbowe bila sababu kwa sababu na mimi ningekuwa mbowe ningechukua msimamo huo huo. Nina mashaka kwamba katika mkakati huu una agenda mbaya na Chadema na si bure.
Nimesema na narudia si vema kwa namna yoyote ile Chadema kuungana na CUF tena kwa hizi mbwembwe za CUF kila mmoja apambane kivyake. Nadhani hata ungeita msimamo huo wa Chadema kuwa ni wa Kishenzi bado nasisitiza si sawa chadema kuungana na CUF tena. Nadhani CUF ndio washenzi lakini Chadema ni wastaarabu.
 
CHADEMA wembe huo huo hakuna kuungana na mamluki CUF, tena sitaki kusikia habari ya mazungumzo ha hao waio na mbele wala nyuma achaneni nao kabisa. Ndumila kuwili hao watendeni mbali kabisa. CHADEMA inaweza bila msaada wa hao wala UROJO.:nono:
 
Kikwete na sera ya udini
Hivi leo nimesikia kikwete anasema kuna udini mkubwa sana hapa Tanzania na akaongea kwa msisitizo kabisa,guys is it true?
Ianzishie thread kwani nadhani this is not a right place to discuss these issues.

Hapa tuko kwenye issue za Rashid na muunganiko wa cuf na chadema
 
Jamani kumbe CHADEMA wana maadui wengi ,CUF wanakeraa sana ,toka waunde serikali (waolewe) na CCM wana nyodo sana.Sijui mimba inawasumbua?? Khaa!!!!!!!!:


I like this
 
Mkandara huwa ninakuelewa na kukubaliana nawe kwa mambo mengi. Lakini samahani kwa hili sintakubaliana nalo na nasikitika kwamba unambebesha lawama Mbowe bila sababu kwa sababu na mimi ningekuwa mbowe ningechukua msimamo huo huo. Nina mashaka kwamba katika mkakati huu una agenda mbaya na Chadema na si bure.
Nimesema na narudia si vema kwa namna yoyote ile Chadema kuungana na CUF tena kwa hizi mbwembwe za CUF kila mmoja apambane kivyake. Nadhani hata ungeita msimamo huo wa Chadema kuwa ni wa Kishenzi bado nasisitiza si sawa chadema kuungana na CUF tena. Nadhani CUF ndio washenzi lakini Chadema ni wastaarabu.
Mkuu wangu nadhani bado kabisa hujanipata na wala hutaweza kunielewa ikiwa umeshindwa kunielewa hapo juu. Katika mfano wetu hapo juu nachosema mimi kwamba yale mahusiano baina ya Chadema na CUF yasipotee tu kwa sababu CUF ni mwanamke anayetafuta chake.

Chadema hawana sababu wala haja ya kuungana au kurudia mahusiano yake na CUF kama ilivyokuwa zamani, sipendi wala sipendekezi lakini kama wataweza kumweka hasira na wivu CCM Kisiasa basi ni pale Chadema watakapo onyesha wapo bado karibu na vyama vingine vya Upinzani na hasa CUF hata kama..

Kutokana na wivu wa mtandao hasa tunavyomjua jamaa yetu asiyependa kuona mazoea ya namna hii watalazimika kujiuliza mengi sana.

Kumbuka ikiwa Zitto leo mnamwekea mashaka sana kwa sababu yupo karibu na JK au kaunga mkono baadhi ya maswala ya JK,iweje kuwa vigumu kwenu pia kutumia mbinu hiyo hiyo ya CCM kuwaweka ktk mashaka?..Sikupenda kuandika mengi kuhusiana na hili isipokuwa kama mimi ningekuwa Mbowe na tumeweza kufika hapa tulipo na CUF, bado ningeelea kuwatumia ktk baadhi ya maswala tunayokubaliana nao na ningehakikisha zaidi nafahamu kila hatua ya mapatano yao na CCM zaidi ya wao kuyajua ya Chadema.

Labda nikutonye tu kwamba tazama baraza la mawaziri litakalo tangazwa, utashangazwa na mengi..
 
hamad rashid mnafiki mkubwa, hana lolote, mbona Znz yeye alikuwa wa Kwanza kutomtambua Karume kwa kutokushinda Urais, hadi Serikali ya umoja wa kitaifa ilipoundwa na kuua upinzani Znz ndio wakamtambua na CHADEMA wanafanya hivyo hivyo na hatutaki serikali ya kuunganisha CHADEMA na CCM, tulishinda kihalali, Hamad alitaka achaguliwe awe tena kiongozi wa upinzani bungeni kakosa, CHADEMA waliona huyu si mpinzani ni mkinzani, safiiiii, he is a scraper
 
hamad rashid mnafiki mkubwa, hana lolote, mbona Znz yeye alikuwa wa Kwanza kutomtambua Karume kwa kutokushinda Urais, hadi Serikali ya umoja wa kitaifa ilipoundwa na kuua upinzani Znz ndio wakamtambua na CHADEMA wanafanya hivyo hivyo na hatutaki serikali ya kuunganisha CHADEMA na CCM, tulishinda kihalali, Hamad alitaka achaguliwe awe tena kiongozi wa upinzani bungeni kakosa, CHADEMA waliona huyu si mpinzani ni mkinzani, safiiiii, he is a scraper
Mkuu wangu uloyasema sii kweli, Chama kilichoshika nafasi ya pili ndicho chenye jukumu la kumchagua kiongozi wao wa Upinzani..walichokitaka CUF ni kushirikishwa vyama vyote vya Upinzani na sioni baya ikiwa ni kushirikishwa tu kuunda kambi..Elewa moja hawa wote wanataka Ulaji katika hayo mabaraza yatakayo undwa...Njaa babu njaa! bado hamjui tu.
 
Back
Top Bottom