Uko sahihi, CUF sio chama cha upinzani tena hivyo hakiwezi kuungana na Chadema, ukiangalia Ndugu Mrema wa TLP kwenye kampeni alikuwa anampigia kampeni JK, hivyo binafsi simwamini hata kidogo kuingia kambi ya upinzani kwani anaweza kuwa chanzo cha migogoro na kuturudisha nyuma zaidi. Ukiangalia pia NCCR Mageuzi pia hawaaminiki ukianzia na kukuru kakara za mwenyekiti wake wakati wa kampeni hata sasa juu ya Chadema na wabunge wake, hivyo ni bora Chadema kusimama kama wao ili kuepuka migororo ambayo ingetokana na wao kuungana na vyama vingine.Asante mkuu. Litakuwa kosa kubwa kwa CHADEMA kushirikiana na CUF ambao wanamakubaliano ya siri na wakubwa zao CCM. CHADEMA wakishirikiana na CUF basi by default CHADEMA itakuwa ni CCM. Dhama za chama kimoja tutarudi huko. Kazi kubwa ya CUF kwenye yale makubaliano yao ni kuuwa upinzani na CHADEMA. Nafurahi viongozi wa juu wameliona hili. CUF imepoteza identity ya upinzani nadhani tamaa ya viongozi wao imewafikisha huko. 2015 CUF itakuwa imefutika kabisa
Mch Masa K
Naafikiri baadae tutawaelewa viongozi wa Chadema nini wanachokifanya sasa hivi.