nickname
JF-Expert Member
- Dec 20, 2009
- 544
- 147
ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.
Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.
Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.
Amewataka viongozi wa Chadema wawe ‘matured' na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).
Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.
Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.
Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.
Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.
Source: Basil Msongo, HabariLeo, Dodoma; Tarehe: 18th November 2010