Madela Wa- Madilu
JF-Expert Member
- Mar 24, 2007
- 3,063
- 744
Jamani kumbe CHADEMA wana maadui wengi ,CUF wanakeraa sana ,toka waunde serikali(waolewe) na CCM wana nyodo sana.Sijui mimba inawasumbua?? Khaa!!!!!!!!:angry:
Mimba tena!
Jamani kumbe CHADEMA wana maadui wengi ,CUF wanakeraa sana ,toka waunde serikali(waolewe) na CCM wana nyodo sana.Sijui mimba inawasumbua?? Khaa!!!!!!!!:angry:
Nakubakiana nawe mkuu, lakini chanzo kikuu ni hicho, you wait and see hali iko hivyo time will tell na wewe utashuhudia hayo. Hatuna haja ya kubishana let us hope for the best.Mkuu tukiangalia hivyo na tukienda down that road utaanza kuona kwamba wote wana makosa. Maana CUF wanaonekana ni Waislamu na Chadema Wakatoliki/Wachaga. Udini upo na ukabila upo sikatai. Hata katika hali ya kawaida mtu ukiwa na nafasi uka kutana na mtu wa kabila lako au dini yako una kuta ni rahisi zaidi kuwasaidia ila haimaanishi wewe ni mkabila au mdini.
Ila mkuu hamna haja ya mimi na wewe kubishana. Unaweza kuwa sahihi kusema udini umechangia nami nasema muafaka nao kwa kiasi kikubwa umechangia. Mbona wakati CUF ndiyo wameunda baraza kivuli bunge lililo pita wali washirikisha Chadema? Wakati huo udini haukuepo? Kwa mantiki hilo swala la kwanza linalo kuja kichwani mwangu ni kwamba it's not a matter of "udini" per se bali inferiority complex inayo izuia CUF kuwa chini ya Chadema kwenye baraza kivuli ndani ya Bunge.
jamani naona kuna watu huenda hawajafahamu au kwa makusudi hawataki kufahamu kilichozungumzwa
mm nimeona vitu viwili
kwanza chadema wao wako tayari kushirikiana na CUF na wala hawaonyeshi kua na wasi wasi na kuunda upinzani na CUF
la Pili chama cha CUF kinaona sio busara kuunda umoja wa upinzani wa Vyama viwili tu, wao wanaona vyama vyote vyenye wabunge vya upinzani vishirikishwe na wanaamini kuwafata CUF tu wawe kwenye kambi hio sio sawa na CUF wanahesabu ni mtego na Chadema kukosa msimamo
la tatu alizungumzia kuhusu gharama ya kutomtambua Rais
na la mwisho ambalo hata na mm ningependa kujua kua Chadema imewakwaza viongozi wakuu wa NCCR na CUF kivipi ?
Mimi naona kwa hili kuwa kama Zanzibar vyama viwili ndio vimeungana serikari ya Kitaifa kwa nini wasihusishe na vyama vingine huko zenji?
Hapa tukubali tukatae kuna element za udini, japo kuna deeper issues than this. Nilitegemea kusikia maneno ya busara yangetoka kwa Hamad Rashid, matokeo yake katoa pumba tupu. Totaly immatured!
Jamani, mi nafikiri CUF sio chama cha Upinzani, na CHADEMA hawana sababu ya kuwashirikisha CUF kuunda kambi ya upinzani maana wataidhoofisha sana.
Sababu:
Ikiwa CUF na CCM wameunda serikali Zanzibar na Katibu wao (CUF) Mkuu ndiye makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na wabunge wake 7 wameshika wizara. Si rahisi kwao kuja Bara (Serikali ya Muungano) na kugeuka kuwa Wapinzani wakiwa chini ya Katibu Mkuu wao ambaye pia ni Serikali.
Hapa panahitaji fikra za dhati na uelewa mkubwa!!!!!!! Naamini CHADEMA ndio wapinzani wa kweli wanaoweza kuleta changamoto kwa Selikali kwa manufaa ya Taifa.
Jamani, mi nafikiri CUF sio chama cha Upinzani, na CHADEMA hawana sababu ya kuwashirikisha CUF kuunda kambi ya upinzani maana wataidhoofisha sana.
Sababu:
Ikiwa CUF na CCM wameunda serikali Zanzibar na Katibu wao (CUF) Mkuu ndiye makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, na wabunge wake 7 wameshika wizara. Si rahisi kwao kuja Bara (Serikali ya Muungano) na kugeuka kuwa Wapinzani wakiwa chini ya Katibu Mkuu wao ambaye pia ni Serikali.
Hapa panahitaji fikra za dhati na uelewa mkubwa!!!!!!! Naamini CHADEMA ndio wapinzani wa kweli wanaoweza kuleta changamoto kwa Selikali kwa manufaa ya Taifa.
jamani naona kuna watu huenda hawajafahamu au kwa makusudi hawataki kufahamu kilichozungumzwa
mm nimeona vitu viwili
kwanza chadema wao wako tayari kushirikiana na CUF na wala hawaonyeshi kua na wasi wasi na kuunda upinzani na CUF
la Pili chama cha CUF kinaona sio busara kuunda umoja wa upinzani wa Vyama viwili tu, wao wanaona vyama vyote vyenye wabunge vya upinzani vishirikishwe na wanaamini kuwafata CUF tu wawe kwenye kambi hio sio sawa na CUF wanahesabu ni mtego na Chadema kukosa msimamo
la tatu alizungumzia kuhusu gharama ya kutomtambua Rais
na la mwisho ambalo hata na mm ningependa kujua kua Chadema imewakwaza viongozi wakuu wa NCCR na CUF kivipi ?
Pamoja na hao wabunge 7 wa CUF wameshika wizara hiyo ni kwa ajili ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar ujuwe Nchi yetu inaendeshwa na Serikali mbili Serikali ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania sasa hao Wabunge 7 wa chama cha CUF waliochaguliwa kwa upande wa Serikali ya Zanzibar tu si kwa ajili ya Serikali ya Muungano. Usichanganye suala la Seriakali ya Mapinduzi Zanzibar na ukatia na masuala ya Serikali ya Mungano wa Tanzania ni vitu viwili tofauti hapo mkuu.
tusiwe blinds kwenye hili... Lazima tuelewe ukweli kabla ya kudhani CUF hawana point
Much as we seek for changes, it has to be very systematic and sophisticated... nadhani kuna haja ya CHADEMA ku-take things slow and cut off drama ili wajipange upya, including kujenga kambi ya upinzani
Nakumbuka niliuliza kuhusu kambi ya upinzani, nikaambiwa kwamba CHADEMA ndio walikua na haki ya kufanya, lakini naamini kama wangeamau kukaribisha wapinzani wote, hilo lingeleta maana zaidi na ile courtesy ingezaa imani ndani ya upinzani
Najifunza hayo masiasa because i am for changes lakini nadhani kuna tatizo kidogo... haiwezekani wewe tu ndio uchukiwe na kila mtu
Having said that, nashauri wakuu chadema wakae chini na wa-shut down media for three months kupunguza impurities and reach out to wapinzani ili kujenga upya upinzani
Mimba tena!
ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.
Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.
Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.
Amewataka viongozi wa Chadema wawe matured na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).
Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.
Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.
Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.
Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.
Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010