CUF na Operesheni "Zinduka"

CUF na Operesheni "Zinduka"

Mbunge wa Viti Maalumu(CUF), Mkiwa Kimwaga amemwanika mbunge wa jimbo la Karatu, Dr Slaa kuhusu unafiki wake. Mheshimiwa Kimwaga aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama chake juzi kwenye operesheni zinduka katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa furahisha katika wilaya ya Nyamagana.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza mbunge huyo amesema kwamba Dr Slaa ni mtu anayeongoza kwa unafiki kwa kuwasema mafisadi wa CCM wakati ambapo yeye mwenyewe ameoa mke ambaye ni diwani wa CCM.

Kutokana na hali hiyo mbunge huyo aliwataka wananchi kuzinduka na kukichagua chama cha CUF kwa kuwa kina viongozi ambao hawana doa lolote la ufisadi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa siasa wa chama hicho, Mbarara Maharagande amewataka watanzania kuipuuza Operesheni Sangara inayofanywa na CHADEMA kwa kuwa haina maslahi yoyote kwa taifa.

"Hao CHADEMA wanapita na kuwaita wananchi kuwa ni Sangara. Wana dharau sana na hawana maslahi yoyote kwenu hivyo ni vyema mkawapuuza", alisema Maharagande.

Hata hivyo mkutano huo ulikaribia kuingia dosari baada ya kikundi kimoja cha wahuni kilichokuwa kinahudhuria mkutano huo kuanza kuzomea kila viongozi hao wa CUF walipokuwa wakianika ukweli kuhusu Dr Slaa.

Wakizungumzia hali hiyo, viongozi hao wa CUF walisema kuwa chama cha CHADEMA ni chama cha wahuni ambao hawataki kusikiliza sera za vyama vingine badala yake wapita wakivuruga mikutano ya vyama vingine. Viongozi hao walilitaka jeshi la polisi kuimarisha ulinzi na kupiga marufuku wavamimizi wa mikutano ya vyama vingine ili kila chama kipate fursa ya kueneza sera zake.

Mikutano ya Operesheni Zinduka inaendelea katika mkoa wa Mwanza ambapo kwa sasa inaelekea katika wilaya ya Ilemela.

.....ndiyohiyo

kwa jinsi nilivyoisoma hii habari sijaona mahalim kokote panapoonyesha kuanikwa kwa Dr. Slaa, isipokuwa mleta habari ndiye kaweka heading ya kuonyesha kuwa Dr. Slaa ameanikwa. Sijui kama HNH amefanya hivyo makusudi au kwa bahati mbaya.
hata hivyo suala la iktikadi ya kisiasa haliwezi lufungamana na ndoa yao.
Au huyo mbunge wa CUF anataka Dr. Slaa awe kama wapemba?manake huko ndiko hawaelewi somo la mke na mume kuwa na itikadi tofauti za kisiasa, huko ndiko imeshuhudiwa wanawake wakiachika kwa kuwa na itikadi tofauti na waume zao. Yaani kama mume ni CUF marufuku mke kuwa CCM, akithubutu tu, talaka.
 
hawa cuf nafikiri wanazidi kujichimbia kaburi. wamekosa cha kuongea. hata kama dr slaa ni mnafiki, wabunge wao wapo zaidi ya 30 bungeni wamefanya nini. ikitaka kufahamu watumwa wa ccm, tafadhari fuatilia cuf wanasema nini.

SIO TU CUF hata huyu mleta HOJA, unless na yeye awe ni CUF hapo kuna kuanika GANI??????????
Mbona mimi mke wangu Aserna/Simba wakati mimi MANU/YANGA? wakati wa mpirs tunsnuniana tukienda KITANDANI yanaisha?????
 
waacheni wafu wawazike wafu wenzao, CUF ni uozo mtupu, wabunge zaidi ya 30 sioni mchango wao vidi ya vita vya ufisadi, kama mpinzani hapambani na ufisadi naye ni fisadi
 
Hivi nyinyi mnafikiri jeraha walilolipata Bukoba ni mchezo?!!!! Nadhani jeraha hilo limeruhusu maji taka yaingie vichwani mwao
 
Ukisikia kukosa sera ndo huko,CUF badala ya kunadi sera zao wanaanza ooh Dr. Slaa ameoa mke mwanachama wa CCM,mbona makongoro nyerere alitofautiana na baba yake alipoona CCM haina dira akaenda NCCR enzi za Mzee wa injii hii,walichokionyesha CUF ni ufinyu wa sera walionao maana tunategemea kwenye operation zinduka waongee mambo ya maana ikizingatiwa uchaguzi wa serikali za mitaa ni mwaka huu wanaanza kuongea mambo ambayo hayana kichwa wala miguu,nadi sera tujue una lipi jipya na mwaka huu aliyekuwa anawaokoa upande wa bara ndo kahama chama kazi mnayo.
 
Mbunge wa Viti Maalumu(CUF), Mkiwa Kimwaga amemwanika mbunge wa jimbo la Karatu, Dr Slaa kuhusu unafiki wake. Mheshimiwa Kimwaga aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama chake juzi kwenye operesheni zinduka katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa furahisha katika wilaya ya Nyamagana.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza mbunge huyo amesema kwamba Dr Slaa ni mtu anayeongoza kwa unafiki kwa kuwasema mafisadi wa CCM wakati ambapo yeye mwenyewe ameoa mke ambaye ni diwani wa CCM.

Kutokana na hali hiyo mbunge huyo aliwataka wananchi kuzinduka na kukichagua chama cha CUF kwa kuwa kina viongozi ambao hawana doa lolote la ufisadi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa siasa wa chama hicho, Mbarara Maharagande amewataka watanzania kuipuuza Operesheni Sangara inayofanywa na CHADEMA kwa kuwa haina maslahi yoyote kwa taifa.

"Hao CHADEMA wanapita na kuwaita wananchi kuwa ni Sangara. Wana dharau sana na hawana maslahi yoyote kwenu hivyo ni vyema mkawapuuza", alisema Maharagande.

Hata hivyo mkutano huo ulikaribia kuingia dosari baada ya kikundi kimoja cha wahuni kilichokuwa kinahudhuria mkutano huo kuanza kuzomea kila viongozi hao wa CUF walipokuwa wakianika ukweli kuhusu Dr Slaa.

Wakizungumzia hali hiyo, viongozi hao wa CUF walisema kuwa chama cha CHADEMA ni chama cha wahuni ambao hawataki kusikiliza sera za vyama vingine badala yake wapita wakivuruga mikutano ya vyama vingine. Viongozi hao walilitaka jeshi la polisi kuimarisha ulinzi na kupiga marufuku wavamimizi wa mikutano ya vyama vingine ili kila chama kipate fursa ya kueneza sera zake.

Mikutano ya Operesheni Zinduka inaendelea katika mkoa wa Mwanza ambapo kwa sasa inaelekea katika wilaya ya Ilemela.

.....ndiyohiyo

The pathetic diatribes characterized by this type of hollow talk and punctuated with a ton of grossly diseased and shamelessly opportunistic misguided attacks, quite apart from achieving the intended harm on the target, serve well in exposing the base and deplorably helpless and quite possibly irredeemably ignorant nature of the attacker.

The lack of depth, policy, political acumen, communication tact and the obvious employment of some barely masked stale machinations reveal a somber disposition forwarded by these devious demons hardly making an effort at hiding their horns.

The lack of respect for the masses by squandering this opportunity to talk issues, and instead focusing on petty nitty-gritties underscores a deeper level of unreadiness.The cynical rivalry with an opposition figure betrays gravely misplaced priorities on the part of CUF, which should really focus on unseating CCM and gaining more parliament seats.The timing of these attacks leave much to be desired and a big question mark on whether CUF and some of it's ranking members are irked by the defection of some of it's ranking members to CHADEMA.

If this is the correct reflection, then the imbalanced CUF has a lot of maturing to do.
 
Ukisikia kuanza kuishiwa mtaji wa kisiasa ndio huku! CUF msituletee siasa za kizamani kama mlivyotaka kuleta kule pemba watuy wakashindwa kuzikana kwa sababu ya tofauti za kiitikadi. Unafiki uko wapi Dr Slaa kuowa diwani wa CCM, kwanza mi nafikiri Dr Slaa anastahili pongezi kwa hili, kaweza kuweka tofauti zake za kiitikadi pembeni na kujinga familia na mpinzani wake kisera. Huyo mbunge mbona yeye hasemi mume wake ni chama gani (kama na mume), afadahli tunajua Dr Slaa mke wake ni CCM, mbona hamsemi mke wa Lipumba, Seif, Juma Duni, Hamad Rashid, huu ubaguzi wenu ndio mnajimaliza. Zindukeni!
 
hiyo ndo CUF bwana hawana lolote chama kisichokuwa na dira tena na watazomewa sana tu wasipoangalia pemba pia ndo hivyo inaondoka hicho ni kifo cha mfa maji poleni sana CUF you are truly running out of time while making little pace ahead with a supersonic speed back.
 
Absolutely nonsense, hawa CUF hawana maana yoyote, ni wabaguzi, wadini na watu wenye fitina, kama hawana sera waendelee kubaki huko zanzibar ambako watu wanapenda udini, ukabila na waafitini.Tukiangalia kwa umakini, sasa huo ndo upinzani gani kama siyo unafiki, idadi ya wabunge CUF bungeni ni wangapi na wamefanya nini mpaka sasa? real they are very much disaponting us, au ni mapandikizi ya CCM?
 
Duh! Yaani CUF imefulia kiasi hiki! Hawa sasa afadhali waanzishe kundi la Taarab tu waendeleze mipasho. Siasa imewashinda! Mie niliposikia wanaanza Operesheni Zinduka nikadhani kuna kitu cha maana kinakuja ili wapate support ya wananchi. Hii imekaa vibaya. Hebu angalia hata anachoongea mwenyekiti wao LIPUMBA, ni pumba tupu. Au wamelogwa na CCM? Aibu...
 
Mbunge wa Viti Maalumu(CUF), Mkiwa Kimwaga amemwanika mbunge wa jimbo la Karatu, Dr Slaa kuhusu unafiki wake. Mheshimiwa Kimwaga aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama chake juzi kwenye operesheni zinduka katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa furahisha katika wilaya ya Nyamagana.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza mbunge huyo amesema kwamba Dr Slaa ni mtu anayeongoza kwa unafiki kwa kuwasema mafisadi wa CCM wakati ambapo yeye mwenyewe ameoa mke ambaye ni diwani wa CCM.

kWELI HUKU NI KUISHIWA SERA.

KWANI NI DHAMBI MKE AKIWA SHABIKI WA YANGA NA MUME KUWA SHABIKI WA SIMBA.

HAKIKA SUALA LA NDOA HALITENGANISHWA NA ITIKADI ZA SIASA.

MAMA HANA SERA
 
KAFU wana misimamo na miongozo ya Kiislam .Ukitaka kumuoa Muislam unasikia wanalia lazima ubadili dini .Lakini unajiuliza nyumbani kwa Mzee Hamidu ume enda kutafuta dini ama binti yake awe mkeo ? Udini huu unawatokea kubaya sasa na hata wanashindwa kujua kwana Slaa kaoa mwanamke mpenzi na diwani wa CCM na hata angaliwa ni binti wa CCM si dhambi kuoa mke na hajaoa wala kushikamana na CCM.

Akili ni mali .Endeleeni kukanyaga mafuta tweneda tutaona wapi mafuta yataishia , muda si mrefu .
 
Nadhani CUF sasa kisiwe chama cha siasa ila kiwe ni kikundi cha uchekeshaji kama ilivyo Comed
 
hawa cuf nafikiri wanazidi kujichimbia kaburi. wamekosa cha kuongea. hata kama dr slaa ni mnafiki, wabunge wao wapo zaidi ya 30 bungeni wamefanya nini. ikitaka kufahamu watumwa wa ccm, tafadhari fuatilia cuf wanasema nini.

kumbe pemba kuna wabunge zaidi ya dar+mwanza +arusha kwa pamoja wawtu wenyewe laki saba
nasikia kuna wabunge 25
 
Chadema pelekeni operesheni sangara pemba mkazike hii takataka coz imeshindwa kuwatumikia wananchi.
Lipumba kwishen kabisa
 
Niliwahi kusema hili la mke kuwa CCM au mume kuwa CUF au vinginevyo,hii inamaana wote wawili hawafai ,mke na mumewe watafute biashara wafanye ,haiwezekani haiwezekani ,maana hata kuelekea haielekei isipokuwa mnailazimisha tu ,na hili sio kwa walio nje ya Chadema hata wale waliokuwa ndani ya Chadema wanaliona ni jambo la ajabu kabisa ,ikiwa mke au mume ameshindwa kumshawishi mwenziwe kwa sera za Chama chake itawezekanaje kuwashawishi wengine ,ni lazima hapo pana walakin.
DR Slaa jitahidi sana kumshawishi mama watoto ajiunge na Chadema ,maana kama nikipiga picha unapata Raisi ni Chadema na First lady ni CCM ,yaani mmoja ataendeleza sera za mafisadiCCM na mwengine za Chadema.
 
Mawazo hafifu haya na ukandamizaji wa uhuru wa watu wa aina hii unapatikana makao makuu ya waislam kule Iran .Kama unapinga sema tuanze mjadala .
 
DR Slaa jitahidi sana kumshawishi mama watoto ajiunge na Chadema ,maana kama nikipiga picha unapata Raisi ni Chadema na First lady ni CCM ,yaani mmoja ataendeleza sera za mafisadiCCM na mwengine za Chadema.

Ninavyoelewa hivi sasa Dr. Slaa ni kiongozi wa Chadema na Mama Slaa ni kiongozi CCM na wanaishi bila taabu ama ? Huko Marekani California nasikia The Terminator ni Republican Governor lakini First Lady ni Democrat, mbona hamna taabu ? Mkuu Mwiba, naamimi wewe ni CUF kweli kweli lakini fanya kama alivyofanya Lwakatare please jump ship - it is sinking !
 
KAFU wana misimamo na miongozo ya Kiislam .Ukitaka kumuoa Muislam unasikia wanalia lazima ubadili dini .Lakini unajiuliza nyumbani kwa Mzee Hamidu ume enda kutafuta dini ama binti yake awe mkeo ?....

Na muislamu akitaka kuoa mkristo haya hakutani nayo? Hivi kuna Padre ama Mchungaji anaweza kufunga ndoa ya muislamu na mkristo?Acha prejudice, wote tuna matatizo hayo....

omarilyas
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom