CUF na Operesheni "Zinduka"

CUF na Operesheni "Zinduka"

Taarifa zilizopo ni kuwa operation Zinduka inaenda kwa mafanikio makubwa na wananchi wameikubali kwani kila mkutano unaofanywa watu wanaofurika kwa wingi sana..
 
Taarifa zilizopo ni kuwa operation Zinduka inaenda kwa mafanikio makubwa na wananchi wameikubali kwani kila mkutano unaofanywa watu wanaofurika kwa wingi sana..

Mkuu mwaga picha basi, Make za Sangara tuliziona sana.
 
Miwba,
Mkuu wangu ni lazima ukubali kwamba Lipumba amechemsha na wala sii kidogo.. kibaya zaidi hakuanza jana, muda sasa hivi anazungumza vitu ambavyo havilingani na elimu yake..Yawezekana alipeta sana mchele alokuwanao kabakia na pumba..Kupeta mpunga kunahitaji ujuzi, laa sivyo mchele wote unaweza ishia chini mchangani na ukabakia na pumba ktk ungo - ndicho anachokifanya mkulu wetu..
Sijui umeliona jibu la Mr WBSlaa au unakimbia kivuli chako,labda nikupe kipande ambacho Mkuu Slaa alikigusa
...Kama wote ni maaskari dhidi ya ufisadi, basi nadhani jibu sahihi ni kumwaga ufisadi wa yeyote tunayemtuhumu bila kujali cheo, nafasi yake, ili jamii iweze kufahamu adui yetu hasa ni nani ili iweze kuchukua hatua stahiki...
Umiona hako kamstali ,naweza kusema Lipumba ametumia hapo ,kinachohitajika ni Lipumba kuwajibika katika kutoa ushahidi otherwisw itakuwa ni empty words ,kisiasa empty word ipo na inafanya kazi kwa kiwango chake until iwe challenged ,pengine kwa ujanja wa kutumia vyombo vya habari kama itawezekana kuwakutanisha wenye vyama kwa maana ya wakuu wa vyama na hapo kuna masuala ya papo kwa papo ,na hili liwe kama utamaduni haswa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu ,ili tuwasikie wakuu wakipeana majibu kutokana na harakati za kichama kama huko kushuhutumiana ,ila inatakikana mwandishi jasiri asie elemea mrengo wowote ule ,katika kuzabua masuali ,na moja linawezekana hilo la Lipumba kusema Wakuu wa Chadema ni mafisadi (Shutuma mnazoziona kama ni empty words).

Sasa hayo maneno ya sijui kachemsha au kasonga ni madudu yasio na macho na yanaweza kuuliwa kirahisi kabisa.Labda ninachokingojea ni kuona Lipumba ameweka ni jinsi gani WaChadema walihusika au walifanya ufisadi gani ? Ila kwa sasa namuunga mkono Lipumba kwa kuwa bado Chadema hawajajibu kupitia mikutano au vyombo vya habari ,wakidai ushahidi au wakikana kwa maana wananchi wengi watapata kusikia na kupima ukweli ni upi.Kama CUF hawana ushahidi itakuwa wameweka maji kwenye pakacha na hili litawezekana tu pale Chadema watakapo dai ushahidi ,japo wanajua haupo.
 
Mheshimiwa Mwiba, Hebu taja hizo kashfa zinazohusu wana-Chadema. Lipumba amehusisha Muasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei na pia Bob Makani na kuchomwa kwa jengo la BoT. Tukio hili lilikuwa la mwaka 1984 wakati Charles Nyirabu akiwa Gavana. Sina hakika kama Bob Makani alikuwa Deputy Gavana wakati huo.

Mzee Mtei alikuwa Executive Director wa IMF wakati huo na alikuwa Washington D.C. siku hiyo. Amenijulisha kuwa alipigiwa simu na rafiki yake wa Dar es Salaam akimwarifu kuwa jengo alilohusika wakati likijengwa lilikuwa linateketea kwa moto. Sasa Profesa Lipumba anahusishaje Mzee wa watu na kuungua huko?
 
Mheshimiwa Mwiba, Hebu taja hizo kashfa zinazohusu wana-Chadema. Lipumba amehusisha Muasisi wa Chadema, Mzee Edwin Mtei na pia Bob Makani na kuchomwa kwa jengo la BoT. Tukio hili lilikuwa la mwaka 1984 wakati Charles Nyirabu akiwa Gavana. Sina hakika kama Bob Makani alikuwa Deputy Gavana wakati huo.

Mzee Mtei alikuwa Executive Director wa IMF wakati huo na alikuwa Washington D.C. siku hiyo. Amenijulisha kuwa alipigiwa simu na rafiki yake wa Dar es Salaam akimwarifu kuwa jengo alilohusika wakati likijengwa lilikuwa linateketea kwa moto. Sasa Profesa Lipumba anahusishaje Mzee wa watu na kuungua huko?
Inabidi mumtafute Lipumba ajibu ,na kuwa makini sana katika kumjua muhalifu Mkapa alipopeleka majeshi kwenda kuua Pemba alikuwa hayupo hapa nchini ,hilo halimfanyi kuwa yeye hakuhusika na misheni nyingi mhusika mkuu huwa hakai karibu....Ila ninachosubiri kuona ni ushahidi sasa na wewe bora usubiri na ufahamu kukaa kimya ni kukubali. Nafunga majadiliano kwa upande wangu.
 
It is part of the history of Tanzania that Mzee Edwin Mtei ceased to be Governor of the BoT in 1974 when he was appointed Secretary General of the then East African Community. He was an Exucutive Director of IMF residing in Washington DC when the BoT building was burnt down in 1984.

Wewe Mwiba unayesema nimekutana na Mzee Mtei "uchochoroni" una maanisha kwamba amesema uongo? Miaka kumi baada ya Mzee Mtei kuacha uGavana ndipo jengo la BoT lilipoungua. Kama wewe Mwiba ni mwanaJF, basi jiondoe maana you are not a great thinker.

Naona ufafanuzi uliotolewa kuhusu hotuba hizi za CUF "Kuzinduka" kwamba ni Maharagande aliyetoa hiyo miropoko kwamba Mzee Edwin Mtei alihusika na uchomaji moto wa jengo la BoT. Hata hivyo ni jukumu la kiongozi wao, Profesa Lipumba, kuwasahihisha pale wanapokosea na kutoa matamshi ambayo hayaingii akilini. Endapo Mtei atachukua hatua za kisheria kusafisha jina lake, CUF itakuwa ina-divert efforts zake toka mambo muhimu ya politics ili itoe defence in court.

Mzee Mtei amenieleza kwamba, Lipumba aliteuliwa Mshauri uchumi Ikulu baada ya Profesa Justinian Rweyemamu, aliyekuwa Mshauri Uchumi wa Nyerere, kuungana na kundi la Wataalamu waliokuwa wanatayarisha mapendekezo juu ya Operations of Transnational Corporations huko Geneva, Uswisi. Mzee Mtei kama Secretary General wa EAC alikuwa anawakilisha East African Community ktk kundi hilo; lakini kutokana na kuvunjika kwa EAC na yeye kuteuliwa Waziri, alimpendekeza Rweyemamu achukue nafasi yake.

Haya yote Mzee Mtei amenieleza kutokana na kwamba Lipumba anafahamu kwamba hata yeye akiwa Ikulu, Mtei alikuwa waziri wa fedha, na original jengo la BoT lilikuwepo. Sasa kwa nini awachie Maharagande kutunga hadithi za uongo? Labda amechoka na siasa. Arudi UDSM kama mhadhiri mwandamizi.
 
Last edited:
Mbunge wa Viti Maalumu(CUF), Mkiwa Kimwaga amemwanika mbunge wa jimbo la Karatu, Dr Slaa kuhusu unafiki wake. Mheshimiwa Kimwaga aliyasema hayo katika mkutano wa hadhara wa chama chake juzi kwenye operesheni zinduka katika mkutano uliofanyika katika uwanja wa furahisha katika wilaya ya Nyamagana.

Akihutubia mamia ya wakazi wa Mwanza mbunge huyo amesema kwamba Dr Slaa ni mtu anayeongoza kwa unafiki kwa kuwasema mafisadi wa CCM wakati ambapo yeye mwenyewe ameoa mke ambaye ni diwani wa CCM.

Kutokana na hali hiyo mbunge huyo aliwataka wananchi kuzinduka na kukichagua chama cha CUF kwa kuwa kina viongozi ambao hawana doa lolote la ufisadi.

Katika hatua nyingine, Mkurugenzi wa siasa wa chama hicho, Mbarara Maharagande amewataka watanzania kuipuuza Operesheni Sangara inayofanywa na CHADEMA kwa kuwa haina maslahi yoyote kwa taifa.

"Hao CHADEMA wanapita na kuwaita wananchi kuwa ni Sangara. Wana dharau sana na hawana maslahi yoyote kwenu hivyo ni vyema mkawapuuza", alisema Maharagande.

Hata hivyo mkutano huo ulikaribia kuingia dosari baada ya kikundi kimoja cha wahuni kilichokuwa kinahudhuria mkutano huo kuanza kuzomea kila viongozi hao wa CUF walipokuwa wakianika ukweli kuhusu Dr Slaa.

Wakizungumzia hali hiyo, viongozi hao wa CUF walisema kuwa chama cha CHADEMA ni chama cha wahuni ambao hawataki kusikiliza sera za vyama vingine badala yake wapita wakivuruga mikutano ya vyama vingine. Viongozi hao walilitaka jeshi la polisi kuimarisha ulinzi na kupiga marufuku wavamimizi wa mikutano ya vyama vingine ili kila chama kipate fursa ya kueneza sera zake.

Mikutano ya Operesheni Zinduka inaendelea katika mkoa wa Mwanza ambapo kwa sasa inaelekea katika wilaya ya Ilemela.

.....ndiyohiyo
 
hawa cuf nafikiri wanazidi kujichimbia kaburi. wamekosa cha kuongea. hata kama dr slaa ni mnafiki, wabunge wao wapo zaidi ya 30 bungeni wamefanya nini. ikitaka kufahamu watumwa wa ccm, tafadhari fuatilia cuf wanasema nini.
 
HIvi hawa CUF mpinzani wao ni CCM au CHADEMA? khee sasa Dr.Slaa kuoa diwani wa CCM ndo nini?mhhh CUF yaleyale ya kutokuzikana huko zenji yanataka kuletwa huku
 
Kwamba Slaa ameoa mke ambaye ni mwanachama wa CCM si siri kiasi cha kusema kuwa ukiisema utakuwa umemwanika. hebu tupe huo uanikaji
 
Mke wa Dk. Slaa abanwa
• Adaiwa kutoa siri za ubadhirifu Hanang

na Ramadhani Siwayombe, Hanang’


amka2.gif
MKE wa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilbrod Slaa, Rozi Kamili, ambaye ni diwani wa Kata ya Basotu (CCM), yupo matatani baada ya kuhojiwa na Kamati ya Maadili ya Madiwani wa Halmashauri ya Hanang', akituhumiwa kutoa siri za ubadhirifu wa fedha ndani ya halmashauri hiyo.
Licha ya kamati hiyo ya maadili kuwahoji lakini juzi imeshindwa kutangaza hatua za kinidhamu atakazochukuliwa diwani huyo na wengine watatu wa halmashauri hiyo wanaotuhumiwa kwa kukiuka kanuni za maadili za madiwani.
Madiwani wengine waliohojiwa na kamati hiyo ambao wanasubiri maamuzi ni Anju Mang'ola (CCM), Kata ya Gehandu, Leonard Gepchojiga (CCM), Kata ya Mogitu na Venosa Bura, Viti Maalumu (CHADEMA).
Hata hivyo ajenda ya kutangazwa uamuzi wa kamati hiyo, ilitarajiwa kutangazwa jana, lakini iliondolewa ghafla, kwa sababu ambazo hazikuweza kufahamika mara moja.
Diwani Mang'ola na Gapchojiga wanatuhumiwa kukataa watu waliohamishwa katika Mlima Hanang wapewe ardhi katika mashamba yaliyokuwa yakimilikiwa na Shirika la Taifa la Chakula (NAFCO), ambayo baadhi yaliyorejeshwa kwa wananchi yapo katika vijiji vyao.
Diwani Bura anatuhumiwa kwa kushawishi wafanyabiashara katika Soko la Katesh kutolipa kodi, hadi mikataba yao imalizike, baada ya kujenga wenyewe vibanda vyao.
Akizungumza nje ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri hiyo mara baada ya kuahirishwa kutangazwa kwa hatua zitakazochukuliwa dhidi yao, mke wa Dk. Slaa, Rozi Kamili, alisema wanashangaa kwa kushindwa kutangazwa hatua hizo, kwani wamehojiwa zaidi ya mwezi mmoja uliopita.
“Walituhoji na tumesisitiza tunachokiamini kuwa ni ukweli na kutoa vielelezo vya kuthibitisha hayo, pia nimeiambia kamati kama inaona nimekiuka kanuni wanifikishe mahakamani,” alisema diwani huyo.
Diwani Kamili, alisema yeye ameibua tuhuma zilizomo ndani ya halmashauri hiyo, za wizi wa sh milioni 20, ambazo zilitengwa kwa ajili ya kukarabati vituo vya afya na zahanati na mradi huo haujafanyika na mwaka wa fedha uliishapita.
Mang’ola, Gapchojiga na Bura kwa pamoja wanadai kuwa tuhuma zinazowakabili ni za kupandikizwa ili kuwachafua, hivyo wanasubiri uamuzi wa kamati utolewe ili nao wapate nafasi ya kwenda mahakamani.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri hiyo, Ndoliwa, alikataa kuzungumza na waandishi wa habari walipomfuata kutaka kufahamu sababu za kutotangazwa kwa uamuzi wa kamati ya maadili katika kikao hicho.
 
Hoja zinapoisha,vioja huchukua nafasi.Ni vema kama watawaeleza wananchi kuwa ni nini watadeliver endapo watachaguliwa. Kuliko hzi bla bla wanazoendelea kuzpga sasa.Hivi wamesahau kuwa JK alishndwa kwa 80%??Hii inaweza ikareflect kuwa wanagombea the remaining 20%.Ni kama vita vya panzi vile.
 
wamepoteza mwelekeo...kwa nini wasione kuwa slaa anakuwa na advantage ya kujua nini kinaendelea ndani ya CCM kwa kuoa diwani wa chama hicho? CUF go to hell
 
Kafu ooh sory kafie ooh nop CUF kwisha habari yao, watafute habari zenye mvuto kwa wananchi sisi tunataka mambo yaende mbele, watabaki kuambulia kura 20 kati ya 300,000 na idadi itashuka kadri tunavokaribia uchaguzi, wamefulia tayari, hawana jipya hawajafanya kitu, more viongozi wao wanakula hela za govt kwa madai ya muafaka, pambaf kabisa hao KAFU.
 
Hawa CUF wanajichimbia kaburi wao bila ya kujijua kama ndo wanakufa kisiasa.
Kikubwa wanaona wivu CHADEMA wanavyo paa kwa mafanikio na ushindani wa juu ndo maana wao ni moja na TLP kila kukicha hawaachi kukishambulia chama cha CHADEMA wanashindwa kujenga hoja kuking'oa chama tawala madarakani wao wamejaa na chuki dhidi ya chama cha upinzani. Na wananchi sasa wamesha washtukia CUF ni bora wakajiimarisha huko visiwani.
 
Kafu ni kichekesho tu. Kwishney kabisa.
Wakati wenzao wanaisota kidole serikali ya mafisadi wakileta hoja kali mezani wao wanakuja na hoja ya mke wa mtu.
Kwani mimi nikiwa kafu ni lazima nimlazimishe na mke wangu awe kafu?
Je akikataa tutengane?
Jamani mnayasika ya kafu hayo? tukiwasema hapa wanatokeza memba wengine kutaka kutumeza. Haya basi jioneeni wenyewe.
Wao na wenzao sisi Maf...... lao moja.
Wakizomewa wanataka kupigana ngumi. Lakini hii style si imekuwa initiated na sisi Maf... kupitia yule puppet wao anaitwa Komba?
Kuna wimbo ule anaoimba " Ohh wazomee wavunje vunje..............🙂"
Na sasa wale waliokuwa wanakuwa instructed kufanya hayo wamegundua kuwa walitapeliwa na wanafanya yale yale waliyofundishwa dhidi yao wenyewe.
Nakwambia huu ni mwanzo tu. Ngoja 2010 waone zomea zomea itakavyokuwa watajua mchicha si bangi!
 
Hapa kaanika nini ? Hoja ipi inamfanya mleta hoja hii hapa aje kasi na utumbo huu ? Hii forum inakosa mwelekeo ama wachangiaji mamluki ndiyo wanataka kutuyumbisha ?
 
Hivi hii habari imeandikwa kwneye chombo chochote cha habari? ili nione kama uandishi wetu umefikia hapo?

Hao wabunge wa viti maalumu ni bora waondolewa kabisa maana hawajui siasa, hawana hoja, na hawajui kujenga hoja,, wamepewa nafasi hiyo kwa sababu nyingine kabisa! Ni wakati wa kuabolish hivi vitu kila mtu aenda kwa wananchi amwage sera zake, kisha tuone kama haowa wanao'mwanika' Dr Slaa kuwa mke wake ni CCM watachaguliwa!
 
Any way , lazima tuwe realistic, huyu mama ana uwezo gani wa kufikiri, we imagine mambo ya kuoa yanakujaje kwenye kampeni, kwa hiyo ana maana kuwa ukiwa CDM HUWEZI KUOA CCM au CUF, mbona huyu mama amepotoka. cha msingi labda angeongelea kuwa Dr Slaa anawafunika Bungeni, may huyu mama alikuwa anataka kuongelea hayo, Cuf waache wapiganaji waendelee kupigana, kama wao nio purpet basi wakae kimya, labda ajenda yao ni kutaka kuua upinzani, tumewastukia, CDM na itadumu daima, na inshallah Mungu yu pamoja nasi, tutaikomboa Tanzania tu. Mengi mtasema, lakini CDM ni alama ya ukombozi Tanzania.

Rom
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom