CUF na Operesheni "Zinduka" | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CUF na Operesheni "Zinduka"

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Habarindiyohiyo, Jul 14, 2009.

 1. H

  Habarindiyohiyo JF-Expert Member

  #1
  Jul 14, 2009
  Joined: Aug 11, 2008
  Messages: 263
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Chama cha Wananchi(CUF) kimezindua Operesheni yake maarufu kama Zinduka kwa kutoa hadharani siri nzito. Siri hiyo ilitolewa na Mwenyekiti wake Profesa Lipumba katika mfululilizo wa mikutano ya hadhara iliyofanyika juzi, jana na leo mkoani Mwanza.

  Profesa Lipumba akihutubia mikutano hiyo ameeleza kwamba tishio kubwa la amani na maendeleo ya Tanzania ni kundi la watu aliowaita mafisadi nyangumi. Profesa Lipumba ameeleza kuwa watu hao hutumia vyombo vyao vya habari kueneza ubaguzi katika taifa kwa kisingizio cha vita dhidi ya ufisadi.

  Katika hatua nyingine, chama cha CUF kimekituhumu chama kingine cha upinzani cha CHADEMA kuwa ni CCM B. CUF imedai kuwa chama cha CHADEMA kinapiga kelele za ufisadi wakati chenyewe kimejaa ufisadi.

  Wakieleza ushahidi wa wazi kuhusu ufisadi wa CHADEMA, viongozi mbalimbali wa CUF wameweka wazi kwa wananchi katika hotuba zao katika mfululizo wa mikutano hiyo kuwa viongozi wa CHADEMA ni mafisadi.

  Viongozi hao wa CUF wamesema kuwa CHADEMA imeasisiwa na mafisadi wakina Edwin Mtei na Bob Makani ambao waliiba katika benki kuu na kuchoma benki hiyo ili kupoteza ushahidi.

  Viongozi hao wameeleza kwamba hata viongozi wa CHADEMA waliofuata wakina Freeman Mbowe, Dr Slaa na Zitto Kabwe wote wana tuhuma mbalimbali za ufisadi zinazowakabili.

  Viongozi hao wamewataka wananchi kuzinduka na kuunga mkono chama cha CUF kwani ndio chama pekee cha siasa chenye viongozi safi na walio mstari wa mbele kupambana na CCM.

  Chama hicho kimeeleza kuwa ni viongozi wa CUF ndio wana historia ya kufungwa na kusumbuliwa na CCM kutokana na misimamo yao.
   
 2. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #2
  Jul 14, 2009
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Huyu naye alikuwa wapi wakati wote? Atueleze vile vile uhusiano wake na RA
   
 3. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #3
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mimi nakwambia kuwa CUF ndio inapoteza ulekeo wake na Kuwasema CHADEMA hakuna maana yoyote ile, Narejea makala ya mchambuzi wa kisiasa kuwa CUF katika operetion zinduka adui wao mkubwa ni CCM na Sio CHADEMA, Kamwe CUF hawawezi kusema juu ya hali hii na kupata umarufu kupitia CHADEMA na pia itakuwa vigumu sana kupata support kubwa,
   
 4. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #4
  Jul 14, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  kweli RA kawatuma kuja kubomoa upinzani sasa.CUF wamechanganyikiwa mpaka wamekubali kutumiwa.wanachofanya wanazidi kujibomoa.
   
 5. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #5
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Wanajiboa wao mwenyewe na sio siri CUF inabidi wabadilike sana sana na sio kuwasema CHADEMA hata kidogo na pia huku bara sio sawa na kule visiwani hivyo waje na mikakati mikubwa sana na siyo udaku
   
 6. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #6
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mchambuzi wa Gazeti la Tanzania Daima Mr Kibanda aliwahi kuyasema mambo haya na kwa kuwaonya CUF na CHADEMA pia sasa ndio kuchanganyikiwa kwenyewe na hawajui la kufanya kwa sasa na pia walikuwa wanapoteza muda mwingi sana kuhusu Mwafaka na kuliko active politics kwenye majimbo wao CHADEMA walianza muda mwingi sana kuhusu operation SANGARA
   
 7. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #7
  Jul 14, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  mie sikutegemea kabisa kama watatoka hivi.yani "MENGI" ndio wanamuona mbaya wa nchi kuliko wale mafisadi wengine? hii kali ya mwaka.
   
 8. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #8
  Jul 14, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Yaani jamaa u-Profesa wake anaudhalilisha si kidogo. Maana hii ni wazi kabisa kuwa katumwa na RA kubomoa upinzani. Na hajui kuwa watu sasa wamechoka ni hizi porojo tu za kurushiana maneno bali wanataka mikakati hasa ya kulinusuru taifa kutoka kwenye lindi la umaskini ikiwemo kudhibiti wizi wa rasilimali za taifa na si hizo porojo za maneno. Arudi akajipange upya maana bara hakuendeshwi kwa jazba za chuki dhiki ya mtu fulani tu.
   
 9. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #9
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Tupe ushahidi wa hayo unayosema...kabla hatujaita ni umbea
   
 10. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #10
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  So wewe tu pekee yako maana hawa jamaa walikuwa wanapoteza muda mwingi sana kwa ajili ya mwafaka na huku walikuwa wanapoteza pesa za walipa kodi juu wa mwafaka na hakuna mwafaka wala nini sasa wao ndio wamezinduka sasa lakini wao CHADEMA walifanya siku nyingi sana
   
 11. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #11
  Jul 14, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Kweli inasikitisha sana. Watu walioifilisi nchi yetu ndo wanaonekana bora na huyu Mangi wa watu ndo anaonekana kuwa mbaya wao. Lol! Kazi ipo. Hii nchi yetu hii, mhhhhh! Ngoja tusikilizie.
   
 12. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #12
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Kweli mimeamini kwamba akili ya Lipumba ni Pumba kama huko aliko.Anataka wazinduke yeye analala .Yeye anaweza kusimama na ajenda dhidi ya Chadema akafanikiwa kweli huyu jamaa ? Hajui kwamba Bara CUF haina nguvu na ushahidi ni huo kwamba hata pale walio waislam wengi kama Dar bado CUF hata seikali za mtaa haina kiongozi .Kwa nini asianzie kule Pemba ambako ndiko kuna mizizi yao na watu wana nyanyasika ? CUF kweli tu ndiyo waaga hivi hivi .
   
 13. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #13
  Jul 14, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Tumanini unataka ushahidi wa namna gani wakati maneno ya Lipumba yanajieleza? Hivi wewe unafurahi tu unapoona hawa akina Rostam wanazidi kuifilisi hii nchi? Usianze kuleta element za udini tena kwenye jambo hili yatupasa tupambane na mafisadi bila kujali dini zetu.
   
 14. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #14
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli amechanganyikiwa kweli, Inabidi aseme ni kwanini mwaka 2005 walikosa hata mbunge mmoja huku Bara?? Then ni kwanini alikuwa anapoteza muda mwingi sana kwenye mwafaka na CCM huku akijua kuwa haliwezekani kabisa?? Lipumba kusema CHADEMa bara ni makosa makubwa sana
   
 15. W

  Wanzuki Senior Member

  #15
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 119
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  CUF ni chama cha Tanzania visiwani, huku bara wanapoteza muda! na huyu Lipumbu kawekwa tu kama ushahidi, hana lolote!! Kwa jinsi wanavyoendesha chama chao, hawawezi hata siku moja kupata umaarufu huku bara!
   
 16. M

  Mugishagwe JF-Expert Member

  #16
  Jul 14, 2009
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 295
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Lipumba kesha katiwa , anaonyesha yale madai ya watanzania kwamba CUF kuna udini mie naongezea anasimama kumtetea Rostam kwa mshiko na kwa kuwa wote wanatoka Tabora .Mtu mwenye heshima na akili timamu hata ndani ya CCM they will never stand for Rostam trust me and at least not in the open like this .Lipumba kweli pumba .Kesha jua CIF imekufa visiwani sasa anaisaidia CCM bara .
   
 17. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #17
  Jul 14, 2009
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  ushahidi ulishawekwa hapa mda mrefu sana.unaweza kusearch post zilizopita.
   
 18. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #18
  Jul 14, 2009
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  CUF wakitaka ku-protect credibility yao waeleze ufisadi wa hao waliotajwa. Si blah blah tu. Ukiangalia kwa makini CUF sasa inaanza kukosa mwelekeo baada ya kupigwa danadana ya MUAFAKA. Kama siasa zimekushinda acha kupiga blah blah bali toa FACTS.
   
 19. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #19
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Kweli hata mimi nashangaa sana kusikia maneno kama haya, Hata hiyo operation Zinduka ni kuiga tu kwa CHADEMa ambao walianza muda mwingi, kwanza aje na kuomba samahani kwa Watanzani kwa kupoteza kodi za wananchi Watanzania na pia muda kwa ajili ya mwafaka na pia nyinyi Ndugu zangu mtaona wenyewe baada ya uchaguzi wataanzisha MWafaka 5 na 6 na 7 ni ulaji hakuna jipya juu ya CUF bara, Walipoteza hata jimbo la TEMEKE, Bukoba na kule maswa sijui, Maana inatia shaka msimamo wa huyu jamaa au ndio kwa ajili wanatoka sehemu moja na wakina RA?? CUF mkitaka kupata watu acha kuwasema CHADEMA na Pia Lipumba ni mmoja wa JF aje kusoma humo ndani alama za nyakati juu ya hilo
   
 20. Tumain

  Tumain JF-Expert Member

  #20
  Jul 14, 2009
  Joined: Jun 28, 2009
  Messages: 3,158
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Kivipi mbona unataka kukwepa hoja nakuingiza udini?? labda wewe ndiyo umeanza udini??
  Lipumba anaongelea mafisadi wote either wako chadema, wako CCM it doesn't matter?? ,Masikio yangu yako huru nasubiria kusikia chadema wakijibu hizo tuhuma kwa faida ya nchi!!
   
Loading...