Dr. Willibrod Slaa
Public Figure
- Jul 1, 2008
- 675
- 1,523
Mwiba,Naona mmepandishwa mkenge, Yaani toka ajiunge ana zaidi ya mwaka na posti yake ya mwanzo ndio hii na kama amejiunga Dec 2008 bado hajakaribia hata mwaka yupo nusu ya mwaka ,hapa Usalama wa makao makuu JF unajaribu kuchomekea. Ila tiendelee...@newz
Kuna kifungu humo ambacho kilitokeza na mtu ambae alidai kumpigia simu Mtei katika posti moja iliyopita,kifungu hicho hakijapoteza hata spelling ni copy & paste.
Haya tukubalianeni kuwa Mtei imebidi amwage razi na kuingia tena hapa JF baada ya muda unaokaribia Mwaka ,sasa kama Ntei nae anataka aombwe radhi jamani sio kupitia hapa JF ,aitishe tu vyombo vya habari adai madai ya kutaka kusafishwa ,Bob Makani ni mwanasheria kigogo nae pia awakilishe hoja hizo za kuwadai CUF ushahidi ,au CUF waombe radhi.
Ila jamaa wa CUF wamesema wana ushahidi mzito juu ya madai yao ,hivyo sidhani kama itakuwa rahisi kusema waliteleza.
Hapa inaonekana Mtei kukanusha kuwa alihusika kuichoma moto benki ila ameshindwa kukanusha kuwa alikwiba ,Je anaogopa kuwa pengine kuna wizi alifanya na ushahidi wa wizi huo umepatikana ?
Kuna madai makubwa kutoka kwa WaTanzania wakidai uchunguzi kuhusiana na Mabenki yetu hasa Benki kuu umeanzia padogo ,wakihitajia uchunguzi huo ungeanza tokea miaka 30 nyuma na kuchunguza kimoja kimoja hatua kwa hatua ,wakimaanisha huu wizi wa miaka ya akina Mkapa ni padogo sa na kwa shughuli za kibenki ,inawezekana kabisa kuwa huu ni wizi ambao haukuanza jana wala juzi ni muendelezo tu wa wizi uliokuwa ukifanyika ambao waajiriwa wepya waliukuta na kuuendeleza ,ila kamba imekatikia pabaya.
Mtei ana uhakika gani ikiwa uchunguzi utarudishwa nyuma kwa miaka kadhaa ,yeye atasalimika ?
Wakati huo ilikuwa rahisi kuiba kuliko wakati tulio nao na mahesabu ya benki kwa wakati huo ilikuwa hakuna anaeweza kuhoji wala kuuliza ,muda huo akina Mtei na wenzake walikuwa wakitamba hapa Tanzania ,hakuna anaewakaribia ,WaTanzania walikuwa hawajui EPA ni madudu gani.
Hii mikataba haikuanza juzi na jana wala WaTanzania hawakuwa wakiifuatilia na kufahamu umuhimu wake na ni kwa jinsi gani iliididimiza Tanzania ,wala WaTz walio wengi hawakufahamu kodi inayopatikana na inayosamehewa ,akina Mtei ndio waliokuwa waidhinishaji wa mwisho katika mahesabu aidha kukopeshwa au kulipwa. Mtei hukuchoma moto je kuiba ?
Kama umekwiba kwa maana nyingine ulichoma moto na kupoteza ushahidi ila katika kuungua vitabu vikubwa mara nyingi haviungui vikamalizika.!!!
Mtei huyu si ndie yule Mwenyekiti pale Tanzania Coffee Research Institute tokea 2007 na wakulima wa kahawa tunawasikia hadi leo wanapiga kelele ?
Pamoja na kuheshimu kila mtu hapa JF, nilikwisha kusema, tusiendekeze hisia na majungu. Kama kuna mtu anafikiri Mzee Mtei aliiba, ashushe hapa. Tuna mambo muhimu zaidi ya kujadili kuliko hisia. Halindwi mtu, hata kama angelikuwa nani katika masuala ya ufisadi, lakini tusifanye JF kama mahali pa mjadala bila lengo, we need to do justice to this nation. Yeyote mwenye facts, aje clearly ili tujadili vema hoja, kuliko "unfounded" allegations.