Obhusegwe
JF-Expert Member
- Dec 28, 2008
- 231
- 28
Kaka hapo kama bado unahamu ya kutumia hiyo kadi ya CRDB inabidi uwe mvumilivu kwel kweli. Uwezokano mkubwa hapo tatizo lipo CRDB. My guess itakuwa kwamba hiyo kadi haijawa activated kwa ajili ya internate. Unauhakika kwamba iko activated? Na ulijaza kale kamkataba?
Nenda CRDB, hasa pale Azikiwe, waelezee Tatizo. Ukiona hamuelewani, waambie wakuunganishe na jamaa wa Card Center. Ukiongea na jamaa wa card center wasisitizie hiyo message, maana saa nyingine hata wao wanakuwa hawaelewi. Jibu watakalokupa, lipost hapa tafadhali.
Hatimaye mimi nimefanikiwa baada ya miezi kadhaa ya kupiga kwata na kupiga simu CRDB. Na tatizo lilikuwa kwamba system zao zilijikoroga, transaction ile ya paypal yenye verification code haikufanyika automatically, ikabidi ifanywe manually. Na mtu aliyefanya manually hakuona kwamba zile zina umuhimu wowote, akaziachilia mbali. Kwa hiyo hata kama ningekuwa natumia online account, nisingeweza kuona chochote.
Chakushangaza ni kwamba mtu wa mwisho niliyeongea naye aliyenitatulia tatizo haikumchukua hata masaa mawili kutrace hizo information kwenye intermediate servers. Sasa sijui siku zote nilikuwa naongea na vilaza ama nilikuwa nawakuta kwenye bad-mood, au nilitakiwa niwahonge ... sijui. Inawezekana mimi ndio mwenye mkosi ...
Aaaaghhhh!! Nilishajikatia tamaa zamaaaani!