CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CRDB Visa Card: Utata wa matumizi yake mtandaoni

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Manitoba, Jan 19, 2009.

 1. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #1
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kama una CRDB Visa Card, na ulikuwa unafikiria kuitumia kwenye internet, basi usithubutu kutia sahihi kuiwezesha kutumika mtandaoni (ila kama tu unajua unachokifanya).

  CRDB wametoa card mpya zenye nembo ya visa, ambayo wanatangaza kwamba unaweza kununulia vitu mtandaoni. Inaonekana kama ni bonge la wazo mpaka pale utakapogundua jinsi gani zisivyo salama hata kiduchu.

  Mtu yeyote mwenye namba ya kadi yako, pamoja na vile vinamba vitatu vya "usalama" vilivyo nyuma, anaweza kuitumia hiyo kadi yako kwenye mtandao bila tatizo lolote. Kwa hiyo ukiitumia kwenye tovuti ambayo si salama, basi ni kama umegawa namba yako kwa watu wengine kujihudumia.

  Pia ukiisahau kadi yako mezani, na mtu/rafiki yako/mtoto wako mtukutu/mpenzi wako/secretary wako akapata mda wa kunakili pembeni hizo namba zako, basi pia inakuwa imekula kwako.

  Kama ulikuwa unafikiria ile pin yako, basi sahau maana haina kazi kwenye mtandao.

  Address Verification
  Unaweza ukawa unajiuliza mbona kuna watumiaji wengi tu wa credit cards duniani na wasiwe na wasiwasi hivyo?

  Moja ya njia ambayo huwa inatumika kupunguza wizi wa kutumia kadi za wengine ni kufanya uhakiki wa anuani. Kiasi kwamba mtu akiweka oda ya kitu basi oda yake itakubaliwa na kadi kutumika ikiwa tu anuani ya ambapo vitu vya kwenye oda hiyo vitatumwa ni sawa na anuani ya mwenye kadi.

  Kwa CRDB hii feature wameifinya, kiasi kwamba mtu yeyote duniani anaweza kutumia kadi yako na kununua na kutuma vitu vyake sehemu yoyote duniani anavyotaka.

  Paypal
  Kutumia site kama www.paypal.com inaweza kusaidia kuondoa uwezekano wa mtu kukuibia namba za kadi yako online.

  Kujiunga kadi yako na paypal sio tatizo, tatizo ni jinsi ya paypal kuihakiki kwamba kweli ni ya kwako.

  Paypal wanachofanya ni kukuchaji fedha kidogo (wastani wa 2,000TZS), halafa katika muamala huo wanaweka namba ya siri fulani. Sasa wewe inabidi uangalie statement yako kutoka benki, uione hiyo namba, halafu uwape paypal. Assumption hapo ni kwamba hakuna mtu mwingine anaweza kuona statement yako zaidi ya wewe.

  Sasa ndani ya paypal unaweza ukakamilisha taratibu. Ukija CRDB ili kupata tu details za hiyo transaction, jasho litakutoka. Inaweza ukadhani ni kitu simple tu kupata details za transaction (hata mimi nilifikiria hivyo), lakini amini usiamini utashangazwa :) ... Nimefanya si chini ya trip 10 kwenda CRDB kwa ishu hiii, usihesabu simu, na nimetoka kupiga nyingine sasa hivi ... lol ...

  Ningetakiwa niwe nimeshakata tamaa ila tu nataka tu nifuatilie mpaka mwisho waniambie inawezekana au haiwezekani.

  Ila kama huu ndio utaratibu, sioni ni jinsi gani wataweza kuwahudumia wateja hata 100 tu wanaotaka kujiunga na paypal. Achilia mbali kwamba hawa watu 100 inabidi wapige kwata CRDB more that 10 times, halafu wawe wanapiga simu mara kwa mara kuwakumbushia CRDB case zao. Na mara nyingi watu unaoongea nao CRDB hata hawaelewi unazungumzia nini.

  Makubaliano yako na CRDB ni soo
  Ili kuiruhusu kadi yako kutumika online, itabidi utie saini makubaliano yako na CRDB, ambayo yanavipengele ambavyo vinaiondolea CRDB jukumu lolote la kukuhakikishia usalama wako unpotumia kadi yako kwenye mtandao. Kwa hiyo ukiwa online na kadi yako, jua you are on your own.

  Kwa watumiaji wengine duniani kuna taratibu za jinsi ya mtu kupinga kuchajiwa transaction ambazo hujazifanya wewe. Na kuna taratibu za jinsi gani utarudishiwa pesa zako.

  Mpkataba wa CRDB hauoneshi kama kuna kitu kama hicho. Kwa hiyo mtu akipata details za kadi yako, siku zote itakuwa inakula upande wako.

  Kwa hiyo baada ya kuutia saini tu nimehakikisha kadi yangu haiondoki machoni pangu, na pia nahakikisha akaunti hiyo ya CRDB haina vijisenti vingi ... mpaka ntakapomaliza hii exercise. :)

  Hitimisho
  Sasa hivi unaweza kutumia kadi yako ya CRDB kwenye mtandao, lakini you do it at your own risk, tena risk kubwa tu.

  Kinachonitisha ni kwamba kama kadi yako imewezeshwa kutumika kwenye internet, mtu hana haja ya kukuibia kadi nzima kwa sababu utashtuka, utaripoti, na kadi itafungwa. Anachotakiwa kufanya ni kupata namba za kadi zilizopo mbele, na vile vijinamba vitatu vilivyopo nyuma ya kadi, na inakula upande wako kimya kimya.

  Kama umeiwezesha kadi yako kutumika kwenye mtandao, na kama vijinsenti vyako kwenye akaunti yako sio vidogo, na kama huwezi kuitunza details za kadi kiasi hicho, ni vyema ungewaambia waizibe isitumike kwenye mtandao ... or u may have to learn the hard way.
   
 2. B

  Boney E.M. JF-Expert Member

  #2
  Jan 19, 2009
  Joined: Jan 22, 2007
  Messages: 425
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Katika hali kama hii ni vipi wadau watahamasika kununua hisa za CRDB wakati ikiingizwa katika soko la hisa? Hizi ni weaknesses ambazo bila ya kutafutiwa ufumbuzi zita-cast a shadow of doubt kwa customers kama pesa yao iko safe. Can U please educate me on this?
   
 3. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #3
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  Kuna wakati server ya crdb inayohusiana na hiyo ili crash watu wa nchi nyingi za asia walikuwa wanatoa pesa tu kwa wale waliokuwa wanajua jamaa walikaa kama siku 4 hivi mpaka mtaalamu wao walipokuja toka majuu

  walahi kazi ipo nakwambia
   
 4. tonge nyama

  tonge nyama JF-Expert Member

  #4
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 28, 2008
  Messages: 372
  Likes Received: 377
  Trophy Points: 80
  Wadau naomba mtufahamishe vizuri, je ni wakati gani unapoweza ama kuruhusu au kuzuia kadi yako kuweza kutumika mtandaoni je nipale unapo apply for the new card au wakati wa kuichukua? nimeomba kadi crdb baada ya niliyokuwa nayo ku-expire.
   
 5. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #5
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Wanaangalia kama benki inapata faida mwanawane. Na inapata faida. Kumbuka pesa zikiibwa hapo, ni zako ndio zimeubwa, wewe ndio umepata hasara sio wao ... tena wao watakuwa wametengeneza mapata kidogo kwa transaction hiyo ya wizi ... sasa sioni kwa nini hata wewe usiende wekeza huko :)
   
 6. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Walipoanza haya mambo ya kadi kutumika mtandaoni, ilikuwa kwamba unapewa kadi ikiwa tayari kutumika mtandaoni.

  Nadhani baada ya kugundua hizo loopholes ndio wakaweka utaratibu wa kukusainishe wewe makubaliano ambayo yanaiondolea CRDB wajibu wowote wa kukuhakikishia usalama wako, na hivyo hata ukiibiwa ni juu yako.

  Kwa hiyo ukipata kadi yako mpya hutaweza kuitumia mtandaoni mpaka usaini kale kamkataba kao. Kwa hiyo uko salama mpaka pale utakapotia saini kale kamkataba kalikokaa upande.
   
 7. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
  Nafikiri inategemea. Nimetumia mara kadhaa na hakuna shaka, na jamaa wengi nawajua wanatumia bila shaka. Kwa kufananisha, nimewahi ona mtu hapo Norway kapata kwenye account yake 6 billions NKR ikiwa inatoka na makosa ya Kibenki na vivyo hivyo kule Sweden kuna jamaa wa Moscow (Mrusi) alilamba zaidi ya SKR equivalent to USD 2 ml bila wenyewe kushtuka kwa mwaka mzima kwa kucheza na Credit Cards. Huyu Mrusi mpaka leo anatafutwa huku akiendeleza huo uzandiki. Zingine nyingi zinafahamika.

  CRDB VISA CARD haiwezi kuwa tofauti na hizi incidences. Ni pro and cons za technology. technology Inaweza kukubamiza au kukunyanyua.
   
 8. Lole Gwakisa

  Lole Gwakisa JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2009
  Joined: Nov 5, 2008
  Messages: 3,962
  Likes Received: 403
  Trophy Points: 180
  Thanks Manitoba, itakuwaje kutumia kadi yako kwa single transactions-yaani ukitaka kununua kitu kwenye mtandao unacharge akaunti yako na fedha zile tu zinazohitajika?
  Nimeona wengine wanatumia mtindo huu, imekaaje hapo mkuu!
   
 9. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mzee mimi nadhani wanao-design hizi technologies huwa wanashirikisha sana akili. Kama tungekuwa sisi basi ndio tungesema hivyo kirahisi tu kwamba "Inaweza kukubamiza au kukunyanyua". Lakini wenzetu wanashirikisha akili na kujitahidi kuhakikisha kuwa technolojia inasaidia zaidi kuliko inavoumiza.

  Sasa naomba nikupe fact mbili tatu ambazo pengine zitakubadili mawazo.

  Kwa wenzetu interests za mwenye kadi zinakuwa protected. Kwengine kunakuwa na jinsi ambayo mwenye kadi anaweza kuilalamikia transaction ambayo hakufanya yeye, na issuer wa card yake akaissue kitu chaitwa "charge back" ambapo mwenye kadi anarudishiwa pesa yake, na mtua huduma anakatwa hiyo pesa.

  Kwenye sehemu zenye utaratibu huu, anayeumia ni mtoa huduma na si mwenye kadi. Kwa hiyo hayo mabilioni unayoyatolea macho ni hasara zaidi kwa mtoa huduma kuliko kwa mwenye kadi.

  Utaratibu huo unahakikisha kwamba mtoa huduma anajiridhisha kwamba hiyo kadi ni halali na mtumiaji wake ni halali. Na njia za kufanya hivyo kwa kutumia technolojia hiyo hiyo zipo, na zinatumika huku duniani: si mapambo.

  Tofauti ya CRDB card hapa nikwamba mtu akitumia card yako ya CRDB, na ukaona transaction ambayo hukuifanya wewe, huna pa kulalamika. Maana yake CRDB ni kama wanasema ukiibiwa ni shauri yako. Yaani inawezekana hata kumtafuta mwizi wasikusaidie. :) Wakati kwa wenzetu ukiibiwa aliyesaidia wizi ndio anabanwa.

  Umeona hiyo tofauti?
   
 10. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #10
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Kutumia card ya CRDB kwenye mtandao ni wazo zuri. Na CRDB inabidi wapongezwe kwa hatu hiyo.

  Ninachosema hapa ni kwamba CRDB wamejitoa kwenye tatizo lolote litakalotokea kwa matumizi ya kadi yako. Kitu ambacho ni tofauti na kwa wenzetu kwa jinsi ninavyofahamu mimi.

  Hiyo inafanya matumizi ya hii card yawe na risk zaidi. Yaani hata kama kosa ni lakwao bado hakuna wa kukusaidia.

  Kwa mfano ukinunua kitu online halafu kwa bahati mbaya anayekuuzia akatoa fedha zaidi ya zile alizotakiwa kutoa. Halafu kwa bahati mbaya akawa anasuasua kukurudishia fedha zako. Hapo utakuwa huna jinsi ila kukubali umeliwa kimachomacho. Lakini kwa wenzetu kuna taratibu za kupinga transaction ambayo si sawa au si halali, na mwenye kadi waweza kurudishiwa pesa ambazo hukutakiwa kukatwa. Kwa CRDB inaonekana hakuna kitu kama hicho.

  Sisemi kwamba CRDB wanatakiwa waweke utaratibu kama huo. Ila nasema wewe mtumiaji ujue hali ilivyo, usije ukang'atwa siku ndio ukaanza kutoa macho na kuwa mkali na CRDB.
   
 11. Outlier

  Outlier JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2009
  Joined: Dec 28, 2008
  Messages: 325
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mimi nimetumia huduma hii kwa miezi sita na mpaka sasa sijapata matatizo na ukweli inarahisisha sana transactions zako. Zaidi ya kununua, unaweza pia ku-transfer pesa kwenda kwa mtu mwingine.
  Cha muhimu angalau ukumbuke kila siku kuingia mtandaoni na kuangalia salio lako.
  Mwanzo mgumu ila am confident "we" are progressing.
   
 12. Shadow

  Shadow JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2009
  Joined: May 19, 2008
  Messages: 2,908
  Likes Received: 71
  Trophy Points: 145
  Je kuna haja ya kuomba ushauri wa baraza la walaji? hii ndio kazi yao kumlinda mlaji. Mimi naona kuna haja ya kushirikisha baraza hili na si kukaa kimya.
   
 13. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2009
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kwa hili CRDB wamepiga hatua, ila nafikiri cost ya hii kitu itakuwa ni kubwa zaidi ya Benefit. Cha kufanya kwa wale wenye kutaka huduma hii ni bora kuwa na account mbili yaani Moja ni kwa ajili ya transaction za online, unahamisha pesa na kufanya transactions on spot, hapo hapo. Nyingine ni kuhifadhia pesa kama una wasiwasi
   
 14. M

  Mtu wa Kawaida JF-Expert Member

  #14
  Jan 19, 2009
  Joined: May 2, 2008
  Messages: 217
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Ni kweli kabisa. Hii itaondoa wasiwasi wa kwamba unaibiwa au watu wanachezea account yako.
   
 15. Kana-Ka-Nsungu

  Kana-Ka-Nsungu JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2009
  Joined: Oct 4, 2007
  Messages: 2,260
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 135
  Sielewi kwa nini CRDB wameifinya hiyo feature ya address, kwa kufanya hivi wenye account zetu tumekuwa more exposed to fraud. Au ndio wanataka kuutangazia ulimwengu mzima kuwa- watanzania hatuna address?
  Nisingemshauri mtu yoyote kutumia hii huduma for the time being hadi pale kutakapokuwa na uhakika kwamba kuna 100% protection kwa wateja na Bank iko tayari kuwa responsible pale ambapo kutatokea 'ufisadi'.
   
 16. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #16
  Jan 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 17. M

  Manitoba JF-Expert Member

  #17
  Jan 20, 2009
  Joined: Jul 8, 2008
  Messages: 240
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sawa kaka.

  Sisemi kwamba wewe ndio ulivyo, ila sisi tuna kawaida sana ya zima moto. Kwa sababu inafanya kazi, basi kheri. Yakianza kutokea matatizo, unaona kama muujiza na kulalama kwa nini benki yako haikulindi. Lakini pengine mtu ungejua ukweli ulivyo, mtu ungejua risks ziko wapi na ungekuwa makini zaidi na unachokifanya.

  Sadakta! Ndio maana nikasema, "usithubutu ila tu kama unajua unachokifanya".

  Wasiwasi wangu mkubwa ni kwamba kwa jinsi CRDB wanavyoitangaza kama vile hakuna risk yoyote, watu watazikurupukia na wengi wataumia.

  Bottom line is, know what you are doing.

   
  Last edited: Jan 20, 2009
 18. M

  Mwanjelwa JF-Expert Member

  #18
  Jan 20, 2009
  Joined: Jul 29, 2007
  Messages: 961
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
   
 19. C

  Caroline Danzi JF-Expert Member

  #19
  Jan 20, 2009
  Joined: Dec 19, 2008
  Messages: 3,629
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  Tehe tehe sisi wa vijijini tumepona maaan tumezoea kupanga foleni ya NMB, VISA wapi na wapi? Asante kwa taarifa incase tumepata na sisi fulsa hiyo tutakuwa makini.
   
 20. K

  Kinvaba Senior Member

  #20
  Jan 20, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nakushukuru sana Manitoba. Wahenga walisema, ukiona mwenzio ananyolewa, nawe tia maji. Kinga ni bora kuliko kutibu. Nawashauri wenzangu wote tunaotumia kadi hii ya CRDB tuwe makini, tusipuuzie kwani kilio kitakuwa mjukuu wetu. CRDB nao wanatakiwa kujibu maswali wanayoulizwa na wateja wao kuhusu usalama wa matumizi ya kadi hii, kwani kukaa kimya nako kunatoa mwanya kwa wateja wao na watu wengine kusema wanayoona yanawafaa
   
Loading...