CRDB ni Moja ya Benki zenye huduma mbovu sana

CRDB ni Moja ya Benki zenye huduma mbovu sana

kitengo cha FOREIGN TRANSFERS, au wanaopoke international money transfers ni wababaishaji sana....kawaida Telegraphic Money Transfer, kama umetumiwa kutoka nchi nyingine let's say Uingereza inapaswa pesa kuonekana kwenye account yako baada ya masaa 24 lakini hawa CRDB kwa sababu nisizozifahamu wanashikilia sana pesa za watu kabla ya kuwawekea kwenye account husika... Mimi nashangaa wanashikilia pesa za wateja kwa sababu gani? Ukienda mapokezi wanakwambia eti Value date bado.....huu ni wizi kabisa. Bank inanufaika kutokana na fees itakayokatwa kweny pesa zilizopokelewa hawana uhalali kabisa kushikilia pesa za mteja kabla ya kuzi release kwenye account yake. Sisi tunaolipwa kutoka nje tunapata shida sana unakuta pesa zimetumwa zaidi ya wiki hujazipata wakati ni kitendo cha masaa tu...

tupo makini na money laundering,lazima tujiridhishe kabla ya kukuwekea pesa zako,unadhani sisi Mkombozi unawekewa bilioni bila maelezo!
 
Uchagganization utaimaliza hii bank. Ilikuwa inapiga hatua nzuri sana.
 
naona malalaliko mengi,hawa CRBD waje kufungua thread yao hapo juu kama NMB.
 
Na ukiwakuta hao banktellah sijui du! wanapitapita mara huyu aende kuongea na yule mara wacheke na muda wote mpo kwenye foleni..!!
 
Mie naona wamiliki wa hizi bank wanakuwa wagumu kutoa ajira kwa raia ndo maana inafikia stage mtu mmoja anakuwa anafanya kazi zaidi ya mbili. Kwa hali hii hata concentration inakuwa zero.... Huwezi mtu uka handle kazi kibao kwa wakati mmoja... Watz wengi hawana ajira toeni post izo....
 
Yesu Wangu pumbavu hawa kabisa usinikumbushe hawa mbwa
Crdb ni bank mbaya haijali wateja
 
I
Kiufupi bank ya crdb wafanyakaz wake wavivu sana na wanapenda sana kusingizia system hasa mkoa wa tanga kwa sisi acount zetu tulifungulia mkoa mgine wanatupa tabu sana ukienda kutoa hela utawekwa wee unaambiwa subir tutume fax watujibu ulikofunguliwa mara wanakuambia leta elf 4 ya fax yaan ni upuuz mtupu

Wana dharau
Wadokozi -
Very slow
Walarushwa hasa wale Wa mikopo
Jeuri sana hawajali Wateja
Hawana supervisors kuweka mambo sawa kama kusimamia Huduma kwa Wateja ,
Unachukua namba lakini unakuta mwenzio kachelewa we kwenye foleni, mtu mmoja anaamua anabeba Pesa za watu 5 waliochelewa zaid yako unaendelea
Kusotaaa 😡😡😡
vyumba kuhudumia 8 lakini wanaohudumia waNaotoa /kuweka 2 tu

Wamelewa sifa wanavurunda na viti vyenyewe vya kupumzikia hakuna doooo
Hela yangu Mwenyewe inanitesa loh
 
kitengo cha FOREIGN TRANSFERS, au wanaopoke international money transfers ni wababaishaji sana....kawaida Telegraphic Money Transfer, kama umetumiwa kutoka nchi nyingine let's say Uingereza inapaswa pesa kuonekana kwenye account yako baada ya masaa 24 lakini hawa CRDB kwa sababu nisizozifahamu wanashikilia sana pesa za watu kabla ya kuwawekea kwenye account husika... Mimi nashangaa wanashikilia pesa za wateja kwa sababu gani? Ukienda mapokezi wanakwambia eti Value date bado.....huu ni wizi kabisa. Bank inanufaika kutokana na fees itakayokatwa kweny pesa zilizopokelewa hawana uhalali kabisa kushikilia pesa za mteja kabla ya kuzi release kwenye account yake. Sisi tunaolipwa kutoka nje tunapata shida sana unakuta pesa zimetumwa zaidi ya wiki hujazipata wakati ni kitendo cha masaa tu...

Nina refund nimetumiwa toka november hadi leo wameishikilia,
 
Mimi nina NBC na CRDB nakuhakikishia mkuu CRDB ni far better than NBC ,na sim banking ndio natumia sifiki bank kirahisi mambo yote namalizia home
 
Mimi nina NBC na CRDB nakuhakikishia mkuu CRDB ni far better than NBC ,na sim banking ndio natumia sifiki bank kirahisi mambo yote namalizia home

Mimi naona hii ni vita ya libiashara kama si ya kikabila
Mimi ni mteja kwa zaid ya 15yr sijaona tatizo kubwa kama navoskia hapa pamoja na kua na akaunt 4 lkn at least crdb is better
Siku hizi kuna tabia ya kutumia mitandao kuharibu biashara za wengne na zaid kuna watu wameanzisha vita ya kikabila kwenye mitandao; take care
 
Nina refund nimetumiwa toka november hadi leo wameishikilia,
Unasona kumbe matatizo haya yanawakumba watu wengi...Theory ninayoiona mimi hapa ni kwamba inawezekana wanapozishikilia pesa hizo huwa ni delaying tactic ya kuziingiza kwenye mzunguko wa kibiashara kabla ya kuziachilia...maana wanajua pindi tu waziachiliapo lazima uzidake kwenye ATM....kazi ya benki ni kucheza na pesa za wateja...Uzuri ni kwamba no matter how long watazishikilia eventually lazima watazi release tu!!!
 
Hii benki mwanzoni nilikuwa nikisiakia watu wanailaumu naona kama ni majungu ila nimekuja kuprove kwamba CRDB huduma zao sio nzuri kabisa, Nimefuatilia ishu ya simu benking wiki nzima sasa na wakati najaza fomu niliambiwa ni masaa 48 na kibaya zaidi ni uongo wa wafanya kazi wao kila kitu wanasingizia systeam ilikuwa mbovu, hata kalamu ikiisha wao ni systeam ilikuwa mbovu.

Unajaza fomu wanapoteza inabidi tena ujaze upya fomu, kwa kweli wajirekebishe.

Nilishatoaga ela visa kupitia barclayas alafu iyo ele haikutoka nilifuatlia paka kesho alafu ni wezi awa jamaa
 
CRDB Bank Plc wamejitahidi sana kwenye ATM, na sasa wamekuja wakala wao. Tanzania nzima kuna ATM ana ukikuta hazifanyi kazi kuna sababu nyingi sana. Inaweza kuwa mawasiliano, umeme, nk, kumbuka hivi vyote vipo nje ya hiyo Bank. Pia ukizunguka maeneo ya karibu karibu utawaona Mawakala ambao watakupatia pesa. Pia wana Agency Baking. Kama upo karibu na Posta kuna agent wao na ATM ipo. Nawashukuru sana.

Lingine CRDB Bank ni member wa Master/Visa ambapo Bank yeyote hapa TZ na kote duniani ni member wa Master/Visa unaweza kutumia ATM ama POS zao. Ukiwa na Card ya CRDB una uhakika wa kupata huduma pamahali popote duniani.

Labda mawasiliano kwenye ATM hazifanyi kazi, bado unasehemu nyingine ya kukupatia huduma, nayo ni simbanking. Kwa kutunia simbanking ya CRDB unaweza kumhamishia mtu mwingine pesa, kupeleka kwenye M-pesa, Tigopesa, Airtel Money nk, na ukaendelea kupata huduma. Kwenye Innovation nawakubali sana hii Bank. Ila wale wafanyakazi wazembe wawajibishwe.

Ukitoa pesa visa sometime hazitoki wakati mpunga ushakatwa kwny acount yako....mziki unaanza kwny kufatiloa iyo pesa sas mbona utajutaaaaa...utajaza form paka ufe mara uambiwe siku 40 mara ukirudi unaambiwa jaza tena usubirie siku 40 je iyo ela italipwa na faida? Why wanacheza na ela za watu na uwizi uwizi wa kujinga?
 
Ambacho wengi hawajui ni kuwa kuna mabadiliko ya kimfumo yanayotokana na uwezo na ubora wa graduates wa siku hizi. Ni very poor. Hii inaathiri kuanzia uwezo na umakiji wa Manager mpaka anayefanya kazi teller window.

Ni kweli CRDB ilikuwa bora ila sasa imeahuka sana ubora wake.

Huduma kwa mteja ndio eneo la maana sana kwa biashara kama ya benki ambayo inajengwa zaidi na TRUST. Unaweza kuwa unatoa huduma ndio, ila unaitoaje hiyo huduma? Unajali muda wa mteja? Unamsikiliza na kuelewa mteja kabla ya kuanza kumhudumia? Unapomhudumia unakuwa unamuonyesha mood gani, ya kama unatamani aondoke mbele yako? akiuliza kitu unajibu kama amekusumbua? Haya mambo yanahitaji mtu mwenye kitu kinaitwa people skills na communication skills. Zamani CRDB ilikuwa juu kwa mambo haya ila siku hizi ni ovyo.

Jaribuni Standard Chartered kama service charges mnakubaliana nazo. Wako smart wake watu.
 
Back
Top Bottom