CRDB ni Moja ya Benki zenye huduma mbovu sana

CRDB ni Moja ya Benki zenye huduma mbovu sana

katika benki zote zenye mkono wa serikali na mtandao nchi nzima CRDB inapata B. NMB -C na NBC- E. Mleta mada labda kama una jambo jingine lakn this is one of the best local banks in tz i stand to be correct!

mimi sifanyi kazi benki na sina agenda ila nimeandika kilicho nitokea, sawa?
 
katika benki zote zenye mkono wa serikali na mtandao nchi nzima CRDB inapata B. NMB -C na NBC- E. Mleta mada labda kama una jambo jingine lakn this is one of the best local banks in tz i stand to be correct!

Hapo umeziweka kwa vigezo vya huduma bora au wingi wa branch au kitu gani?
 
Pamoja na mapungufu madogomadogo mimi bado naamini kuwa CRDB Bado ni benki bora Tanzania.
 
labda inategemea imetumwa toka nchi gani, pesa ikitumwa toka Holland ndani ya siku 4 inakuwa ishaingizwa kwa account husika.
Mimi nafanya kazi na shirika la Norway kila wakinitumia hela CRDB wanazizuia kwa muda zaidi ya wiki sijui kwa nini....zamani wakati SIM BANKING imeingia nilienda azikiwe wakaniwekea app yao nilikuwa naweza kuona kabisa pesa kwenye account yangu lakini siwezi kufanya withdrawal ukiwauliza wanasema value date yao bado sasa najiuliza mbona watu wengine wanapokea zinaingia moja kwa moja? ni nini kinachochelewesha Hivi kuna sababu gani inaweza chelewesha TT toka tarehe 9 december siku ya jumanne mpaka leo hii tarehe 16???
 
sitakaa nisahau nilipokuwa nafuatilia VISA kadi..
niliipata baada ya miez 10

nilijaza form ya maombi si chini ya mara tatu sababu kubwa niliambiwa hazionekani maombi hayajatumwa, mara fail halionekani..

daahh..!!!
 
CRDB ni baadhi ya branchi ila branch zingine ni shida

Chasha ukitaka kupona jipu usilipake mafuta, LIPASUE. Taja jina la branch na hata mhudumu 'ikibidi' ili kuwasaidia wananchi na wenye Bank waweze kurekebisha hiyo hali.
 
sitakaa nisahau nilipokuwa nafuatilia VISA kadi..
niliipata baada ya miez 10

nilijaza form ya maombi si chini ya mara tatu sababu kubwa niliambiwa hazionekani maombi hayajatumwa, mara fail halionekani..

daahh..!!!

na ndo hicho nacho lalamikia hata mimi najaza fomu naambiwa masaa 48 kumbe fomu wamepoteza na kwa nini wapoteze fomu?
 
Chasha ukitaka kupona jipu usilipake mafuta, LIPASUE. Taja jina la branch na hata mhudumu 'ikibidi' ili kuwasaidia wananchi na wenye Bank waweze kurekebisha hiyo hali.

Mkuu wao wenyewe wanajua nisha hadi waandike email makao makuu kulalamika, si kwamba hawajui na hata wakiingia humu watajua alie post ni nani, nilikuwa nawatajia branch halafu wanaishia kusema ngoja tuwapigie tuwaulize kumbe hakuna kitu.
 
Hii benki mwanzoni nilikuwa nikisiakia watu wanailaumu naona kama ni majungu ila nimekuja kuprove kwamba CRDB huduma zao sio nzuri kabisa, Nimefuatilia ishu ya simu benking wiki nzima sasa na wakati najaza fomu niliambiwa ni masaa 48 na kibaya zaidi ni uongo wa wafanya kazi wao kila kitu wanasingizia systeam ilikuwa mbovu, hata kalamu ikiisha wao ni systeam ilikuwa mbovu.

Unajaza fomu wanapoteza inabidi tena ujaze upya fomu, kwa kweli wajirekebishe.

Mkuu Chasha,

Pole sana kwa mkasa uliokupata. Ukisoma kwa makini issue yako ni kwamba ulipata tatizo la simbank tu. Nani imani sio Bank yote ni mbovu ama branch zote zaidi ya 100 ni mbovu. Pale pale ulipopata tatizo ungeweza kuona uongozi wa branch na tatizo lako kutatuliwa bila ya kuleta JF. Na hili ndilo tatizo letu wengi Watz, tunapenda sana kulalamika ila hatufanyi juhudi kuhakikisha uzembe ule haujirudii tena. Hata kama aliyefanya kile kitendo afukuzwe kazi!! Ili wengine wajifunze
 
Jana nilisimama foleni mpaka miguu ikaanza kutumbukia tumboni...slow...dirishani yuko mmoja anahudumia makumi ya watu...wengine wana hela zao za kichina hazitoki mpaka kwa mazingaombwe ya wachina....basi tabu tupu. Seriously, bank zetu zinapaswa kuboresha uwezo wao wa kutumikia wateja.

Na mabank yaanze sasa kuwawezesha waajiriwa wao kuongezea skills kwa kuweka mandatory training za namna ya kuwahudumia wateja wao. Imagine toka mtu aajiriwe kuwa teller hakuna lolote analopata kumsaidia asogee mbele...atajari lini hiyo kazi?
 
Kwangu mimi wanachoniboa ni kutokuwepo hela kwenye ATM siku za weekends. Yaani siku ambazo watu tunakwenda shambani tunahitaji hela, wenyewe utakuta ATM zao hazina hela. Huwa nakereka sana.
Ila kwa huduma nyingine naona wanajitahidi, though NBC kwa sasa imeanza kufanya vizuri in terms of huduma hasa baada ya kukimbiwa kwa kasi na wateja.

CRDB Bank Plc wamejitahidi sana kwenye ATM, na sasa wamekuja wakala wao. Tanzania nzima kuna ATM ana ukikuta hazifanyi kazi kuna sababu nyingi sana. Inaweza kuwa mawasiliano, umeme, nk, kumbuka hivi vyote vipo nje ya hiyo Bank. Pia ukizunguka maeneo ya karibu karibu utawaona Mawakala ambao watakupatia pesa. Pia wana Agency Baking. Kama upo karibu na Posta kuna agent wao na ATM ipo. Nawashukuru sana.

Lingine CRDB Bank ni member wa Master/Visa ambapo Bank yeyote hapa TZ na kote duniani ni member wa Master/Visa unaweza kutumia ATM ama POS zao. Ukiwa na Card ya CRDB una uhakika wa kupata huduma pamahali popote duniani.

Labda mawasiliano kwenye ATM hazifanyi kazi, bado unasehemu nyingine ya kukupatia huduma, nayo ni simbanking. Kwa kutunia simbanking ya CRDB unaweza kumhamishia mtu mwingine pesa, kupeleka kwenye M-pesa, Tigopesa, Airtel Money nk, na ukaendelea kupata huduma. Kwenye Innovation nawakubali sana hii Bank. Ila wale wafanyakazi wazembe wawajibishwe.
 
Generally, CRDB huduma zao ni nzuri as compared na bank nyingine nyingi, hata kama kuna watu wanasema ati ''si bora kucompare afya yako na mgonjwa''. Of course kuna baadhi ya branches unaweza kukuta mtu mmoja au wawili wazembe/wapya etc na wanaweza kukukera. But kwa jumla, CRDB ni afadhari ya wengi.

Mimi sijawahi kupatwa na tatizo nao. Natumia internet banking, online purchaces etc na huduma ni bora sana. Hata kama kuna issues, nikiwasiliana nao huwa napata ushirikiano mkubwa sana na response huwa ni fast na ya uhakika
 
kama kimei yuko hapa ningemshauri hii bank aibadili na kuwa group of companies, aivunje aunde bank zingine tatu chini ya crdb group plc, bank moja ihudumie retail banking yaani maswala yote ya simbanking na salary loans, bank nyingine ishughulike na corporate banking na ya tatu ishugulike na investment banking.

huwezi sikia mtu akilalamikia BankM au citi bank kwani hawa wanadeal na corporate banking. lakini unapochanganya retail corporate na investment services katika dirisha moja inakuwa tabu kidogo.
 
kama kimei yuko hapa ningemshauri hii bank aibadili na kuwa group of companies, aivunje aunde bank zingine tatu chini ya crdb group plc, bank moja ihudumie retail banking yaani maswala yote ya simbanking na salary loans, bank nyingine ishughulike na corporate banking na ya tatu ishugulike na investment banking.

huwezi sikia mtu akilalamikia BankM au citi bank kwani hawa wanadeal na corporate banking. lakini unapochanganya retail corporate na investment services katika dirisha moja inakuwa tabu kidogo.

Ushauri wa kitaalam kabisa.
 
CRDB mimi nilienda kurenew card yangu ya bank tawi la singida, nilienda mwezi wa APRIL mwaka 2014, cha ajabu card yangu ilikua master card coz nilikua naitumia kununua vitu online sasa wenyewe wakasema hawatanipa master card na badala yake watanipa visa card, nikawauliza why wakasema ndio utaratibu wa bank yao.....

Tisa kumi, nimepeleka requirements zakupewa card nyingine tangu April lakin mpaka mwezi October sijapewa card, siku hiyo nikawabadirikia eti wakasema nijaze form upya coz yaweza kuwa nyaraka zangu zimepotea.....sasa kama makaratasi tu yanapotea inakuaje kwenye pesa zetu......?

Huo ulikuwa ni uzembe wa mtu mmoja tu, na sio rahisi kwa mteja kubadilishiwa kile anachokitaka. Mimi mwenyewe natumia card za hiyo Bank tatu, yaani Visa/Master na Gold card. Sijapata tatizo la kusumbuliwa. Haitakiwe izidi zaidi ya siku tano za kufanya kazi, card yako itakuwa tayari. Ukiona unasumbuliwa omba kuuona uongozi wa Branch na wakiendelea kukusumbua omba simu za Directors hata ukiingia kwenye website utaona uelezee tatizo lako.
 
Back
Top Bottom