Ngonalugali
JF-Expert Member
- Jan 12, 2008
- 659
- 102
Waheshimiwa, mnamkumbuka jamaa aliyepewa jina la MACHAPATI pale COMPLEX? Kama machapati unasoma thread hii naomba uni PM bwana, mimii nakukumbuka sana.
Sikonge, umenikumbusha mzee Shed!!
Kule paliiitwa beach bwana, kuna pafyumu ya kufa mtu, kuna jamaa alikuwa anavua nguo zote ili kuingia huko kutabaruki.
Na siku ya kula wali unavaa nguo za mapigano. Uji ukiwa hauna sukari na maharage yamejaa wadudu lakini mnagombania!
Sikonge na Ngonalugali - wazee wa Complex, mmnenikumbusha mbali sana. BTW wale watoto wenu mlowaacha pale kijijini Kikuyu sasa ni wakubwa, mnapeleka matumizi wakulu??
hahahahahaha umenikumbusha mbaaaaali miaka yangu yote shuleni sikuwahi kutumia maji lakini cha ajabu nikirudi likizo situmii makaratasi.........kuna wakati magodoro unakuta limenyofolewa wamekwenda kujiswafia.Siku ya Graduation pale Mazengo Sec mwaka 1985, kiongozi wa sherehe alikuwa mshikaji wangu Kasanga. Basi nilimfuata na Kisadolini changu na akanijazia Pilau. Pilau la Mazengo miaka hiyo lilikuwa kali sana. Kwa wenyeji wa Dodoma watakuwa wanamkumbuka Mzee Mapilau na yale Mapipa yake (SHABA). Nilikula siku hiyo hadi nikawa siwezi kuhema. Jamaa walishangaa kuwa mbona hawaoni tumbo kutokea. Basi kutoka siku hiyo nikajulikana kuwa nina tumbo kama la Mamba, linafutuka pembeni.......
Upuuzi wa Mazengo ilikuwa ni chooni. Utakuta mtu anapita koridoni na karatasi yake anaipekecha ili ilainike.... "pyeke pyeke pyeke..." na akitoka huko basi anapita kwenye ule mti nyuma ya bweni la Mwongozo na kujipigapiga na mtawi. Hii ilikuwa inasaidia kuuwa ile perfume uliyoikwaa kule NYUMBA KUBWA. Ule mti ulikuwa na harufu moja kali sana na ukitoka hapo unanukia freshi. Mabinti wa Msalato, mlivumiliaje ile harufu??
Siku ya Graduation pale Mazengo Sec mwaka 1985, kiongozi wa sherehe alikuwa mshikaji wangu Kasanga. Basi nilimfuata na Kisadolini changu na akanijazia Pilau. Pilau la Mazengo miaka hiyo lilikuwa kali sana. Kwa wenyeji wa Dodoma watakuwa wanamkumbuka Mzee Mapilau na yale Mapipa yake (SHABA). Nilikula siku hiyo hadi nikawa siwezi kuhema. Jamaa walishangaa kuwa mbona hawaoni tumbo kutokea. Basi kutoka siku hiyo nikajulikana kuwa nina tumbo kama la Mamba, linafutuka pembeni.......
Upuuzi wa Mazengo ilikuwa ni chooni. Utakuta mtu anapita koridoni na karatasi yake anaipekecha ili ilainike.... "pyeke pyeke pyeke..." na akitoka huko basi anapita kwenye ule mti nyuma ya bweni la Mwongozo na kujipigapiga na mtawi. Hii ilikuwa inasaidia kuuwa ile perfume uliyoikwaa kule NYUMBA KUBWA. Ule mti ulikuwa na harufu moja kali sana na ukitoka hapo unanukia freshi. Mabinti wa Msalato, mlivumiliaje ile harufu??
hahahahahaha umenikumbusha mbaaaaali miaka yangu yote shuleni sikuwahi kutumia maji lakini cha ajabu nikirudi likizo situmii makaratasi.........kuna wakati magodoro unakuta limenyofolewa wamekwenda kujiswafia.
Hii topic tangu niianzishe mimi ni vicheko tu. Wakuu naona mmekumbuka mbali sana. Interesting to read em commentsSikonge wewe ni noma, kumbukumbu yako sio mchezo.
Kuna kipindi magazeti yanaadimika kabisa, inakulazimu kuchana daftari la mtu.
Form I walikuwa wanakera maana walikuwa wanashindwa kilenga shimo. Ndama wengine wakiingia wanapanga magogo hadi mlangoni. Hapo inabidi mtu uingie chaka.
Nakumbuka nikiwa Form 1, tulikuwa tunafanya mtihani wa kiingereza basi baada ya muda wa mtihani kuisha mwalimu akasema wote wekeni kalamu chini, mimi kuangalia nilikuwa nimejibu maswali kama matano tu kati ya kumi na tano , basi tulivyoambiwa kila mtu alete mbele karatasi tulizofanyia mtihani mimi niliificha ya kwangu sikuikusanya kabisa. Siku mwalimu anarudisha makaratasi ya mitihani kwa wanafunzi na mimi nikamdai kuwa mbona mimi sijapata mtihani wangu, basi mwalimu alienda ofisini alitafuta bila kupata baade ikabidi anipe tu maksi akaniandikia 78%.
Wakuu mmesahau? Form 1 a.k.a njuka, amoeba, mswaki, single cell etc. alikuwa anapewa pesa kama dola moja hivi, anaambiwa alete paketi kadhaa za sigara na change juu! Maskini walikuwa wanaleta. Wakati mwingine kama Njuka hana pesa anaandikiwa barua kutuma kwa wazazi kuwa amevunja dining hall ikaangukia roll call kwa hiyo wamtumie pesa ya kulipia uharibifu huo. Au kwamba wazazi walisahau kumnunulia ameoba au hydra hivyo wamtumie pesa haraka kabla hajafukuzwa shule!