#COVID19 Covid 19 sio janga kubwa la mwisho, tujiandae na janga kubwa lingine - Bill Gates

Kwani yeye atabaki! !!alikwepo furauni Misri sembuse geti kila mtu ataondoka kwa kadri alivyopangiwa
Huyo bwege hatanii, si mmeleta ujinga kudharau chanjo zake? Sasa analeta third wave hio kiboko! Itachinja watu kama Ukimwi wa mwaka 88"
 
Habari wana Kijiji,

Katika pirika pirika za hapa na pale kusoma taarifa za habari, nimekutana na mahojiano aliofanya tajiri wa marekani mnamo tarehe 27 January 2021, tajiri huyo miongoni mwa matajiri wa dunia alipokua akihijiwa na The Cable, Bill Gates.

Katika mahojiano hayo, Bill Gates amesema kua dunia itapambana na milipuko ya majanga makubwa mengine, na kusisitiza Covid 19 halitakua janga la mwisho kubwa kuikumba dunia.

Bill Gates aliendelea na kusisitiza serikali zote duniani zinapaswa kuchukulia maanani zaidi na kujiwekeza zaidi katika system nzuri za afya (Invest more on Healthcare Systems) ili kuepusha vifo vitakavyoweza kuepukika kutokana na sekta za afya kuwa imara, kwani zisipo jiwekeza vizuri katika sekta za afya basi zitapambana na majanga makubwa mengine ya mlipuko.

Gates amesema mataifa yote, zikiwemo nchi za africa, zinakumbwa na vifo vingi sana kuliko vifo vya Covid 19 kutokana na sekta za afya kutokuwa imara.

Amesema (Nanukuu) "Vifo vinavyotokana na kukosekana kwa system nzuri za afya zinasababisha idadi kubwa sana ya vifo kila mwaka, kuliko vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid 19 huko africa. Hivo natumai kila mtu atachukulia maanani katika kujiwekeza zaidi katika system nzuri ya afya."

Tajiri huyo wa marekani amesema kuwa Covid 19 halitakuwa janga la mwisho, hivo serikali zinapaswa kujiandaa na janga lingine mapema kabla halijaripuka.

Amesema (Nanukuu) "Ukweli usiopingika ni kwamba Covid 19 inaweza ikawa sio janga kubwa la mwisho kuikumba dunia. Hatujui janga gani lingine litafatia na itakua lini, kama litakua ni Virusi Vya Corona, mafua, au gonjwa lingine ambalo hatujawahi kuliona au kulisikia."

" Tunachofahamu ni kwamba tunapaswa kujiandaa mapema kabla hatujakumbwa na mlipuko mwingine bila kujiandaa vizuri, wazo la janga lingine linapaswa kuwa ndani ya vichwa vyetu kila kukicha. Hivo tujiandae tusije tukakubwa wakati tumejisahau tena."


Bill Gates aliwahi kutabiri kwamba janga la Covid 19 linaweza kwenda mpaka mnamo mwaka 2022, licha ya hatua stahiki kuchukuliwa na baadhi ya serikali kupambana nalo kwa kuweka lock down pamoja na kutengeneza chanjo dhidi ya Covid 19. Pia ametabiri vifo zaidi ya 200,000 kuongezeka katika kipindi kijacho.

  • The Cable.
  • TCK.

View attachment 1688244
Huyu anayajuaje haya au ndiye muasisi wa majanga haya?
 
Hata sis tusio na akil tulishasemaga zaman kua covid imekua ishu sanaa sabab imegusa had wakubwa..lakin kitakwimu watu wanaokufa kwa ngoma au tb au malaria au homa za matumbo kwa siku africa ni kubwa mara mbili ya hao wanaokufa kwa covid....so yasiwe maneno meng..tuendelee na maisha

Covid imewatisha matajir wazung sabab walisha sahau kufa kwa magonjwa ya kuambukiza siku nying...ndomana imekua ishu..lakin kama ishu ya kufa tuu africa..tunakufa kinoma noma
 
Huyu anayajuaje haya au ndiye muasisi wa majanga haya?
Inawezekana kuwa kirusi cha COVID-19 kimetengenezwa maabara au lah. Ila siyo mara ya kwanza kuibuka ugonjwa hatari ambao binadamu hawakwuahi kuuona hapo kabla, mfano kipindi cha Bubonic plague a.k.a black death tena miaka ya 1340's ambapo binadamu hakuwa hata na uwezo wa kutengeneza kiumbe maabaara.
Ukaua watu kati ya milion 75-200. Ingekuwa sasa tungesema kauleta mzungu
 
Wazungu wamesavei wameona daa!! ngozi nyeusi haidhuriki na bacteria/virusi vya kibwegebwege. Maji ya mtoni ambayo hata hayajachemshwa, yanalambwa tu, no kuharisha wala kukohoa!, embe linanunuliwa sokoni, linasafishwa kwa ulimi halafu hiloo tumboni, no kuharisha wala kukohoa.
Sasa wanatafakari, hizi chanjo nani atanunua?
OK! Ongeza dozi ya virusi!!
 
Jamaa matamanio yake ni kuona dunia imebaki na watu tisa tu

As if yeye ataishi milele hapa duniani, wakati nalo litakufa tu kama linavyotaka wengine wafe. Akamuulize Hitler na ukatili wake wote aliishia wapi
 
Back
Top Bottom