#COVID19 Covid 19 sio janga kubwa la mwisho, tujiandae na janga kubwa lingine - Bill Gates

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,502
23,582
Habari wana Kijiji,

Katika pirika pirika za hapa na pale kusoma taarifa za habari, nimekutana na mahojiano aliofanya tajiri wa marekani mnamo tarehe 27 January 2021, tajiri huyo miongoni mwa matajiri wa dunia alipokua akihijiwa na The Cable, Bill Gates.

Katika mahojiano hayo, Bill Gates amesema kua dunia itapambana na milipuko ya majanga makubwa mengine, na kusisitiza Covid 19 halitakua janga la mwisho kubwa kuikumba dunia.

Bill Gates aliendelea na kusisitiza serikali zote duniani zinapaswa kuchukulia maanani zaidi na kujiwekeza zaidi katika system nzuri za afya (Invest more on Healthcare Systems) ili kuepusha vifo vitakavyoweza kuepukika kutokana na sekta za afya kuwa imara, kwani zisipo jiwekeza vizuri katika sekta za afya basi zitapambana na majanga makubwa mengine ya mlipuko.

Gates amesema mataifa yote, zikiwemo nchi za africa, zinakumbwa na vifo vingi sana kuliko vifo vya Covid 19 kutokana na sekta za afya kutokuwa imara.

Amesema (Nanukuu) "Vifo vinavyotokana na kukosekana kwa system nzuri za afya zinasababisha idadi kubwa sana ya vifo kila mwaka, kuliko vifo vinavyotokana na mlipuko wa Covid 19 huko africa. Hivo natumai kila mtu atachukulia maanani katika kujiwekeza zaidi katika system nzuri ya afya."

Tajiri huyo wa marekani amesema kuwa Covid 19 halitakuwa janga la mwisho, hivo serikali zinapaswa kujiandaa na janga lingine mapema kabla halijaripuka.

Amesema (Nanukuu) "Ukweli usiopingika ni kwamba Covid 19 inaweza ikawa sio janga kubwa la mwisho kuikumba dunia. Hatujui janga gani lingine litafatia na itakua lini, kama litakua ni Virusi Vya Corona, mafua, au gonjwa lingine ambalo hatujawahi kuliona au kulisikia."

" Tunachofahamu ni kwamba tunapaswa kujiandaa mapema kabla hatujakumbwa na mlipuko mwingine bila kujiandaa vizuri, wazo la janga lingine linapaswa kuwa ndani ya vichwa vyetu kila kukicha. Hivo tujiandae tusije tukakubwa wakati tumejisahau tena."


Bill Gates aliwahi kutabiri kwamba janga la Covid 19 linaweza kwenda mpaka mnamo mwaka 2022, licha ya hatua stahiki kuchukuliwa na baadhi ya serikali kupambana nalo kwa kuweka lock down pamoja na kutengeneza chanjo dhidi ya Covid 19. Pia ametabiri vifo zaidi ya 200,000 kuongezeka katika kipindi kijacho cha hili janga la Covid 19.

Screenshot_20210128-152853_Opera%20Mini.jpg
 
Ukiona hivyo jua kuna kirusi kingine kiko jikoni kinaivishwa kwa kasi ya 5G. Afrika tujiandae
Kuna toleo jipya linakaribia kutolewa muda si mrefu, limeanza kupigiwa promo kama matoleo ya "IPHONE/SAMSUNG au kama promo za Fiesta za DabliuuEsiBiii Wasafi" yanavyo pigiwa promo.

Afrika tujiandae, hasa kwa nchi zetu zenye viongozi wajeuri ndio tutatolewa kama "FOR EXAMPLE" kwenye hayo matoleo mapya yanayokuja.
 
Yaani moyo umenistuka baada ya bill gate kuongea janga lingine litatupata
Hawa jamaa maisha yetu wamegeuza biashara, unapigwa janga moja matata halafu unaambiwa uuziwe chanjo. Kifupi chagua utoe hela au ufe. Ni sawa na ujambazi wa kutumia bunduki.

Kama shida yao kutuondoa africa yote si watutandike bomu la NUKLIA AU HIROSHIMA tufe haraka, kuliko kututesa hivi kwa kutusukumia mara Ebola mara Covid 19 Pro Max.
 
Jamaa wanapambana kufanya utafiti wa chanjo halafu ukatae kununua dawa hapo wanaleta wanachokijua wao.

Inabidi waafrika tuamke na kuacha tegemezi la kila aina.

Hapo hajakosea ni bora kujikita na kuwekeza zaidi kwenye sekta ya afya.

Nchi nyingi masikini zinawekeza kwenye silaha kupambana na wanaowakosoa badala ya kuwa na afya bora.

Matokeo yake tutakuwa tegemezi tu na kama huna afya huwezi kufanya kitu.
 
Back
Top Bottom