Mshana Jr
Platinum Member
- Aug 19, 2012
- 269,634
- 697,916
Siasa majnuni zimetufundisha unafiki, uzandiki na rohombaya. Kuna turubai lingine laja
EL kaumwa na kuugua sana! Je, ni wangapi tulimwombea yeye na wagonjwa wengine wote? Watu wako busy na nyama choma na bia na zipu. Leo kila mmoja anakuja na machozi yake ya mamba! Wanafique wakubwa nyie
Zamani bibi yetu alifariki. Kifo chake kulikuwa sherehe kwakuwa hatimaye alipumzika tabu za dunia.. Alitwaliwa toka maisha haya akiwa na umri wa takribani miaka 121 hivi.
Miaka yake ya mwishoni alikuwa kama mtoto ni wa kubebwa muda Wote hawezi kusimama hawezi kutembea hawezi kula mwenyewe nk bila usaidizi
Mwanzoni hali hiyo ilimuumiza sana.. Mtu aliyezoea kufanya shughuli zake mwenyewe leo hawezi mpaka asadiwe.
Maisha yake yaligeuka ghafla na kuwa na kuwa mageni kwake, ndugu na marafiki wa kukumbushana mambo ya zamani, utoto wao, ujana wao nk! Wote hawakuwepo walishatangulia mbele za haki miaka mingi nyuma
Alitawaliwa na upweke mkubwa hakuna na watu wa kuongea naye, wa kuwa karibu naye. Kusimuliana mengi. Waliokuwepo walimfanyia kila kitu kwa upendo mkubwa lakini hawakuwa sehemu ya past yake!
Siku anaondoka duniani ilikuwa furaha badala ya huzuni. Kayaishi maisha yake.. Kaolewa na kujaaliwa watoto wengi wa kike na wa kiume! Wakasoma na kupata Kazi kisha wakapata na familia.
Akajaaliwa kuwaona wana wa wanawe.. Wajukuu vitukuu na vining'ina.. Mungu akupe nini tena.. Siku anafumba macho milele uso wake ulijawa na amani na tabasamu la ujanani.. Huku akiwa kazungukwa na wanafamilia waliokuwepo! Ni baraka kubwa!
Hakuna kitu chema kama afya na hakuna kitu kibaya kama ugonjwa hasa wa muda mrefu. Ugonjwa huharibu bajeti zote na ratiba zote! Ugonjwa hupangiwa bajeti yake mpya na wahudumu.. Ugonjwa huleta simanzi na majonzi ndani ya familia.
Siku MOJA ya mgonjwa aliyelala kitandani hajiwezi ni ngumu na ni ndefu kuliko hata ya wanaomhudumia
Mtu aliyeishi maisha yake kwa mafanikio makubwa kijamii, kifamilia, kitaifa, kimataifa, kifedha, kiimani nknk kama EL na mwishoni kupata udhaifu wa kimwili kwa muda mrefu. Siku akitwaliwa toka maisha haya inapaswa kuwa siku ya furaha kuu na si unafiki mkubwa wa wanasiasa kwamba.
. Wamepokea kifo chake kwa nshtuko mkubwa
. Taifa limepoteza mtu muhimu sana
. Pengo lake hakuna wa kuliziba nknk
Wengine wanaandika haya wakiwa kwenye dhambi za dunia na divai mkononi. Kama ratiba za maturubai hazitaingiliana basi tujifunze kuacha unafiki na machozi ya mamba.
Sanaa ya kifo

Hii ni habari ngeni kabisa kwa wale watakaobahatika kusoma hii mada na pia wale wenye kupenda kujifunza vitu vipya ni sanaa ya kifo katika uhalisia wetu bila kuchanganya na doctrines za kiimani na kiasili. Kwenye mada nyingi tumeona uhayawani wa mwanadamu tumeona kwa sehemu kubwa jinsi kiumbe...
www.jamiiforums.com
Sanaa ya kifo