Bill Gates "Afrika kuna njaa na Utapiamlo, Mazao ya GMO yatawasaidia. Je, hii si kauli ya dharau kwa Waafrika?

ChoiceVariable

JF-Expert Member
May 23, 2017
43,076
49,784
Ni lini Waafrica tutajitambua na kujipambania tuache kutukanwa na kudharilishwa kiasi hichi?
---
Bilionea maarufu duniani kutokea nchini Marekani Bill Gates anaeleza namna ambavyo mazao yanayotengenezwa maabara kwa kubadilishwa vinasaba 'GMO' (Genetically modified organism) yatakavyosaidia uzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika na kupunguza tatizo la njaa na utapiamlo.

Mpango wa bilionea huyo wa kuleta mazao ya GMO katika nchi za Afrika umeibua ukosoaji mkubwa kwa baadhi ya wadau wa Afya na mashirika ya kiraia kwa kile wanachodai kuwa mazao yanayotokana na kubadilishwa kwa vinasaba kupitia uhandisi wa jeni unaweza kupelekea athari za kiafya kwa watumiaji wa chakula hicho.

*Bill Gate anatetea mpango wa mazao ya GMO kwa hoja zake zifuatazo

-Bill Gate anadai endapo nchi zote za Afrika zitakubali matumizi ya mazao ya yanayotokana na GMO itawasaidia kupunguza tatizo la njaa na utapiamlo.

-Bill Gate anadai kuwa mbegu za GMO zinastahimili ukame na wadudu hivyo itasaidia uzalishaji mkubwa wa chakula.

Hoja za wadau mbalimbali na mashirika ya kiraia zinazokosoa mpango wa Bill Gates kuhusu kuleta mazao ya GMO Afrika.

- Wanadai mazao ya chakula yanayotokana na mbegu za GMO yanaweza kuwa na athari kiafya kama kansa, presha n.k huku wakitolea mfano wa ripoti katika baadhi ya nchi ambazo zimekwisha kubali mpango huo miaka kadhaa iliyopita kama Afrika Kusini na Kenya.

- Wadau wanadai kuwa mpango wa Bill Gate kuhusu matumizi ya GMO unaweza kupelekea kutoweka kwa mbegu asilia za mazao ya chakula, jambo litakalopelekea utegemezi wa mbegu kutoka makampuni ya Magharibi kama Monsanto, jambo hili litapelekea kutoweka kwa Usalama wa chakula barani Afrika kutokana na kutegemea mbegu za GMO kutoka mataifa ya magharibi.

Una maoni gani kuhusu mpango wa Bill Gates juu ya kuleta mazao ya GMO barani Afrika?
 
Hii imeenda tujiandae tu kama wanafadhili chuo cheti chakilimo SUA hapo kuna nini tena, na vyakula na mifugo kuna madawa ya kutosha leo ng`ombe na mbuzi wanakula chanjo za kutosha, kuku wengi leo tunao kula ni hao wamaabara kuku wetu wa kienyeji wanazidi kupotea na hakuna mkakati wowote .
 
Hivi nini hatari ya hizi mbegu za GMO?
 
Hivi ndio mahindi yalivyokuwa yanafana kabla wanasayansi hawsjayabadilisha
cornbrefimg.jpg
 
Hivi nini hatari ya hizi mbegu za GMO?
Huoni Wanaume wa Dar wakiwa na matiti, hipsi na hata sauti za kike?

Je homone imbalance kwa Me & Ke hata kupelekea changamoto za uzazi?

Ke wengi siku hizi hawana haiba ya kike kwa sauti, ndevu na mwonekano ni wa kiumeni tu.

Magonjwa ya kansa, kuoza kwa maini na figo ni kugusa tu.

Kuzeeka kwa haraka tokana na many chemical drinking ingredients in human beings.

Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
 
Ni lini Waafrica tutajitambua na kujipambania tuache kutukanwa na kudharilishwa kiasi hichi?
---
Bilionea maarufu duniani kutokea nchini Marekani Bill Gates anaeleza namna ambavyo mazao yanayotengenezwa maabara kwa kubadilishwa vinasaba 'GMO' (Genetically modified organism) yatakavyosaidia uzalishaji mkubwa wa chakula barani Afrika na kupunguza tatizo la njaa na utapiamlo.

Mpango wa bilionea huyo wa kuleta mazao ya GMO katika nchi za Afrika umeibua ukosoaji mkubwa kwa baadhi ya wadau wa Afya na mashirika ya kiraia kwa kile wanachodai kuwa mazao yanayotokana na kubadilishwa kwa vinasaba kupitia uhandisi wa jeni unaweza kupelekea athari za kiafya kwa watumiaji wa chakula hicho.

*Bill Gate anatetea mpango wa mazao ya GMO kwa hoja zake zifuatazo

-Bill Gate anadai endapo nchi zote za Afrika zitakubali matumizi ya mazao ya yanayotokana na GMO itawasaidia kupunguza tatizo la njaa na utapiamlo.

-Bill Gate anadai kuwa mbegu za GMO zinastahimili ukame na wadudu hivyo itasaidia uzalishaji mkubwa wa chakula.

Hoja za wadau mbalimbali na mashirika ya kiraia zinazokosoa mpango wa Bill Gates kuhusu kuleta mazao ya GMO Afrika.

- Wanadai mazao ya chakula yanayotokana na mbegu za GMO yanaweza kuwa na athari kiafya kama kansa, presha n.k huku wakitolea mfano wa ripoti katika baadhi ya nchi ambazo zimekwisha kubali mpango huo miaka kadhaa iliyopita kama Afrika Kusini na Kenya.

- Wadau wanadai kuwa mpango wa Bill Gate kuhusu matumizi ya GMO unaweza kupelekea kutoweka kwa mbegu asilia za mazao ya chakula, jambo litakalopelekea utegemezi wa mbegu kutoka makampuni ya Magharibi kama Monsanto, jambo hili litapelekea kutoweka kwa Usalama wa chakula barani Afrika kutokana na kutegemea mbegu za GMO kutoka mataifa ya magharibi.

Una maoni gani kuhusu mpango wa Bill Gates juu ya kuleta mazao ya GMO barani Afrika?
Hakuna uongo, ila labda solution yake ndio tatizo. Hata kule kijijini, sehemu yenye mvua na mashamba ya kutosha, bado kuna familia zinalia njama. Afrika tumerogwa.
 
Back
Top Bottom